Ndugu zangu watanzania,
Baada ya matarajio ya Chadema kuwa tofauti na kupokelewa tofauti na watanzania na kupuuzwa na watanzania katika harakati zao kutokana na kukosa hoja na Sera za kuwashawishi na kugusa maisha Yao wameanza kuwatupia watanzania lugha za udhalilishaji kwa kusema watanzania Ni waoga na wavivu.
Chadema wameanza mikutano Yao kwa porojo pasipo Sera Wala ajenda Wala hoja zenye kugusa maisha ya watanzania na kufikiri kuwa ndio Mahitaji ya watanzania na kupelekea kukosa uungwaji mkono, kutokana na kukuta kazi kubwa imefanywa na mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani.
Shida ya watanzania siyo katiba mpya na Wala ukija vijijini kwetu huku Hakuna anayelia Wala kuwa na mahitaji ya katiba na Wala hawana habari na katiba na Wala haiwagusi katika suala la mbolea ,Bei za mazao yao Wala Elimu au Afya au Miundombinu au ajira kwa vijana vitu ambavyo Rais Samia amevigusa na kuvipatia majibu yaliyoleta Tabasamu mioyoni mwao na kuinua matumaini kwao.
Jiulize wewe unayesoma hapa kuwa Ni lini mama yako au Bibi yako kule kijijini alikuomba umtumie katiba? Lini alikuomba umtumie na kumsaidia kuipata rasimu ya warioba?
Hayo siyo Mahitaji ya watanzania ndugu zangu,Mahitaji ya watanzania Ni Yale ayafanyayo Rais Samia na serikali yake Kama vile kuwapatia watanzania maji Safi na salama,Elimu bure na Bora,ajira na mikopo ya Elimu ya juu kwa vijana,mbolea za Ruzuku,huduma Bora za Afya,uwepo wa madawa mahospitalini,vitendea kazi na wataalamu wa Afya,mazingira mazuri ya biashara,maslahi Bora na mazingira mazuri kwa watumishi wa umma,kutendeka kwa haki kwa kila mwenye kuhitaji haki,Usawa katika utolewaji wa huduma na mgao wa keki ya Taifa.
Sasa baada ya kuwa Rais Samia amekata kiu ya watanzania kwa kuwapatia wanachohitaji na kupata uungwaji mkono iliyopelekea watanzania kuwatupilia mbali wapinzani, imepelekea chadema wachanganyikiwe na kuanza kuwatukana watanzania bila sababu za msingi,Nasema na bado maana Moto wa mama Samia utachoma kila kichaka na kuteketeza vyama vyote vya kibabaishaji vilivyokuwa Kama miradi ya watu kujipatia Ruzuku,vinakwenda kusambaratika muda siyo mrefu.
Kazi Iendeleee , mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627