Mbuge Flatei Massay apiga sarakasi Bungeni kuonesha kulalamika kuhusu ahadi anazopewa kila mara bila kutekelezwa, afanya marejeo ya sauti za mawaziri

Ukipinga bajeti unatakiwa kukabidhi kadi ya chama mlangoni wakati wa kutoka, katiba ya ccm inasema hivyo.
 
Mheshimiwa mbunge ana haki kabisa ya kupiga sarakasi ili kuonyesha hisia zake kwa jambo linalowakera watu wa jimboni kwake.
Mlioko mijini sasa hivi mnajengewa barabara za gorofa wakati huku vijijini wakati wa masika wototo wetu inabidi wavuke mito kwa mitumbwi, na akina mama wajawazito wanajifungulia majumbani tu bila kupata huduma za afya kwa kuwa barabara hazipitiki.
Hako kasungura (keki ya taifa) inabidi kagawanywe kwa uwiano mzuri ili sote tufaidike.
 
Ndio maana mna muongelea humu...message imefika kwa wahusika, niliwahi ona bunge la Thailand ngumi zilipigwa vibaya sanampaka spika akatoka mbio
 
Ukipinga bajeti unatakiwa kukabidhi kadi ya chama mlangoni wakati wa kutoka, katiba ya ccm inasema hivyo.
ndio maana wanalazimishwa kura za wazi, lakini wao ni wawakilishi wa wananchi sio chama
 
Amelipwa posho ajili ya kwenda kufanya maigizo huku watu wanashida
 
Walinda legacy mpo?

Huo ndio urithi mlioachiwa na dikteta .
 
Hayo ni matokeo ya Wanaoongoza nchi toka uhuru kudhindwa kufanya hayo.
 
Watu wengine bhana cjui mkoje, Ety mnasema hajielewi. Sasa mlitaka afanye jambo gani ili serikali imuelewe.? Mbona chadema walikuwa wanatoka nje huku kikao cha bunge kinaendelea, je tuseme nao hawana nidhamu mbele ya bunge.?
Acha kuleta mifano yakijinga ili kutetea ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…