Mbuge Flatei Massay apiga sarakasi Bungeni kuonesha kulalamika kuhusu ahadi anazopewa kila mara bila kutekelezwa, afanya marejeo ya sauti za mawaziri

Mbuge Flatei Massay apiga sarakasi Bungeni kuonesha kulalamika kuhusu ahadi anazopewa kila mara bila kutekelezwa, afanya marejeo ya sauti za mawaziri

na hizo sarakasi zote lakini utashangaa bajeti inapita kwa kishindo maana ndio usanii wao huo kila mwaka wa fedha. Mimi katika moja ya vitu ninavyotamani katika kupata katiba mpya ni wananchi kupewa nguvu ya kikatiba kuwawajibisha wawakilishi wao pale wanapoona ameshindwa kutimiza ahadi/malengo waliyojiwekea kuondoa huu usanii wa wawakilishi kuwakilisha vyama na sio wananchi kama ilivyokua kwenye rasimu ya warioba
Ukipinga bajeti unatakiwa kukabidhi kadi ya chama mlangoni wakati wa kutoka, katiba ya ccm inasema hivyo.
 
Mheshimiwa mbunge ana haki kabisa ya kupiga sarakasi ili kuonyesha hisia zake kwa jambo linalowakera watu wa jimboni kwake.
Mlioko mijini sasa hivi mnajengewa barabara za gorofa wakati huku vijijini wakati wa masika wototo wetu inabidi wavuke mito kwa mitumbwi, na akina mama wajawazito wanajifungulia majumbani tu bila kupata huduma za afya kwa kuwa barabara hazipitiki.
Hako kasungura (keki ya taifa) inabidi kagawanywe kwa uwiano mzuri ili sote tufaidike.
 
Ndio maana mna muongelea humu...message imefika kwa wahusika, niliwahi ona bunge la Thailand ngumi zilipigwa vibaya sanampaka spika akatoka mbio
 
Mbuge wa Mbulu ameoneshwa kukerwa hadi kuamua kupiga sarakasi bungeni bila kujali uwepo wa spika

Ni sawa mmbuge kupiga sarakasi au mweleka kuonesha kukerwa na ahadi zizizo tekelezeka?

===

Kuruka sarakasi kwa mbunge Flatei ni jambo analotamani kulifanya mara nyingi, Mei 17, 2021 pia alipokuwa akilalamikia matatizo ya jimboni kwake aliomba kuruka sarakasi ili kuonesha kuwa ametumwa na wananchi wake kuwasemea.

Kabla ya kuruka sarakasi, Mbunge huyo wa Mbulu alifanya marejeo kwenye kishkwambi chake ya sauti zilizorekodiwa za waziri wa ujenzi na naibu wake wakitoa ahadi kwenye vikao vya Bunge vilivyopita za kukamilisha ujenzi wa barabara Mbulu jambo ambalo halijatimizwa hadi sasa.

Pia soma: Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay almanusura kupiga sarakasi Bungeni ili ajengewe barabara jimboni

Amelipwa posho ajili ya kwenda kufanya maigizo huku watu wanashida
 
IMG-20220524-WA0061.jpg
 
Mheshimiwa mbunge ana haki kabisa ya kupiga sarakasi ili kuonyesha hisia zake kwa jambo linalowakera watu wa jimboni kwake.
Mlioko mijini sasa hivi mnajengewa barabara za gorofa wakati huku vijijini wakati wa masika wototo wetu inabidi wavuke mito kwa mitumbwi, na akina mama wajawazito wanajifungulia majumbani tu bila kupata huduma za afya kwa kuwa barabara hazipitiki.
Hako kasungura (keki ya taifa) inabidi kagawanywe kwa uwiano mzuri ili sote tufaidike.
Hayo ni matokeo ya Wanaoongoza nchi toka uhuru kudhindwa kufanya hayo.
 
Watu wengine bhana cjui mkoje, Ety mnasema hajielewi. Sasa mlitaka afanye jambo gani ili serikali imuelewe.? Mbona chadema walikuwa wanatoka nje huku kikao cha bunge kinaendelea, je tuseme nao hawana nidhamu mbele ya bunge.?
Acha kuleta mifano yakijinga ili kutetea ujinga.
 
Back
Top Bottom