Mbunge Ally Kessy: Road licence ihamishiwe kwenye mafuta(petrol & diesel)

Ahh sawa mkuu
 
Kutakuwa na vituo vya aina mbili. Vtuo vya mafuta vya wenye vyombo vya moto (gari,pkpk nk), Na vituo vya mafuta kwa ajili ya majenereta na vifaa vingine visivyotembea baraabarani????
haitawezekani,,, italeta suala la vituo haramu/ feki vya mafuta.,,
 
Iliwashika papaya. Hii ni baada ya Gvt & TRA KUWA DIGITAL hakwepeki. Ukuweka kwenye mafuta walio na mitambo isiyotembe barabarani vipi
Mafuta yatapanda
Vipi mkiendelea na utaratibu huo kwani kama Gari haetembe report police na TRA
 
Wacha kuongea vitu vya kufikirika wapi wanatumia mafuta ya nchi jirani? Au unaongelea hizo gari mbili mpakani.
 
Kutakuwa na vituo vya aina mbili. Vtuo vya mafuta vya wenye vyombo vya moto (gari,pkpk nk), Na vituo vya mafuta kwa ajili ya majenereta na vifaa vingine visivyotembea baraabarani????
Ndugu yangu umetisha kwani hata mwenye mashine yakukata majani atalazimika kulipia ROAD LICENCE!!!
 
Ndugu yangu umetisha kwani hata mwenye mashine yakukata majani atalazimika kulipia ROAD LICENCE!!!
Ndo mawazo ya wawakilishi wetu, halafu wanahimiza kilimo cha umwagiliaji, lile pampu nalo litalipa road licence.
 
Wacha kuongea vitu vya kufikirika wapi wanatumia mafuta ya nchi jirani? Au unaongelea hizo gari mbili mpakani.
Mbona umekuwa Mkali katika Jambo la kawaida sana?

Si uulize ili tukuelekeze namna Magendo ya Mafuta yanavyoungia na kutumika Nchini bila ya kulipiwa kodi?

Moja ya maeneo hayo ni Ununio na Mwambao watoe wa Ufukwe wa Bagamoyo
 
NINAUNGA MKONO HOJA 100%. KUNA KIJANA ALIACHIWA CANTER TRUCK MIAKA 5 ILIYOPITA. ILIKUWA YA URITHI BAADA YA BABA YAKE KUFARIKI,WAKATI HUO AKIWA NA MIAKA 14. ILIPAKIWA HADI AMALIZE SEKONDARI. MWAKA JANA KAMALIZA SHULE, KAIFANYIA SERVICE AANZE KUITUMIA,KADAKWA NA JAMAA,WA KODI ANADAIWA ALMOST 4M DENI HUKU HAIJATEMBEA WALA KUFANYA KAZI YOYOTE! SIJAJUA KAMA ATAIUZA ALIPE DENI AU VIPI.
KWA HIYO WAZO HILI LIKIPITA,LITAOKOA WENGI,NA SERIKALI ITAPATA MAPATO ZAIDI.
 
Iliwashika papaya. Hii ni baada ya Gvt & TRA KUWA DIGITAL hakwepeki. Ukuweka kwenye mafuta walio na mitambo isiyotembe barabarani vipi
Mafuta yatapanda
Vipi mkiendelea na utaratibu huo kwani kama Gari haetembe report police na TRA
Ili kuondoa mkanganyiko, hiyo kodi inaweza kupewa jina lingine kama issue ni jina "road". Kwani mitambo inayotumia diesel au petrol nje ya magari,hailipi kodi? Kama nh hivyo,dawa ni ku harmonize zile kodi kupitia bei ya nishati ya mafuta.
 
Kodi ya road license kukatwa kwenye mafuta ni wazo murua kabisa,unajua Yale makodi mengine yalikuwa yanagongana unapolipa Kodi ya nyumba au school fees,so ilikuwa mzigo kwakweli ila kama itakuwa unalipia kidogo kidogo kwenye mafuta itakuwa haiumizi sana itakuwa kama ongezeko LA bei ya mafuta tu.
 
Ki ukweli ukitafakari kwa umakini utaona waliotufikisha hapa ndio hao hao wanaojifanya kutuonea huruma..yaani vinyago tumechonga wenyewe Leo vinatutisha..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…