Mbunge wa Jimbo la Same mashariki, Anne Kilango Malecela akizungumza Bungeni leo Juni 22, 2026, amewataka Wazazi kuchukua Jukumu la kuwale watoto hasa katika kipindi cha umri wa 0 hadi miaka 18 ikiwa ni kipindi cha kumjenga Mtoto Kiakili.
"Nina wasiwasi na malezi na makuzi ambayo tunawapa watoto kipindi cha cha umri wa sifuri mpaka miaka 18. Ndio maana nasema naomba niongee na Watanzania.
Kipindi hiki ndio tunapotengeneza marais, ndipo tunapotengeneza mawaziri, ndipo wanapotengenezwa wabunge, ndipo wanapotengenezwa makahaba, ndipo wanapotengenezwa majambazi, ndipo wanapotengenezwa wauaji.
Nawaomba Watanzania waangalie kipindi cha sifuri mpaka 18 ndio sisi sote. Mheshimiwa mwenyekiti, mimi ninasema ukweli, wazazi hatuwapi nafasi watoto. Kipindi cha sifuri mpaka miezi 18 hatuwaangalii watoto vizuri. Watoto wanaangaliwa na mabajaji, wanaangaliwa na bodaboda, wanaangaliwa na mayaya, wanaangaliwa na wasichana wa kazi.
Wazazi hatuwapi nafasi watoto. Tunabaki kulalamika oh nchi ina majambazi, nchi incha, tunawaangalia watoto?