Mbunge wa Momba Condester Michael Sichalwe ametolewa ndani ya ukumbi wa Bunge ili akabadilishe mavazi yake baada ya Mbunge wa Nyangw'ale Hussein Nassor Amar kuomba muongozo wa Spika kuwa kuna baadhi ya Wabunge wamevaa mavazi yasiyo na maadili.
Spika baada ya kumuamrisha kuondoka Bungeni pia aliwaambia askari wa Bunge, kuanzia sasa mbunge yeyote atakaevaa mavazi yasiyo na Staha na kinyume na kanuni waishie getini. Sakata hilo lilianza kwa mbunge mwenzake kuomba muongozo wa spika akimtolea mfano kama mbunge aliyevaa mavazi yasiyo na staha.
Mbona haijabana!!!! Hao wazee vipi!!!! Yaani inaonyesha aina ya wabunge tulio nao. Watajadili masuala muhimu ya taifa kweli? Ubaya wa hiyo suruali sijauona kabisa!!!! Wazee wasichaguliwe kuingia bungeni!!!!