Mbunge Condester Michael atimuliwa Bungeni kwa kuvaa ovyo. Spika awaagiza askari wa bunge kuwazuia getini wavaa ovyo

Mbunge Condester Michael atimuliwa Bungeni kwa kuvaa ovyo. Spika awaagiza askari wa bunge kuwazuia getini wavaa ovyo

Pameibuka tabia ya wabunge wa viti maalumu kuvaa vinyela momo(skin tight) wawapo kwenye vikao vya bunge, hii haikubaliki.

Ukivaa kimnyelala momo basi vaa gauni juu yake ili kulinda heshima na utamaduni wa kitanzania.

Ni angalizo tu.

Picha tafadhali !
 
Hivi hiyo mibichwa yenu huwa inawaza kabla ya kupost? Wewe umeambiwa mbunge aliyetoa hoja ni wa Nyang'wale umekurupuka huko bila kuchamba umeanza na wapemba. Ukiona kofia tuu huwazi mara 2.Pumbavu sana
Huyo mbunge ni wa jimbo LA Nyang'hwale mkoa wa Geita.
 
Huyu Mbunge katuaibisha sana wana Momba, yaaani badala ya kuvaa nguo zinazo endana na Bunge letu tukufu yeye anavaa nguo za casino!!
Hata kama hujaolewa lkn unapaswa ujiheshimi.

lkn pia kama alivyo sema Spika kuwa kuna kina MAMA pia huvaa nguo zisizo na heshima wala adabu.
unavaaje suruali imeshika makalio na mapaja halafu unaenda BUNGENI?!! huo ni utovu wa nidhamu na kulikosea heshima jengo la Bunge.

Sehemu zenye Heshima ambazo hatutegemei Mwanamke mwenye kujiheshimu kuvaa mavazi ya ajabu ni;

1. IKULU
2. JESHINI
3.BUNGENI
4.MAHAKAMANI.
maeneo yote hayo niliyo tlyataja hapo juu yanaongozwa na nidhamu za mavazi.
ukitaka kuvaa vimini vyako na tight nenda casino.

Spika katoa maelekezo kuwa kuanzia kesho yeyote atakaye kuja Bungeni huku amevaa nguo zilizo bana makalio asiruhusiwe kuingia getini, lkn pia tunawaomba wawe wanaturushia picha zao ili tuwaweke kwenye orodha mwaka 2025.
Kaka siyo huyo mbunge wenu tu, bado kuna huyu pia sijui unasemaje hapo, hii no tabia yao tena imejengeka haswa, utaendaje bungeni namna hii?

E2zZUU5XMAQVG9B.jpg
 
Nikajua labda shati limebana nyonyo kweli kifua kimetuna, suruali tight hips lote njee nje; kumbe matatizo binafsi tu ya huyo mzee hivi utasemaje yale mavazi hayana maadili.
 
Nikajua labda shati limebana nyonyo kweli kifua kimetuna, suruali tight hips lote njee nje; kumbe matatizo binafsi tu ya huyo mzee hivi utasemaje yale mavazi hayana maadili.
kanuni zinazo ongoza JENGO LA BUNGE ndio zinakataza nguo za kuchora shepu, sio spika wala mbunge aliye sema.

wabunge wetu haswa wanawake wakae wajitathimini, maaana Spika kasema kuna hata kina mama watu wazima wanavaa nguo za disco wanatinga nazo mjengoni.
 
hata hivyo inaonekana kuna baadhi ya wabunge watukutu ama hawatambue lengo lao la kuwa bungeni.
nakumbuka Spika alionya na kutahadharisha siku za mwanzoni tu wakati Bunge linaanza tu. hata mm ambaye sio mbunge nazifahamu kanuni sembuse wao.!
 
kanuni zinazo ongoza JENGO LA BUNGE ndio zinakataza nguo za kuchora shapu, sio spika wala mbunge aliye sema.

wabunge wetu haswa wanawake wakae wajitathimini, maaana Spika kasema kuna hata kina mama watu wazima wanavaa nguo za disco wanatinga nazo mjengoni.
Hizo picha ukiziangalia kuna shape yeyote unayoona hapo zaidi ya ngozi yake ya shingo na juu ya kifua kidogo (sehemu ambazo hata mama zetu wanaacha wazi kulingishia mikufu yao).

Labda kama hiyo kanuni inasema nguo za kike ziwe ‘top necks jewel’ only hapo ndio kuna kosa.

Walinzi wa kike wa mama Samia kaunda zao tight kuliko za huyo mmbunge, wanavaa suruali na masharti umbile lote nje nje.
 
Mbunge wa Momba Condester Michael Sichalwe ametolewa ndani ya ukumbi wa Bunge ili akabadilishe mavazi yake baada ya Mbunge wa Nyangw'ale Hussein Nassor Amar kuomba muongozo wa Spika kuwa kuna baadhi ya Wabunge wamevaa mavazi yasiyo na maadili.

Spika baada ya kumuamrisha kuondoka Bungeni pia aliwaambia askari wa Bunge, kuanzia sasa mbunge yeyote atakaevaa mavazi yasiyo na Staha na kinyume na kanuni waishie getini. Sakata hilo lilianza kwa mbunge mwenzake kuomba muongozo wa spika akimtolea mfano kama mbunge aliyevaa mavazi yasiyo na staha.




Naona sasa wanaume ndiyo tunafuatilia wanawake wamevaa vipi! Sijasikia mwanamke yeyote kaongea🤔 mambo ya kike kufuatilia wanawake
 
haiongezi chochote wala haipunguzi chochote, na hizo sio suala la msingi sana kulifanya bungeni kuliko kufanya mambo yenye maslahi mapana kwa wananchi. wabunge wana nini cha kujivunia? tabia njema? wakati wakitoka pale getini wanafanya mambo ya ajabu, mioyo imejaa uchafu ila kwa nje ndio wanataka wajifanye wasafi? watu kibao hao wanaloga, wanakula hadi uchafu wa ajabu ili wapate huo ubonge, kila mtu hapo ana siri zake, halafu wanataka kujifanya watakatifu? wakitoka tu kwenye geti hapo hata hao wengine wanavaa nguo za ajabu na wanafanya mambo yakifirauni balaa. ngoja mtu aishi vile alivyo moyoni, sio kwa kuigiza. na hivyo ndivyo sote twahukumiwa hata mbele za Mungu.

Mkuu, kwani hili swala la mavazi hawakua na taarifanalo hapo kabla?
 
Huoni ukiwa umevaa vazi la hijab na baibui hakuna mwanaume atakae kutamani!!!!! Lakini dada zenu mnawaachilia hovyo na vinguo vinaonyesha ndani, chupi, sidilia, mipaja yote wazi, nywele zimesimama kama mwendawazimu, kiufupi nguo mnazowaachia dada zenu/mama zenu ni aibu, na ndiomaana wana shawishika kwa wanaume na hupelekea kubakwa na kutongozwa. Hii sio sifa ya mwanaume kuwaachia dada/mama zako wakijiachia. Watu wa ajabu nyie sijapata kuona, mpo kidunia zaidi.


Wangelikuwepo wakina ottoman empire/Sultan/Eturgrul n.k mngenyooka tu.
Nyie mawazo yenu ngono tu. Hamuwezi ku imagine mtu anaweza kum admire mwanamke alivyopendeza bila kumtaka kingono? Au kuwa mwanamke ana haki na uwezo wa kumkatalia mtu akimtongoza.

Basi wanawake wenu wasiingie kabisa bungeni ili tusiwatamani. Kama vile wakina Taliban walivyokuwa wanafanya. Waficheni tusiwaone kabisa. Wapuuzi wakubwa nyie.

Amandla...
 
Wewe nawe kwani kutongozwa dhambi? Si amkatae tu mwanaume kama hampendi... Mfundishe mkeo/ mwanao/ dada zako kukabiliana na yaliyopo duniani. Wafundishe kujitambua na kusema NO. Kuna wanaume wanabaka bibi zao, watoto zao huko nako wameona nini cha kuwavutia?
Mtu anaejitambua hawezi sapoti huu ujinga. Zindukeni!

Nyie mawazo yenu ngono tu. Hamuwezi ku imagine mtu anaweza kum admire mwanamke alivyopendeza bila kumtaka kingono? Au kuwa mwanamke ana haki na uwezo wa kumkatalia mtu akimtongoza.

Basi wanawake wenu wasiingie kabisa bungeni ili tusiwatamani. Kama vile wakina Taliban walivyokuwa wanafanya. Waficheni tusiwaone kabisa. Wapuuzi wakubwa nyie.

Amandla...

Duh! Mwanamme mzima unasapoti ujinga. Wewe ndio baba wa familia unachangia haya!!! Dunia imebadilika mno
 
Hii nchi ni ya kipuuzi sana, Tatizo la huyu dada ni nini? na bado kuna watu wanasapoti huu upuuzi uliofanywa.
 
Mi najaribu ku-zoom hiyo picha lkn wapi? Sioni kitu..kuna picha nyingine?
 
Back
Top Bottom