Mbunge Condester Michael atimuliwa Bungeni kwa kuvaa ovyo. Spika awaagiza askari wa bunge kuwazuia getini wavaa ovyo

Mbunge Condester Michael atimuliwa Bungeni kwa kuvaa ovyo. Spika awaagiza askari wa bunge kuwazuia getini wavaa ovyo

Maadili ni jambo la muhimu kuzingatiwa, hata kama unahoja nzuri kichwani, bado tunapaswa kujenga heshima na kuzinatia maadili ya jamii.

Tusitetee ukosefu wa maadili, ipo siku watu wataingia uchi na je, tutaendelea kusema ili mradi anatema madini kutoka kichwani kwake?!!!
Sawa mkuu tuna haki ya kutofautiana kwa hili but will NEVER happen Mh.Mbunge kuingia uchi!
 
Bunge katika mwendelezo wa utawala Dume! Mwanamke ana uhuru wa kuvaa chochote anachokipenda kwa siku hiyo na wanaume wasitafsiri hii kuwa she need sex! Kinachotakiwa bungeni ni madini kutoka kwa Mh. Mbunge sio kavaa nini, pls my speaker tembelea bunge la SA uone, wabunge pale wengine wanavaa maovaroli na wengine kama domestic worker na kila kitu kipo safi, haya masheria ya kipuuzi futilia mbali na unyanyasaji ndani yake.
Siyo kila linalo tendeka SA linafaa kwetu kukopi, mazingira na tamaduni zao zaweza kuwa tofauti na zetu. Mbona hujachukua mfano kutoka China, Saudi Arabia na Uturuki?.

Kuvaa kwa heshima wala si suala la mfumo dume/jike. Bunge ni kioo cha jamii lazima wabunge wajiheshimu na kujistahi.
 
Mwomba mwongozo kaona hiyo ndiyo hoja ya uwakilishi wa wananchi wa Momba?

Hili ndilo ametumwa na wapiga kura wake?
Hapo kawatetea wanyonge wa Momba?

Alikosa namna ya kulimaliza/kumrekebisha nje ya kamera ili kutumia muda huu adhimu kwa manufaa mapana ya taifa.

Tunahangaishwa na yasiyo ya muhimu wakati tukipuuza au kunyamazia ya LAZIMA.
Kumradhi naomba ilipoandikwa Momba isomeke Nyang'wale badala ya Momba.

Hivyo isomeke:
Mwomba mwongozo kaona hiyo ndiyo hoja ya uwakilishi wa wananchi wa Nyang'wale?

Hili ndilo ametumwa na wapiga kura wake?
Hapo kawatetea wanyonge wa Nyang'wale?

Alikosa namna ya kulimaliza/kumrekebisha nje ya kamera ili kutumia muda huu adhimu kwa manufaa mapana ya taifa.

Tunahangaishwa na yasiyo ya muhimu wakati tukipuuza au kunyamazia ya LAZIMA.
 
Bunge la Ndugai ni dhaifu sana. Hoja za msingi za kujadili changamoto za Wananchi hazipo ila kuangaliana mavazi. Hata wazee wetu wa miaka 80 sina hakika kama wanaweza kuwa na mawazo ya kuona binti huyu amevaa vazi lisilo la maadili.

Ni vizuri Spika kujiridhisha kabla ya kukurupuka.

Kula rushwa, kuiba kura, uvivu, kutofuata sheria kote ni kukosa maadili, ila kwenye mavazi ndo huwa mnatoa mimacho.

IMG-20210601-WA0000.jpg
 
Iwe fundisho kwa wengine, bunge ni mahali patakatifu. Uhuni ni barabarani sio bungeni.
 
Huyu Mbunge katuaibisha sana wana Momba, yaaani badala ya kuvaa nguo zinazo endana na Bunge letu tukufu yeye anavaa nguo za casino!!
Hata kama hujaolewa lkn unapaswa ujiheshimi.

lkn pia kama alivyo sema Spika kuwa kuna kina MAMA pia huvaa nguo zisizo na heshima wala adabu.
unavaaje suruali imeshika makalio na mapaja halafu unaenda BUNGENI?!! huo ni utovu wa nidhamu na kulikosea heshima jengo la Bunge.

Sehemu zenye Heshima ambazo hatutegemei Mwanamke mwenye kujiheshimu kuvaa mavazi ya ajabu ni;

1. IKULU
2. JESHINI
3.BUNGENI
4.MAHAKAMANI.
maeneo yote hayo niliyo tlyataja hapo juu yanaongozwa na nidhamu za mavazi.
ukitaka kuvaa vimini vyako na tight nenda casino.

Spika katoa maelekezo kuwa kuanzia kesho yeyote atakaye kuja Bungeni huku amevaa nguo zilizo bana makalio asiruhusiwe kuingia getini, lkn pia tunawaomba wawe wanaturushia picha zao ili tuwaweke kwenye orodha mwaka 2025.
 
Mbona Kama suruali yenyewe imeachia haijabana? Kama Ni maadili ya kiTanzania asili yetu Ni kuvaa ngozi au magome ya miti ambayo yalifunika utupu wa mbele na ule wa nyuma, sembuse huyo kavaa suruali ndefu kabisa mpaka kisiginoni, Huo Nini uonevu, vinginevyo labda alimtaka akamkatalia.
 
1. mbona mimi sioni kama suruali aliyovaa mbunge kuwa iko tight hata kidogo?
2. Mbunge alielalamika aliwezaje kuona suruali aliyovaa huyu dada, hasa ukizingatia umbali wa walipokaa baina yao?
 
Bunge la Ndugai ni dhaifu sana. Hoja za msingi za kujadili changamoto za Wananchi hazipo ila kuangaliana mavazi. Hata wazee wetu wa miaka 80 sina hakika kama wanaweza kuwa na mawazo ya kuona binti huyu amevaa vazi lisilo la maadili.

Ni vizuri Spika kujiridhisha kabla ya kukurupuka.

Kula rushwa, kuiba kura, uvivu, kutofuata sheria kote ni kukosa maadili, ila kwenye mavazi ndo huwa mnatoa mimacho.

View attachment 1804951
1622557850360.png

Mbona bibie kavaa kawaida sana.
Myoa hoja ana uhanga nini?
 
Back
Top Bottom