Just imagine wewe ni mtu kutoka familia masikini kutoka kanda ile ya chapa Ng'ombe, kule ambako mnapenda sana wanawake waupe!, wewe umekwenda chuo, mkiwa darasa moja, kukatokea mdada wa Kichagga kutoka familia bora, wa rangi ya maji ya kunde, kakupenda kafa kaoza, utamkataa kwa sababu tuu sio cheupe?. Mapenzi moto moto ya chuo, na baada tuu ya kumaliza chuo mkaputiliza moja kwa moja altareni mbele ya meza ya BWANA, mkala kiapo cha ndoa takatifu hivyo mkaoana, Msukuma masikini chapa ngombe umeoa mtoto wa tajiri Mchagga wa Machame!.
Kwenye ndoa yenu mmejaliwa kupata watoto 2 a boy and a girl na mmeamua kuendesha maisha ya kizungu kuwa hao watoto wawili ndio mwisho!.
Kufuatia familia ya mke wana uwezo,, mnahamia UK kisha US, wewe ukiwa unamtegemea mke kila kitu!. Wakati mkiwa US familia ya mke, wanaamua kumlipia binti yao, yaani wife wao, scholarship ya 4 years US!. Wewe ndio unageuka house boy na baby sitter wa watoto wenu wakati mama anasoma!. Yaani mke ndio kila kitu, wewe mume kula kulala!.
Mind well, kabla ya kuhamia US, huku bongo, baada ya shule wewe na wife wako ambao wote mlikuwa chuo kimoja na darasa moja, kilichomfanya mtoto wa tajiri kula kuoza ni uwezo wako wa darasani!. Kwanza wewe umesoma St. Katuyumba!, binti kasama Academy!. Kufika chuo, mnakaa next to each other, kwenye mitihani sio mambo ya kuibilizia au kupiga chabo!, no!. Ni mwanamume wa Kisukuma unajipinda kwanza unaipiga paper wako, kisha unaipiga paper yake nzima nzima, yaani unapiga double na zote mnafumua A!. Kanini mtoto wa Kichagga asife asioze?.
Ile kumaliza tuu chuo, wewe unatafuta kazi, mwenzako tayari keshatafutiwa kazi kwenye ile media ya Na wa Kichagga, mume ni family friend toka Machame!. Binti ni bosi wewe unatafuta kazi RTD!.
Huvyo ndani ya ndoa yenu mke analipwa mshahara mkubwa kuliko mume!. Usikwambie mtu, ukitoka familia masikini ukaoa familia tajiri halafu mke akakuzidi kipato!. Japo mume ndio kichwa cha nyumba, lakini the determinant ni mke na familia ya mke!.
Wakati tunaondoka nchini kuhamia UK na US, sponsored by wife's family, mimi tayari ni mtangazaji maarufu wa kipindi cha Kiti Moto!. Hivyo kilazimika to sacrifice kazi yangu kumsuport wife kule US!.
Yale maisha ya mwanamume kuwa dependant wa familia ya mkeo kwasababu umetoka familia masikini ukaoa familia tajiri, makabila mengine wanawaweza hata wenzetu wazungu wanaweza, sisi Wasukuma hiyo hatuwezi!.
Hivyo yale maisha ya US, wife anasoma analipiwa na familia yake, mimi sina kazi na watoto wote tukitegemea familia ya mke, halafu wife ndio bread winner mimi kula kulala!. Nilishindwa!.
Kwa vile bongo nina kazi yangu, nikawasomba wanangu tukarudi zetu Bongo. Wakwe wakaniletea a house girl kutoka Machame, binti mlokole. Ikawa hata nikichelewa home siku nikipitiliza, taarifa zinafika hadi US!.
Ndio nikagundua the source, a house girl wa kutafutiwa na Mama mke, nilimrudisha kwao mimi kutafuta a house girl wa kazi mbili. kazi ya kwanza ni kunisaidia kuwalea wanangu wakati mama yao yuko masomoni. Shule yenyewe ni ya maka 4. House Girl niliye mtafuta ni jina tuu la "a house girl" lakini kiukweli hakuwa ni house girl tuu!. Nilitafuta binti mweupe wa Tanga!, amesoma, she is a hotelier, kazi yake ya pili ni kumsaidia mama!.
Nyumba mwanaume wa Kisukuma yenye mke Mchagga mweusi mwenye English fugure, yuko masomoni US kwa miaka 4, huku nyuma baba keleta a house girl cheupe, Tanga line, guu guu!, shepu shape, figure figure, sura sura!. Hata ungekuwa wewe, miaka 4 ungesubiri tuu?
Katika kipindi hicho, ndugu wa mke hawakauki nyumbani!, excuse ni kuja kusalimia watoto!, yaani ndugu kutoka ukweni kijijini kuja kusalimia mjini, ndugu yao yuko US, halafu ndio wafikie kwangu!. Si wakamuona 'house girl' wakapeleka ripoti!.
Kwanza siku zinapigwa kutoka Marekani, kwa mama kwenda kwa baba "mwachishe kazi" huyo dada!". Baba anauliza nimwachishe kazi kwa kosa gani?. Najibiwa "wee nimwachishe tuu, mimi simtaki". Baba kagoma, kamwambia mama siwezi kumwachisha mtu kazi bila kosa lolote". Wife anakuja juu kuwa nani muhimu zaidi kati ya mke na mdada wa kazi, kama mke ni muhimu zaidi, then mdada wa kazi aondoke!. Asipoondoka, mke harudi nyumbani!". Baba akaamua kwa sasa ambapo wife yuko shule, mdada wa kazi ndie mtu muhimu kwasababu ndie anahudumia familia!. Hivyo nikamgomea wife kumfukuza dada kazi!.
Baada ya wife kumaliza shule, mimi huyoo US, kumfuata. Kufika kule wife kagoma kurudi bongo!. Et kaelezwa dada wa kazi wa Tanga, kamloga baba!. Akirudi hiyo dada anaweza kamloga, hivyo wife kaamua nikitaka ndoa iendelee, mimi ndio nihamie US!.
Wabongo wa DMV nao sio wachoyo wa habari!. Na mimi nikashikwa sikio!. Kila mmoja akaamua kushika lake. Mimi siko tayari kurudi kuishi US, as dependent wa wife. Tukakubaliana kila mtu aishi kivyake. Nikajikusanya nikajirudia zangu Bongo.
Kuna migomo mingine wake zetu mnatugomea mkijijua mmetukomoa!. Yaani mwanamume wa Kichagga unamsusia nyumba mwanamke wa Kitanga huku ukijihesabu umemkomoa!. Adhabu nyingine ni kuvuja tuu kwa pakacha!.
Huku Bongo nako, nikakutana na yale majanga ya ajali ya piki piki, huku dada akawa ndio kila kitu!. Baada ya ajali, taarifa za kuwa nini confirmed to a wheelchair, wife akataka kurudi out of compassion. Nikamgomea kwa hoja moja tuu, niko well taken care of. Kilicho fuata ni we call it a quit, na kuformalize hii Tangaline!. Sasa ni mama wa watoto 4!, mabinti watatu na kidume kimoja!.
Changamoto za Kupata Mtoto Mchanga, Ukiwa Umri wa Kustaafu!. Unakuwa ni Baba Babu!. Dawa ni Kujipanga Kabla, Vinginevyo ni Kubebesha Watu Mizigo Yako!