Mbunge Deo Sanga wa Makambako afunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu

Mbunge Deo Sanga wa Makambako afunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu

Kuna tofauti kati ya siri, secrets, na faragha, the right to privacy!. Hata nikikaa bar openly kujinywea Joni Mtembezi wangu, huruhusiwi kunipiga picha au kunisema popote in public kuwa nimemuona Pasco yuko counter ya Rombo Green View, anapiga vitu!.
Japo sio siri lakini kunipiga picha au kunizungumzia ni kuniingilia my right to privacy.

Ndoa, ni tukio personal la public na inatangazwa openly na inafungwa openly watu wamealikwa openly na kupiga picha na simu janja zao na kushare kwenye social media lakini kuzileta picha hizo kwenye public forum or mainstream media bila ruhusa ya wahusika ni kuingilia their right to privacy!.
P
You're totally wrong on this one na probably una interest binafsi, hivi harusi ya Mrema uliyasema haya? Je na msiba wa public figure mathalan mbunge kuupost hapa janvini itakuwa ni kuingilia privacy ya marehemu?
Utajitetea kwa namna milioni lakini kwenye hili umeboronga sana.
 
Naomba tujifunze kuheshimu the right to privacy ya haki za faragha za watu!.

Mtu kuoa au kuolewa ni issue private ya maisha binafsi ya mtu, kama mtu anapoamua kukaa bar au kustarehe popote, hiyo ni haki binafsi ya faragha, haki hiyo inabidi iheshimiwe, unless kama ni yeye mwenyewe amealika media akawaruhusu mtangazie dunia kuwa ameoa!.
P

... nakubaliana na wewe....
 
Naomba tujifunze kuheshimu the right to privacy ya haki za faragha za watu!.

Mtu kuoa au kuolewa ni issue private ya maisha binafsi ya mtu, kama mtu anapoamua kukaa bar au kustarehe popote, hiyo ni haki binafsi ya faragha, haki hiyo inabidi iheshimiwe, unless kama ni yeye mwenyewe amealika media akawaruhusu mtangazie dunia kuwa ameoa!.
P

Mshamba wewe, ndiyo maana mke wako alikuacha solemba ukaishia kuoa house girl wako!
 
Deo Sanga maarufu kama Jah People ambaye ni mbunge wa Jimbo la Makambako, leo 14/9/2022 amefunga ndoa Takatifu katika Kanisa Katoliki mjini humo .
Mbona wanafanana sana? Yaani hapo kinachowatofautisha ni urefu tu, maan hiyo rangi nyingine itabadilika hivi karibuni
1663294341793.png
 
Naomba tujifunze kuheshimu the right to privacy ya haki za faragha za watu!.

Mtu kuoa au kuolewa ni issue private ya maisha binafsi ya mtu, kama mtu anapoamua kukaa bar au kustarehe popote, hiyo ni haki binafsi ya faragha, haki hiyo inabidi iheshimiwe, unless kama ni yeye mwenyewe amealika media akawaruhusu mtangazie dunia kuwa ameoa!.
P
Hakika mkuu
 
Mshamba wewe, ndiyo maana mke wako alikuacha solemba ukaishia kuoa house girl wako!
Mkuu Maulaga59, hapa nazuia nini na we we unafanya nini kuhusu the right to privacy?. Ila pia kasema ukweli, umbea mwingine...., mimi niko very open kuhusu maisha yangu both public life as well as private life, Enyi Waume Wapendeni Wake Zenu!-Wife Kanirudia Saa12:00 Asubuhi!-Bado Nampenda! humu nilisema kila kitu!.
Background Story!
Mimi nimeoa nikiwa kijana sana, na nilimuoa my school mate na classmate school sweetheart, na baada tuu ya ndoa tukahamia UK kutafuta maisha, utumwa wa box ukanishinda, nikalazimisha kurudi bongo, baadae tukaenda US, by that time tuna watoto 2, kule mwenzagu ndio alipata scholarship ya miaka 4, mimi ndie niwe house boy, house husband na baby sitter wa watoto wetu wawili!. Kwa vile mimi bongo nilikuwa na kazi yangu, tukakubaliana mimi nirudi na watoto, niendelee na kazi, yeye asome, akimaliza atarejea bongo!. Japo nilimtembelea kila miaka 2, nilimpomtembelea mara ya pili ambapo ndio anamaliza shule, yalinikuta yaliyokukuta!, mwenzagu aligoma kurudi bongo!, nilirudi mwenyewe bongo na kusubiri for 7 good years kuwa atarudi, atarudi, hakurudi!.

Katika kusubiri huko, ubinadamu nao lazima uendelee, (sisi sio malaika), hivyo nililazimika kuwa na "rafiki" tena nakumbuka kuna wakati wakuu wangu wa Jumuiya Ndogo Ndogo, walinilalalimikia, "wewe una ndoa ya Kikatoliki", kwa nini "rafiki" umlete home?!. Nilijibu ni kweli ndoa ipo ila ni kwenye makaratasi tuu, "huyu ni rafiki zaidi ya rafiki"!, kwanza ile kukubali tuu, kuwalea wale watoto wangu wawili wa mwanzo, na kukatokea wawili wengine hapa katikati!, nikajiaminisha wanawake wenye upendo wa hivyo, ni wale tuu walioshushwa kutoka mbinguni!.

Katika kuendeleza "ubinaadamu", shetani naye akaleta majaribu mengine!, ...
Kina vitu vingine vinatutokea kwenye maisha yetu unakuta sio sisi ni shetani!. Kwa taarifa yako hiyo dada wala hakuwa a house girl!, ni mdada tuu mwenye kazi yake mzee mzima nikafika bei, nikamuachisha kazi na nikavuta jumla!.

Mastori ya Pasco.

Just imagine wewe ni mtu kutoka familia masikini kutoka kanda ile ya chapa Ng'ombe, kule ambako mnapenda sana wanawake waupe!, wewe umekwenda chuo, mkiwa darasa moja, kukatokea mdada wa Kichagga kutoka familia bora, wa rangi ya maji ya kunde, kakupenda kafa kaoza, utamkataa kwa sababu tuu sio cheupe?. Mapenzi moto moto ya chuo, na baada tuu ya kumaliza chuo mkaputiliza moja kwa moja altareni mbele ya meza ya BWANA, mkala kiapo cha ndoa takatifu hivyo mkaoana, Msukuma masikini chapa ngombe umeoa mtoto wa tajiri Mchagga wa Machame!.

Kwenye ndoa yenu mmejaliwa kupata watoto 2 a boy and a girl na mmeamua kuendesha maisha ya kizungu kuwa hao watoto wawili ndio mwisho!.

Kufuatia familia ya mke wana uwezo,, mnahamia UK kisha US, wewe ukiwa unamtegemea mke kila kitu!. Wakati mkiwa US familia ya mke, wanaamua kumlipia binti yao, yaani wife wao, scholarship ya 4 years US!. Wewe ndio unageuka house boy na baby sitter wa watoto wenu wakati mama anasoma!. Yaani mke ndio kila kitu, wewe mume kula kulala!.

Mind well, kabla ya kuhamia US, huku bongo, baada ya shule wewe na wife wako ambao wote mlikuwa chuo kimoja na darasa moja, kilichomfanya mtoto wa tajiri kula kuoza ni uwezo wako wa darasani!. Kwanza wewe umesoma St. Katuyumba!, binti kasama Academy!. Kufika chuo, mnakaa next to each other, kwenye mitihani sio mambo ya kuibilizia au kupiga chabo!, no!. Ni mwanamume wa Kisukuma unajipinda kwanza unaipiga paper wako, kisha unaipiga paper yake nzima nzima, yaani unapiga double na zote mnafumua A!. Kanini mtoto wa Kichagga asife asioze?.

Ile kumaliza tuu chuo, wewe unatafuta kazi, mwenzako tayari keshatafutiwa kazi kwenye ile media ya Na wa Kichagga, mume ni family friend toka Machame!. Binti ni bosi wewe unatafuta kazi RTD!.

Huvyo ndani ya ndoa yenu mke analipwa mshahara mkubwa kuliko mume!. Usikwambie mtu, ukitoka familia masikini ukaoa familia tajiri halafu mke akakuzidi kipato!. Japo mume ndio kichwa cha nyumba, lakini the determinant ni mke na familia ya mke!.

Wakati tunaondoka nchini kuhamia UK na US, sponsored by wife's family, mimi tayari ni mtangazaji maarufu wa kipindi cha Kiti Moto!. Hivyo kilazimika to sacrifice kazi yangu kumsuport wife kule US!.

Yale maisha ya mwanamume kuwa dependant wa familia ya mkeo kwasababu umetoka familia masikini ukaoa familia tajiri, makabila mengine wanawaweza hata wenzetu wazungu wanaweza, sisi Wasukuma hiyo hatuwezi!.

Hivyo yale maisha ya US, wife anasoma analipiwa na familia yake, mimi sina kazi na watoto wote tukitegemea familia ya mke, halafu wife ndio bread winner mimi kula kulala!. Nilishindwa!.

Kwa vile bongo nina kazi yangu, nikawasomba wanangu tukarudi zetu Bongo. Wakwe wakaniletea a house girl kutoka Machame, binti mlokole. Ikawa hata nikichelewa home siku nikipitiliza, taarifa zinafika hadi US!.

Ndio nikagundua the source, a house girl wa kutafutiwa na Mama mke, nilimrudisha kwao mimi kutafuta a house girl wa kazi mbili. kazi ya kwanza ni kunisaidia kuwalea wanangu wakati mama yao yuko masomoni. Shule yenyewe ni ya maka 4. House Girl niliye mtafuta ni jina tuu la "a house girl" lakini kiukweli hakuwa ni house girl tuu!. Nilitafuta binti mweupe wa Tanga!, amesoma, she is a hotelier, kazi yake ya pili ni kumsaidia mama!.

Nyumba mwanaume wa Kisukuma yenye mke Mchagga mweusi mwenye English fugure, yuko masomoni US kwa miaka 4, huku nyuma baba keleta a house girl cheupe, Tanga line, guu guu!, shepu shape, figure figure, sura sura!. Hata ungekuwa wewe, miaka 4 ungesubiri tuu?

Katika kipindi hicho, ndugu wa mke hawakauki nyumbani!, excuse ni kuja kusalimia watoto!, yaani ndugu kutoka ukweni kijijini kuja kusalimia mjini, ndugu yao yuko US, halafu ndio wafikie kwangu!. Si wakamuona 'house girl' wakapeleka ripoti!.

Kwanza siku zinapigwa kutoka Marekani, kwa mama kwenda kwa baba "mwachishe kazi" huyo dada!". Baba anauliza nimwachishe kazi kwa kosa gani?. Najibiwa "wee nimwachishe tuu, mimi simtaki". Baba kagoma, kamwambia mama siwezi kumwachisha mtu kazi bila kosa lolote". Wife anakuja juu kuwa nani muhimu zaidi kati ya mke na mdada wa kazi, kama mke ni muhimu zaidi, then mdada wa kazi aondoke!. Asipoondoka, mke harudi nyumbani!". Baba akaamua kwa sasa ambapo wife yuko shule, mdada wa kazi ndie mtu muhimu kwasababu ndie anahudumia familia!. Hivyo nikamgomea wife kumfukuza dada kazi!.

Baada ya wife kumaliza shule, mimi huyoo US, kumfuata. Kufika kule wife kagoma kurudi bongo!. Et kaelezwa dada wa kazi wa Tanga, kamloga baba!. Akirudi hiyo dada anaweza kamloga, hivyo wife kaamua nikitaka ndoa iendelee, mimi ndio nihamie US!.

Wabongo wa DMV nao sio wachoyo wa habari!. Na mimi nikashikwa sikio!. Kila mmoja akaamua kushika lake. Mimi siko tayari kurudi kuishi US, as dependent wa wife. Tukakubaliana kila mtu aishi kivyake. Nikajikusanya nikajirudia zangu Bongo.

Kuna migomo mingine wake zetu mnatugomea mkijijua mmetukomoa!. Yaani mwanamume wa Kichagga unamsusia nyumba mwanamke wa Kitanga huku ukijihesabu umemkomoa!. Adhabu nyingine ni kuvuja tuu kwa pakacha!.

Huku Bongo nako, nikakutana na yale majanga ya ajali ya piki piki, huku dada akawa ndio kila kitu!. Baada ya ajali, taarifa za kuwa nini confirmed to a wheelchair, wife akataka kurudi out of compassion. Nikamgomea kwa hoja moja tuu, niko well taken care of. Kilicho fuata ni we call it a quit, na kuformalize hii Tangaline!. Sasa ni mama wa watoto 4!, mabinti watatu na kidume kimoja!. Changamoto za Kupata Mtoto Mchanga, Ukiwa Umri wa Kustaafu!. Unakuwa ni Baba Babu!. Dawa ni Kujipanga Kabla, Vinginevyo ni Kubebesha Watu Mizigo Yako!

Hivyo mtu anayeitwa house girl ni titles tuu, baadhi ya ma house girls ni zaidi ya ma housewife kwenye yale mengineyo!. Unadhani kule kuna alama mama grades kuwa hiyo ni ya housewife ,hiyo ni ya house girl na hii ni wale madanga!, the services are all the same and sometimes more or less!. Tusiwadharau kabisa beki 3!, wanaokoa sana majahazi kwa kuwasaidia sana wale wamama wenye nyumba ambao ni wavivu wavivu!.

P
 
Kwamba kuoa kwake ni siri au unataka kusema JF haturuhusiwi kuwaandika waliooa, tena waliooa hadharani? Huu ndio uanasheria uliosomea law school?

Pascal nani kakudanganya kwamba unao uwezo wa kutupangia cha kuandika?
Kuoana haiwagi siri na ndo maana zinafungwa hadharani na mnaulizwa mbele ya kadamnasi.
 
Ila Hawa Wazee Wamecharuka Sana Sasa Hivi

Professor Kapuya
Mrema * Hatunaye
Deo Sanga
 
Back
Top Bottom