Ukisoma vizuri hiyo aya ya mwisho, na ukifuatilia matumizi ya waheshimiwa .. Dah!Nakubaliana na huyu jamaa, tukumbuke alikuwa Mkurugenzi wa Maji kwenye Wizara ya Maji, dili nje nje....
Ubunge mkavu bila uwaziri, unaibu, uspika, unaibu spika au nafasi nyingine za uongozi ni janga kubwa.
Kwanza familia, ndugu, jamaa na marafiki wakisikia umekuwa mbunge wanajua umetoboa!
Kila mtu atakuganda anataka msaada na fedha
Na wewe mwenyewe katika kutaka "kulinda hadhi" ya mbunge, hutataka kufanya mambo ya bei chee.
Mshahara wa mil 15 ni mkubwa kama una matumizi ya kawaida
Yaani majuzi tu mtu alikuwa mchunga ng'ombe, leo anataka kuishi angani kama kunguru