Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE JAFARI WAMBURA CHEGE: MIMI NI MUOMBAJI, ANAYELETA FEDHA ZA MAENDELEO NI RAIS WA NCHI, DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
Mbunge wa Jimbo la Rorya, Mhe. Jafari Wambura Chege katika muendelezo wa ziara Jimboni amesema kuwa Yeye kazi yake ni kuomba fedha za Maendeleo lakini anayetoa hizo fedha ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Jafari Wambura Chege amesema kuwa, Wabunge wanapoongea bungeni, Mama Samia anasikia na anatekeleza ndiyo maana ndani ya miaka mitatu Rorya imepata miradi mingi sana kwa kipindi kifupi.
"Tumejenga madaraja ya Mto Mole na Mto Maya yamekamilika. Mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan amenipa fedha zaidi ya shilingi milioni 200 ili tupandishe barabara iwe juu iwe sawa ili tuwe tumekamilisha madaraja pamoja na barabara yake" - Mhe. Jafari Wambura Chege, Mbunge wa Jimbo la Rorya
"Aliyenipa fedha za kujengwa madaraja na upanuzi wa barabara ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tumejenga daraja ambalo wananchi wameliomba kwa zaidi ya miaka 40, akina mama na watoto wadogo wamekufa sana"
"Malengo yetu sisi ni mtu Anayetokea Kuluya - Nyamambwuku - Kilogo - Uboche - Kariakoo - Nyabikondo - Uboche B - Shirati kwa kutumia barabara tunaiyojenga. Haya yote anayeyafanya ni Mama yetu Samia"
"Mmeomba Maji kwa muda mrefu, kuna vijiji havina maji lakini Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kuwachimbia kisima ambacho kitatengenezewa miundombinu mizuri ya maji. Nimetoa Milioni 3 mjenge choo ambayo nimepewa na Mama Samia kupitia Mfuko wa Jimbo"
"Uchaguzi unaokuja mwakani Wema ulipwe kwa Wema. Pamoja na haya mazuri yaliyofanyika isije ikafika mwakani tukamuacha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mwakani nitakuja kumuombea Rais Samia kura za kishindo" - Mhe. Jafari Wambura Chege, Mbunge wa Jimbo la Rorya