Mbunge Jerry Silaa aangua kilio bungeni baada ya kumaliza kuchangia mjadala

Mbunge Jerry Silaa aangua kilio bungeni baada ya kumaliza kuchangia mjadala

Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa akilia baada ya kumaliza kuchangia mjadala wa kupitisha makadikio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Jijini Dodoma leo.

Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay yeye aliamua kuruka Sarakasi, Jerry Silaa aangua kilio..Kulikoni kwa hawa wabunge?View attachment 2235484
Walie tuu,wakati wanaimba mapambio miaka ya Jiwe walijua barabara zinajengewa makamasi yao?

Ujenzi wa barabara ulivurugwa na Mwendazake kwa kutoa kipaombele kwenye Reli kwa.kuhamisha.pesa kutoka kwenye barabara..

On top of that Wakandarasi walikuwa wanadai madeni makubwa ya serikali Kwa miradi ya nyuma ambayo ilikuwa imekamilika ila Serikali ilichelewa kulipa kwa kukosa pesa na riba zakawa kubwa zaidi..

Matokeo yake bajeti iliyomalizika iliishia kulipa hayo madeni ya Serikali,aliwahi ongea hata Halima hili jambo..

Hii ndio shida sasa ya kuwa na Rais ambae anajiamulia anavyojiskia yaani hatima ya Nchi iko kwa mtu mmja atakavyojiskia.
 
Hizi Click Baits hizi !!! Ameangua Kilio kweli ? Sababu kuangua kulio ni tofauti na aina nyingine za kulia; hata kama ni kweli kalia
 
Jerry mara nyingi huwa yuko upande wa wananchi mkuu

Na ndiyo maana hata kipindi malalamiko ya wananchi kudai wabunge wapunguziwe mishahara na posho wabunge wote walikataa isipokuwa yeye ambaye aliunga mkono matokeo yake akaishia kupigwa ban kuhudhuria baadhi ya vikao vya bunge

Sasa sijui ulitaka amjengee kila mwananchi nyumba ili uamini kuwa angalau kuna muda huwa yuko upande wa wananchi

Wabongo bhana msipopiganiwa haki zenu mnasema viongozi mafisadi mkipiganiwa haki zenu bado mnasema viongozi wanafiki na ndiyo maana viongozi wengi wameona wajiangalie wao na familia zao tu maana wabongo hamna jema

Lazima mjue siyo viongozi wote wapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi wapo ambao wana uchungu na wananchi
WANANCHI WA JIMBO GANI ? HAJAWAHI KUWA NAO AKIWA DIWANI WALA MBUNGE
 
Ni upunguani wa akili kuamini kuwa Tanzania sasa hivi ina Bunge
 
Jerry mara nyingi huwa yuko upande wa wananchi mkuu.

Na ndiyo maana hata kipindi malalamiko ya wananchi kudai wabunge wapunguziwe mishahara na posho wabunge wote walikataa isipokuwa yeye ambaye aliunga mkono matokeo yake akaishia kupigwa ban kuhudhuria baadhi ya vikao vya bunge.

Sasa sijui ulitaka amjengee kila mwananchi nyumba ili uamini kuwa angalau kuna muda huwa yuko upande wa wananchi.

Wabongo bhana msipopiganiwa haki zenu mnasema viongozi mafisadi mkipiganiwa haki zenu bado mnasema viongozi wanafiki na ndiyo maana viongozi wengi wameona wajiangalie wao na familia zao tu maana wabongo hamna jema.

Lazima mjue siyo viongozi wote wapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi wapo ambao wana uchungu na wananchi.
Mkuu usimtetee huyu jamaa labda kama huishi Ukonga. Hana msaada wowote kwa wananchi na hali ya barabara na huduma za jamii kwenye jimbo la Ukonga inatisha.
 
Mbunge wa Ukonga kupitia CCM, Jerry Silaa akilia baada ya kumaliza kuchangia mjadala wa kupitisha makadikio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Jijini Dodoma leo.

Silaa amemwaga machozi akieleza kuwa Kampuni ya Syno Hydro iliyopewa zabuni ya kujenga barabara ya mwendokasi kuanzia Kariakoo hadi Gongo la Mboto Jijini Dar es salaam imevurunda katika miradi mingine.

Mbunge wa Mbulu Vijijini kupitia CCM, Flatei Massay, yeye aliamua kuruka Sarakasi ikiwa ni njia ya kuonyesha hisia zake kwa kero ya kutokuwa na barabara ya lami jimboni kwake. Jerry Silaa aangua kilio. Flatei Sarakasi. Kulikoni kwa hawa wabunge?

View attachment 2235484
Bungeni kuna comedy hadi inakuwa kama kijiwe Cha kahawa, mwingine amebinuka sarakasi.........Chama Cha Mapinduzi kijitafakari selection ya mtu mwenye sifa za kuwa mbunge
 
binafsi huwa nikiwa na furaha kuna tendo fulani lazima nilifanye muda huo au baada ya hapo..
 
Mbunge wa Ukonga kupitia CCM, Jerry Silaa akilia baada ya kumaliza kuchangia mjadala wa kupitisha makadikio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Jijini Dodoma leo.

Silaa amemwaga machozi akieleza kuwa Kampuni ya Syno Hydro iliyopewa zabuni ya kujenga barabara ya mwendokasi kuanzia Kariakoo hadi Gongo la Mboto Jijini Dar es salaam imevurunda katika miradi mingine.

Mbunge wa Mbulu Vijijini kupitia CCM, Flatei Massay, yeye aliamua kuruka Sarakasi ikiwa ni njia ya kuonyesha hisia zake kwa kero ya kutokuwa na barabara ya lami jimboni kwake. Jerry Silaa aangua kilio. Flatei Sarakasi. Kulikoni kwa hawa wabunge?

View attachment 2235484
Haya huwa ni machozi ya mamba,mchongo hayana Cha umaana chochote,kwa mkwnja Hawa jamaa wanaopokea kwa siku,300K per day,lazima utafanya chochote Ili mradi tu,mbele ya mkwanja mrefu,hata nguo unaweza vua,
 
Kuna vita inaendelea kati ya Bongo Movie Vs Bunge Tulia,

Acha tuone nani ataibuka mshindi, tatizo wengine wanaigiza wakiwa wameshiba na wengine wanaigiza wakiwa na njaa.
Kulisaka tonge la ugali kunahitaji akili sana..!
 
Jerry ni kijana kidogo anaonyesha msimamo sema tu chama alichomo kimejaa wanafiki - akizidi sana hawakawii kumchomoa 2025 kwenye kura za maoni.
 
Jamaa ameruka sarakasi sijajuwa kilichomfurahisha hapa bungeni
Ameruka Sarakasi ili Serikali ipeleke maendeleo, kujengwe barabara ya lami kwenye Jimbo lake..!
 
Back
Top Bottom