Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
SINOHYDRO Corporation LTD wamepewa zabuni kujenga mradi wa mwendokadi BRT-3 Gongo la Mboto-Kariakoo (23.6km) kwa $148.1M na wamepewa zabuni hiyo bila ushindani (single source), wakati ujenzi wa BRT 2 (Gerezani -Mbagala) 20.3km wamejenga chini ya kiwango. Hawa wachina wameturoga?Mbunge wa Ukonga kupitia CCM, Jerry Silaa akilia baada ya kumaliza kuchangia mjadala wa kupitisha makadikio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Jijini Dodoma leo.
Silaa amemwaga machozi akieleza kuwa Kampuni ya Syno Hydro iliyopewa zabuni ya kujenga barabara ya mwendokasi kuanzia Kariakoo hadi Gongo la Mboto Jijini Dar es salaam imevurunda katika miradi mingine.
Mbunge wa Mbulu Vijijini kupitia CCM, Flatei Massay, yeye aliamua kuruka Sarakasi ikiwa ni njia ya kuonyesha hisia zake kwa kero ya kutokuwa na barabara ya lami jimboni kwake. Jerry Silaa aangua kilio. Flatei Sarakasi. Kulikoni kwa hawa wabunge?
View attachment 2235484
Mwigulu ndie mhusika wa 'single source'Silaa amemwaga machozi akieleza kuwa Kampuni ya Syno Hydro iliyopewa zabuni ya kujenga barabara ya mwendokasi kuanzia Kariakoo hadi Gongo la Mboto Jijini Dar es salaam imevurunda katika miradi mingine.
Kitu cha singida hicho kinafanya huu uharamia wote pale hazina! 'Siku zaja kila jiwe litageuzwa'!Ni kama ambavyo wizara ya fedha ilivyoingia makubaliano na mkandarasi China Civil Engineering construction corporation (CCECC) kwa utaratibu wa single source (zabuni bila ushindani) zabuni yenye thamani ya Shs. 6.7 trilioni kujenga lot Na. 6 ya SGR (Tabora - Kigoma).
Wana uchungu gani?kama ana uchungu na nchi angekubali kuwa sehemu ya bunge haramu la uchafuzi,sasa akibinuka ndio hela itapelekwa?Mjinga ni wewe. Watu wana uchungu na nchi we' unaongea upuuzi.