Mbunge wa Ukonga kupitia CCM, Jerry Silaa akilia baada ya kumaliza kuchangia mjadala wa kupitisha makadikio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Jijini Dodoma leo.
Silaa amemwaga machozi akieleza kuwa Kampuni ya Syno Hydro iliyopewa zabuni ya kujenga barabara ya mwendokasi kuanzia Kariakoo hadi Gongo la Mboto Jijini Dar es salaam imevurunda katika miradi mingine.
Mbunge wa Mbulu Vijijini kupitia CCM, Flatei Massay, yeye aliamua kuruka Sarakasi ikiwa ni njia ya kuonyesha hisia zake kwa kero ya kutokuwa na barabara ya lami jimboni kwake. Jerry Silaa aangua kilio. Flatei Sarakasi. Kulikoni kwa hawa wabunge?
View attachment 2235484
SINOHYDRO Corporation LTD wamepewa zabuni kujenga mradi wa mwendokadi BRT-3 Gongo la Mboto-Kariakoo (23.6km) kwa $148.1M na wamepewa zabuni hiyo bila ushindani (single source), wakati ujenzi wa BRT 2 (Gerezani -Mbagala) 20.3km wamejenga chini ya kiwango. Hawa wachina wameturoga?
Zingatia, huo ni mkopo kutoka benki ya Dunia (WB). Na serikali ya Tanzania imekopeshwa $246.7 million kwa ajili ya ujenzi wa BRT-3 ($148.1 million) na BRT-4 ($99.9 million). Wanazo. Wakati huo DART wametumia $2.46 million to 77 kulipa wakazi kupisha ujenzi wa 23.6km kwa BRT-3
BRT-1 ni 21km ilijengwa na STRABAG international GmbH, Kimara kwenda Kivukoni, Morocco, Gerezani kupitia Ubungo, ulikuwa mkopo wa AfDB na WB na $154M. Lakini sasa BRT-2 na BRT-3 wamepewa SINOHYDRO ambao BRT-2 wamejenga chini ya kiwango na baadhi ya sehemu barabara imeharibika.
Ni kama ambavyo wizara ya fedha ilivyoingia makubaliano na mkandarasi China Civil Engineering construction corporation (CCECC) kwa utaratibu wa single source (zabuni bila ushindani) zabuni yenye thamani ya Shs. 6.7 trilioni kujenga lot Na. 6 ya SGR (Tabora - Kigoma).
Ujenzi huo wa lot Na. 6 kutoka Tabora - Kigoma (411km) jumla ya gharama za ujenzi wake ni US$4.8M (Sh.11.1bn) kwa kila 1 kilometer. Hivyo kwa 411 kilometer mkandarasi atatumia Shs. 4.6 trilioni. zabuni hii hawa CCECC wamepewa pia bila zabuni shindani (single source).
Watu timamu wanahoji, mkandarasi China Civil Engineering construction corporation (CCECC), Mwigulu ametoka naye wapi hadi kupewa kandarasi ya trilioni 4.6 wakati kwa miezi 16 amejenga lot Na. 5 kwa 4.4% pekee? DSM - Mwanza ujenzi wake jumla ni Shs. 14.7 trillion (US$6.4 billion)
China Civil Engineering construction corporation (CCECC) Tabora - Kigoma (411km) amechukua Shs. 6.7 trilioni. Zaidi ya nusu ya fedha zote ambazo zimetengwa kwa ujenzi wa Dar Es Salaam - Mwanza ujenzi wake jumla ni Shs. 14.7 trillion (US$6.4 billion). Ni UJAMBAZI hakuna shaka.
Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation alipewa ujenzi wa lot Na. 5, Isaka – Mwanza (249 km). Miezi 16 amejenga 4.4% pekee na HAKUNA hata kipande kimoja cha reli ameweka katika miezi 16. Mwigulu anasema bungeni kwamba haukuwepo ufadhili wa kifedha. Ni utapeli.
Narejea katika hoja yangu ya msingi ya utaratibu wa kutoa zabuni zisizokuwa na ushindani kupitia (single source). Katika hili, TANROADS ndiye procurement entity na ndiyo wanaanda nyaraka za zabuni na kuweka sifa aa muombaji. Kwamba hawajui SINOHYDRO wamekosa sifa? RUSHWA?
Wizara ya fedha ambayo ipo chini ya Mwigulu Nchemba LAZIMA ihusike kuidhinisha matumizi ya fedha za umma. Hili la China Civil Engineering construction corporation lina mfanano sawa na hili la la SINOHYDRO Corporation LTD na wote wamepewa fedha tayari. Kuna harufu mbaya.