Mbunge Jerry Silaa hajui kitu kuhusu ATCL, asijifanye mjuaji

Hivi huko nyuma kabla ya 2016 mlikua na ndege ngapi na watumishi wangapi? Ukijibu hilo utajua slaa alichokua anatetea,kuwa msomi ni pamoja na kuwa na mawazo tofauti na yako.utalipaje Deni bila kua na biashara? Biashara inatakiwa ilipe Deni,ndo maana mabenki yanaweza kuikopesha biashara yako iloyumba ili upate uwezo wa kulipa Deni.
 
Naona wewe ndio mpotoshaji mkuu na nina wasiwasi na kujifanya unajua hadi kukosoa wakati inaonekana unaleta siasa kwenye mambo ya uchumi, tatizo sio kufidia sijui uchumi uko juu ,uchumi kuwa juu hauji kama njugu na ni iradi ya kimkakati ndio inainua uchumi na sio madawa au maji safi mkuu, rudi haraka darasani,tatizo Watanzania tunadhani maendeleo au kuwa taifa lenye uchumi mkubwa nikitu cha papo kwa papo nchi zilizoendelea zilianza na mapinduzi ya viwanda na kujenga miundo mbinu karibu karne 2 zilizopita sasa sisi tunajiangalia wenyewe badala ya vizazi vijavyo,halafu unaposema uchumi wa Kenya upo juu je unajua maisha wanayoishi Wakenya ,kweli unaweza kulinganisha na maisha wanayoishi Watanzania? au unasikia tu ngonjera kwenye magazeti,kwanza robo tatu ya uchumi wa Kenya unamilikiwa na mabeberu mabwenyenye wanachi hawana ardhi utakuta familia zinaishi kama manamba kwenye vibanda vya mabati, tembea uone na sio kuwa mfalme tu wa kubofya vitufe. Halafu hao Waethiopia huo uchumi unaosema uko juu kivipi sijui wakati wananchi wake wanafia kwenye makontena wakisafirishwa kama mbuzi,umasikini wa Waethiopia huwezi kulinganisha na umasikini wetu. Narudia tena muwe mnatembea kwanza kwenye nchi za watu mtaona tofauti zilizopo, tena basi na msiishie kwenye majiji makubwa nendeni hadi uswekeni.
 
Umeonesha kumpinga bila ku challenge chochote alichosema zaidi ya kutaja hasara...

 
Jeri yupo sahihi. Wewe ndio mwehu. Muhimu ni kuwa na deni tunalolimudu. Ila kama unategemea ile kampuni isiwe na deni kabisa basi Wewe sahau.

Na ndege hatuziuzi . Mjipange kivingine kama hamuelewei.
Na mwendazake hafufuki na harudi tenaaaaaaaaaa
 
Marekani wamejenga vingi vingine ndo wakaja kwenye hizo NASA za anasa unazozungumzia! Yaana Mtu hana kodi ya nyumba unamwambia anunue hummer, kisa NASA, NASA pori!
Unahisi Marekani hamna masikini au changamoto zozote za kihuduma za kijamii?

Kwaiyo kuwa na national carrier ni anasa? Duh!
 
Facts

Pongezi sana mkuu.
 
British Airways, United Airlines ni mashirika yanayoserve interests za mataifa ya Uingereza na Marekani, kama ulikuwa hujui ndio hivyo umejua sasa. Usipotezwe na majina la wamiliki yaliyoorodheshwa kwenye official websites za hayo mashirika (kumbuka US na UK ni nchi sophisticated, what you see is not always what it is), we elewa tu kwamba linapokuja suala la interests za mataifa hayo, mfano kutangaza utalii wa nchi hizo kupitia airspaces, au ikitokea emergency evacuations katika nchi zisizofikika, na mambo mengine yasiyoweza kuwekwa wazi na nchi hizo, basi elewa kwamba mashirika haya hutumika kikamilifu.

Spin-off benefits ninazoweza kuziweka wazi kwa sasa kupitia ATCL ni ya kuitangaza nchi kupitia airspaces. Jina tu lenyewe "Air Tanzania" ndege ikiwa imepaki Heathrow au Oliver Tambo airports tayari inafanya maelfu ya watu duniani wajue kuwa kuna nchi inaitwa Tanzania. Au we hujui kwanini Kenya inajulikana sana kuliko Tanzania katika domains za kimataifa?

"Sisi tungewaachia wenye uzoefu watoe hiyo huduma ya usafiri wa anga na hivyo vihela vyetu tungevitumia kuboresha maisha ya wananchi wetu."

Unaona sasa ninachokiita akili za kimaskini? Humu duniani kama tungefuata fikra zako basi tungekuwa mafukara kupita kiasi. Ubora wa maisha hautokani na kujikunyata, hao walio wazoefu wa usafiri wa anga walipataje uzoefu huo? Walizaliwa na huo uzoefu? We hujui kwamba kuna watanzania wengi wameajiriwa na ATCL, kwani hao ubora wao wa maisha hautokani na ATCL?
 
Mkuu muulize huyu mbumbumbu Precision imetusaidia nini kwa miaka yote iliyokuwapo? KLM na Ethiopia wsna agenda zao kibiashara sio agenda ya nchi yetu kama utalii na Export.



 
Stupid as stupid goes. Zile ni private entities na zina serve interests za shareholders wake kwanza.
Kama nia ni kutangaza jina la Tanzania si bora wangekodisha mabango makubwa katika nchi hizo? Hivi kweli, wih a straight face, unasema Kenya inajulikana kwa sababu wazungu wanaona Kenya Airways imepaki ndege zake Schipol Airport! Seriously!
Akili ya kimasikini ni kuchukua akiba yako yote kumcheza binti yako kwa wiki nzima ili majirani wakuone. Kama suala ni ajira, bora hizo pesa wangenunulia korosho ili watu wake waweze kuendesha maisha yao badala ya kununua mavitu ambayo haijaajiri hata watu 1000. Tunajisifu kununua ndege kwa pesa taslimu wakati tunasubiri mabeberu kuwajengea vyoo watoto wetu mashuleni mwao!

Amandla...
 
😯😯😯 like seriously!!!!
 
Kazi kweli kweli. Ngoja twende taratibu, utaelewa kidogo kidogo.

"British Airways (BA) is the flag carrier airline of the United Kingdom."

Hiyo sentensi ndiyo sentensi ya kwanza kwenye wikipedia page ya British Aiways. Nini maana ya flag carrier? Maana yake nini kuitwa flag carrier? "A flag carrier is a transportation company, such as an airline or shipping company, that, being locally registered in a given sovereign state, enjoys preferential rights or privileges accorded by the government for international operations."

Kwa tafsiri isiyo rasmi ni shirika la usafiri linalotambulisha nchi husika, na serikali za nchi hizo hulitumia shirika hilo kwa ajili ya "operations" za kimataifa. Neno operations nimeliweka kwenye mabano makusudi ili kama una akili basi ujiongeze. Ninaamini unazo akili so jiongeze.

Mmezoeshwa kujikataa hadi mnatia kinyaa. Mnaingizwa chaka sana na siasa za ushabiki kiasi kwamba hamuwezi kuchambua ni kipi ni maslahi ya umma, na ni kipi ni maslahi ya wanasiasa au maslahi binafsi. ATCL ni shirika la kimkakati la taifa la Tanzania, period. Kama ilivyo Tanesco, kama ilivyo TBC, hayo ni mashirika yanayotambulisha taifa la Tanzania, na kutetea maslahi ya taifa letu. Kama hiyo kazi hawaifanyi vyema hilo ni suala jingine, lakini kama una akili timamu hauwezi kusimama hapa na kutwambia kwamba kama hawafanyi vyema basi tuvunje hayo mataasisi. Huko ni kufeli, ni kutengeneza a failed state, na viongozi wanaotetea ujinga wa kuvunja ATCL ni viongozi failure takataka kabisa.
 
Hawana jipya kabisa yaani wanalipana posho kwa miezi 3 kwenye kinachoitwa Bunge la Bajeti imagine 120,000 kwa siku mara miezi 3 = 10,800,000 jumlisha na mazagazaga mengine na mshahara wao wa kila mwezi zaidi ya Mil 3 balaa sana. Wakati watumishi nwa umma wana miaka 6 hawana hata buku la nyongeza, halafu hawahawa mbulula wanajiita wabunge hawajawahi kusema lolote wanakula wanavimbiwa wanajamba tu hawajui shida za wananchi, hawawezi kuwa na akili yoyote wala mchango wowote wa maana
 
Kizungu kweli kigumu. Wapi wamesema flag carrier inatumbulisha nchi husika? Wapi wamesema kuwa nchi husika inaweza kuitumia kwa operations zake? Au ulipoona international operations ndio ukaelewa hivyo? Hapa wanazungumzia upendeleo katika international operations za shirika hilo. Kwa mfano, watapewa slots zaidi katika kusafiri kati ya Heathrow na JFK. Serikali hata siku moja haitumii ndege za shirika binafsi kwa operations nje ya utaratibu wa wao kuwa wateja kama watu wengine. Serikali kutumia commercial airlines kwa "operations" zake kutazifanya ziwe target halali kama serikali itaingia kwenye vita na nchi nyingine.

Asante kwa kuniita mjinga. Tangu lini Tanesco na ATCL zimekuwa mashirika ya kimkakati. Nchi nyingi tu hazina mashirika yake ya ndege ( Marekani, Uswisn.k.) na yanaenda vizuri tu. Nchi kama India pamoja na kiburi chake wanafanya kila jitihada kuuza Air India lakini kwa sababu wamechelewa sasa haliuziki. Nchi karibu zote za ulaya usambazaji wa nishati unafanywa na mashirika binafsi. Kazi ya serikali ni ku regulate tu.

Tofauti na unavyosema kuendelea kung'ang'ania mashirika kama ATCL ambayo hata huko kwenye watalii hawaendi kwa kuogopa ndege zao kukamatwa na wanaowadai ndio kutatugeuza kuwa failed state. Nchi haipimwi kwa ndege ngapi iliyokuwa nazo bali hali ya huduma kwa wananchi wake ( wangapi wana elimu ya kuwawezesha kumudu maisha yao, upatikanaji kwa urahisi kwa maji safi na salama, upatikanaji wa tiba bora, uhuru wa kujieleza na kuikosoa serikali yao, uhuru wa kuchagua viongozi wanaowataka n.k). Hizo ndege hata katika vipimo vya maendeleo ya nchi hazimo. Sana sana zinatufanya kuonekana vituko katika macho ya ulimwengu maana inathibitisha usemi kuwa waafrika ndivyo tulivyo.

Amandla..
 
unamshambulia bure Jerry, ana point kati hii hoja. wewe ndio umeandika pumba tupu
 
Ninajitahidi sana nikujibu kistaarabu, lakini unanipa tabu sana. Lakini ngoja niendelee hivyo hivyo.

Umeandika mengi lakini nilipofika ulipoandika "uhuru wa kujieleza na kuikosoa serikali yao" ukanichefua. Yaani katika vipimo vya maendeleo kubwabwaja kinyume na taifa lako nayo unaita kipimo cha maendeleo? Na nieleweke, kwamba sitaki kusema unyimwe uhuru wa kujieleza au kukosoa.... lakini nimeshangaa sana namna gani nyie watu mnameza kila kitu mnacholishwa na systems za kibeberu kiasi cha kuweka uhuru wa kukosoa kwenye mizania sawa na huduma bora za afya.

"Nchi nyingi tu hazina mashirika yake ya ndege ( Marekani, Uswisn.k.) na yanaenda vizuri tu."

Soma United Airlines na Swiss International Airlines (zamani SwissAir). Nimekwambia nchi zote duniani zinazojielewa zipo inshu fulani hivi za kinchi ambazo hufanyika kwa wepesi zaidi au kwa maslahi mapana ya nchi yako iwapo una shirika la ndege imara ambalo serikali inaweza kulitumia kwa muktadha huo. Hakuna serikali functional isiyo na shirika lake la "kimkakati" kwa maslahi ya nchi husika. Ukiona mtu au kikundi cha watu kinatushauri tusiwe na shirika la ndege la serikali ujue huyo mtu au hicho kikundi kina ajenda zake. Nchi kama Marekani zipo sophisticated zaidi; na kutokana na nguvu za kiuchumi walizo nazo wana uwezo hata wa kuficha interests za kinchi kwenye private sector, au kujidisguise ionekane kama ni corporate private entity lakini kumbe inaserve interests za nchi ya Marekani.

"Tangu lini Tanesco na ATCL zimekuwa mashirika ya kimkakati"
"Nchi karibu zote za ulaya usambazaji wa nishati unafanywa na mashirika binafsi. Kazi ya serikali ni ku regulate tu."

Huelewi hata ninaposema kimkakati ninamaanisha nini. Unaposema kazi za serikali nchi za Ulaya ni "kuregulate tu" hata hujaeleza nini kilichomo kwenye kuregulate, wanaregulate nini, serikali imeingia mikataba ipi nao hao private generators and distributers? Hata sisi hapa TANESCO ina (ishawahi) kuwa na mikataba na private generators, refer Songas, IPTL, n.k. La muhimu ni to what extent serikali ina control energy sector. Kama level ya regulation haiziruhusu serikali za nchi hizo kuamua umeme uende wapi, ukatwe wapi, usiende wapi na kwa nini, then nchi hizo zitakuwa miongoni mwa nchi dhaifu sana kiusalama. Hata hivyo hii ni kukufumbua macho tu kwamba usidanganywe na neno "regulation". Hao energy suppliers na distributers wa Europe ni insiders wa European governments, wanaoperate kwa niaba ya serikali zao, kwa maslahi ya serikali zao. Nchini mwetu tulijaribu kuexperiment hiyo model na IPTL kilichotokea tukawa tunapigwa 120M kila siku mitambo iwe on au off.
 
Ngoja nikujibu kwa mara ya mwisho. Kukataa kuwa uhuru wa kujieleza na kukosoa ni nguzo mojawapo ya maendeleo inaonyesha fikra zako zilivyo duni. Hivi unadhani bila uhuru wa kukosoa na kujieleza wananchi wanawezaje kuifahamisha serikali kuhusu utendaji mbovu wa wale waliopewa dhamana ya kuwasaidia ili wapate maendeleo? Tumeona utilities wa miradi ya maji isiyotoa maji, barabara zinazoharibika baada ya msimu mmoja ambapo wananchi inabidi wamsubiri Rais ndio watoe dukuduku zao. Uhuru ungekuwepo, matatizo yangemalizika katika ngazi ya DED. Tumeona madaktari wakiogopa kutoa takwimu kuhusu ugonjwa wa Covid kwa kuogopa kushughulikiwa.

United Airlines ni mali ya United Airlines Holdings Inc, kampuni ya kibiashara. Swiss Air ilifilisika na ikafutwa kabisa. Swiss International Airlines imetokana na Cross Air. Ni Crossfire ndio iliyobadilisha jina kuwa Swiss International Airlines. Hayo unayosema kuhusu unayoita mashirika mkakati ni upuuzi tu na zinatokana na kuangalia mno Netflix. Tunashauriwa tusiwe na shirika la ndege la serikali simply kwa sababu hatuna uwezo wa kulihudumia na kuliendesha ipasavyo. Tunajenga hoja kuwa tunanunua ndege ili tulete watalii halafu tunaogopa kwenda huko kwenye watalii kwa kuogopa kuwa zitakamwatwa. Kama tuna mihela mengi kiasi hicho kwa nini tusiwalipe tu wanaotudai? Au kwa nini tusifanye kama walivyofanya waswiss ( Na CAG wa zamani alivyoshauri) kwa kuiacha ATCL ifilisiwe na madeni yafe nayo. Baada ya hapo ndio tujipange kuanzisha shirika lingingine kama tutaona kuna haja ya kufanya hivyo. Nje ya hivyo tutaishia kupeleka Dreamliner Mwanza na Zanzibar.

Regulators kazi yao ni kuhakikisha kuwa umeme wa kutosha unapatikana na kwa bei inayoeleweka. Mambo ya uende wapi au usiende wapi ni mambo ya kibiashara na soko litaamua. Hayo Mambo ya serikali kutaka kuamua umeme ukatwe wapi na ukatwe lini ndio umechangia sana uharibikaji wa mitambo yetu. Hayo maamuzi yanapaswa kufanywa na wataalamu na sio wanasiasa.

Of course, energy distributors wanafanya kazi kwa maslahi ya serikali zao kwa kulipa kodi na kufuata matakwa ya kisera ( sio uendeshaji wa serikali). Kama malengo ya serikali ni kuondokana na fossil fuels nao watawekeza kwenye nishati safi zaidi maana serikali itawaadhibu kwa kuendelea kutoa nishati chafu. Kama hata hilo haulielewi basi hautakuja kuelewa kitu hata kama tukishinda humu siku nzima. Kwa sababu hiyo, sitakujibu tena maana itakuwa kujipotezea muda.

Amandla...
 
Sio wawakilishi wote wana maono sawa wengine ni wasifia matumbo yao kwa sasa tunaita CHAWA wa bossi.

Katika mradi wa hasara ni ndege bora hizo pesa wangejenga bwawa la nyerere na SGR kwenda Arusha toka DSM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…