Mbunge Jesca Msambatavangu: Wanafunzi wanatumia Boom Kubeti badala ya Kusoma. Serikali itafute utaratibu mpya wa kuwakopesha

Mbunge Jesca Msambatavangu: Wanafunzi wanatumia Boom Kubeti badala ya Kusoma. Serikali itafute utaratibu mpya wa kuwakopesha

Mbunge wa Iringa Mjini Madam Jesca Mtambasavangu bila kumung'unya maneno ameshutumu vikali tabia ya wanavyuo kutumia Fedha za Mkopo wa Kujikimu Boom kubeti badala ya kusoma na kutumia Kwa malengo yaliyokusudiwa.

Akiongea Bungeni Kwa Uchumi amewashangaa Vijana wanaodhani betting itawatoa kimaisha na kuiasa jamii kwamba kubeti kunaharibu ubongo na kufanya watu wasiwe critical thinker wawe mazezeta.


My Take
Aliwahi toa maoni kama haya Mbunge Getere na yule wa Kahama ila walishambuliwa sana.

Ukweli ni kwamba Wafunzi wanatumia hizi hela kubeti na kufanya starehe zingine.Naunga mkono wazo la kutafuta utaratibu mwingine wa kutoa hii mikopo ikiwezekana wapewe vyakula Wakiwa Chuo na Mahitaji mengine directly badala ya Fedha mkononi.

Kukalia kimya jambo hili Kwa kujifanya eti halipo au kuogopa kutukanwa au kutumika Kisiasa haisaidii jmaii Bali inakuza ujinga.

Uganda huko Maelfu ya Wanafunzi walifukuzwa Chuo Kwa kula ada Kwa sababu za betting. Pia soma Mbunge

Pia soma: Getere: Boom lifutwe, wanafunzi wanatumia kulewea
Siyo kubeti tu hata mikopo mingi iliyoko kwenye jamii, (mlangoni kwako) inadumaza akili badala ya kubuni njia ya kukuingizia kipato unaenda kukopa, jamani niwekeeni wimbo wa nitoke vipi hahahaa tulikuwa tunajibu Toka kama ulivyo,. Akili zilezile zilizo tengeneza tatizo haziwezi kutatua,(tatizo), changamoto
 
Hapa shida ni elimu ya matumizi sahihi ya fedha. Watoto wafundishwe personal finance toka wakiwa wadogo, jinsi ya kusimamia hela zake binafsi wawe na uelewa.

Sasa mtu anatoka huko bush hajawahi kushika hata laki ya kwawe mwenyewe, anafika chuo mnamrundikia laki 6 ama 7 ghafla kwenye akaunti lazima achanganyikiwe.

Tuwafundishe matumizi sahihi ya fedha, hawatatumia kubeti watafanyia shughuli nyingine za manufaa zaidi.
Kumbuka kuna kupanga kwa wale wanaokaa mbali, kuna kuongezea hela ya boom kwenye ada na inayobaki ndio inakuwa ya matumizi. Mkuu hiyo hela ni ndogo sana kuliko unavyofikiri kwa hawa wanafunzi.Pili kwanini hawa wabunge wanajumlisha wanafunzi wote ni wanabet?
 
Huyu mbunge badala ya kuzungumzia changamoto zilizoko jimboni kwake, unakuja kuwasemea watu wazima amabao wana akili timamu na kulingana na sheria za nchi yetu betting sio halamu. Hivi tuna wabunge wa namna gani nchi hii mbona wanakosa hoja za msingi za kujadili? Magufuli kitendo cha kufanya na kulazimisha tuwe na bunge la chama kimoja limefanya bunge liwe la wapuuzi na hoja zimekuwa za kipuuzi.
 
Kumbuka kuna kupanga kwa wale wanaokaa mbali, kuna kuongezea hela ya boom kwenye ada na inayobaki ndio inakuwa ya matumizi. Mkuu hiyo hela ni ndogo sana kuliko unavyofikiri kwa hawa wanafunzi.Pili kwanini hawa wabunge wanajumlisha wanafunzi wote ni wanabet?
Kila anaegusa hoja ya kuondoa boom hatarudi bungeni.
 
Back
Top Bottom