Mbunge Jesca Msambatavangu: Wanafunzi wanatumia Boom Kubeti badala ya Kusoma. Serikali itafute utaratibu mpya wa kuwakopesha

Siyo kubeti tu hata mikopo mingi iliyoko kwenye jamii, (mlangoni kwako) inadumaza akili badala ya kubuni njia ya kukuingizia kipato unaenda kukopa, jamani niwekeeni wimbo wa nitoke vipi hahahaa tulikuwa tunajibu Toka kama ulivyo,. Akili zilezile zilizo tengeneza tatizo haziwezi kutatua,(tatizo), changamoto
 
Kumbuka kuna kupanga kwa wale wanaokaa mbali, kuna kuongezea hela ya boom kwenye ada na inayobaki ndio inakuwa ya matumizi. Mkuu hiyo hela ni ndogo sana kuliko unavyofikiri kwa hawa wanafunzi.Pili kwanini hawa wabunge wanajumlisha wanafunzi wote ni wanabet?
 
Huyu mbunge badala ya kuzungumzia changamoto zilizoko jimboni kwake, unakuja kuwasemea watu wazima amabao wana akili timamu na kulingana na sheria za nchi yetu betting sio halamu. Hivi tuna wabunge wa namna gani nchi hii mbona wanakosa hoja za msingi za kujadili? Magufuli kitendo cha kufanya na kulazimisha tuwe na bunge la chama kimoja limefanya bunge liwe la wapuuzi na hoja zimekuwa za kipuuzi.
 
Kila anaegusa hoja ya kuondoa boom hatarudi bungeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…