Mbunge Joseph Kasheku Msukuma ataka Magufuli apewe Mihula minne ya Miaka 20 ili kukamilisha miradi

Mbunge Joseph Kasheku Msukuma ataka Magufuli apewe Mihula minne ya Miaka 20 ili kukamilisha miradi

Amefilisiwa na bank ana ogopa akija mwingine atailipaje madeni yake aliyokopa,wanahaha Sana hawa watu,mwacheni mzee wa watu apumzike kwani ataki kupumzika amekuwa punda KILA siku Kazi tu.Watamalizia wengine alipoishia, maana hata apewe miaka 100 bado kuna vitu atovimaliza.
 
Hawa watu wenye akili kama hizi huwa wanafikaje kwenye ngazi ya ubunge?

Sasa kwa ufahamu huu tutafika popote kweli?
Walipita bil kupingwa hofu akiingia mwingine wataishije, kumbuka hawana ujanja wa kuishi nje ya kulipwa,thus wanauwa Hadi watu Ili washinde
 
Amefilisiwa na bank ana ogopa akija mwingine atailipaje madeni yake aliyokopa,wanahaha Sana hawa watu,mwacheni mzee wa watu apumzike kwani ataki kupumzika amekuwa punda KILA siku Kazi tu.Watamalizia wengine alipoishia, maana hata apewe miaka 100 bado kuna vitu atovimaliza.
Sawasawa
 
Akizungumza bungeni leo Mheshimiwa Msukuma kadai hakuna Rais aliyedhubutu Kama Magufuli tangu tupate uhuru.

Akiitolea mfano China yenye maendeleo makubwa huku mihula ya Urais haizingatiwi, kasema sio dhambi kumpa muda zaidi Rais John Magufuli mwenye udhubutu.

Hata hivyo akiichagiza ushauri huoo kwa bunge, Mheshimiwa Spika Job Ndugai alimwambia muda wako umeisha na muda haupo upande wako.

Nashindwa kuipakua video yake Msukuma You Tube na kuiweka humu.
Msukuma inaelekea kuwa hajui kuwa hata hayo maendeleo ya China yalikuwa wakati wakiwa na term limits.
 
Tanzania kuna wapinzani ? Mimi najua kuna wanaharakati tu. Wapinzani watoke wapi nchi hii ? Usitudanganye hapa eti wewe mpinzani, wa kitu gani hasa ?
Mimi nimeleta tu alichokiongea huyo mbunge wa ccm ili watu wakione. Mimi sipo upande wa ccm mimi ni mpinzani
 
Unakumbuja Nyerere aliongiza kwa muda gani ? Ni miaka 23 ndio akafanya hayo. Kwa hiyo Lazima tujitafakari kuioitia katiba upya
Musukuma asitufanye sisi sote ni wa la Saba Kama yeye. Ni kitu gani cha ajabu ambacho Magufuli amefanya Mtanzania mwingine hawezi?? Angalia mambo ya Nyerere hapa;
Nyerere alijenga madaraja makubwa kama Kirumi, Selander, Wami, Mara na mengine mengi.
Nyerere alijenga viwanda vya kuchakata mazao ya Pamba, Kahawa, Pareto, Chai, Ngozi, Nyama, Maziwa, Viatu.
Nyerere alinunua Meli na vivuko (Panton) katika maeneo kadhaa nchini.

Nyerere alijenga viwanda vya kutengeneza Vifaa/Zana za kilimo, Mbolea, Madawa, Magurudumu n.k
Wakati wa Nyerere wanafunzi walisoma na kusafiri kwenye usafiri wa umma bure.
Nyerere alijenga Reli ya TAZARA

Pamoja na mambo mengine kede kede na kuwafanya Watanzania kuwa wamoja na upendo bila chuki za kikabila kisiasa au ukanda.

Lakini bado aliondoka madarakani kwa hiari yake mwenyewe (kung'atuka) na hakuogopa ama kuhofia kwamba akiondoka madarakani ni nani atafanya kama yeye!

Vimbwanga vya kutaka kuaminisha watanzania kwamba hakuna mwingine mwenye uwezo wa kufanya kama WEWE yanatokea wapi???
 
Katiba siyo msahafu inaweza badilishwa tu
Katiba yetu imetamka wazi kwamba ni awamu mbili achia ngazi wengine waingie..akiruhusiwa kuendelea kisa kafanya miradi mingi inatia mashaka kwa sababu hakuna rais ambae hakufanya jitihada zake ili kuweza kutoka hali moja kwenda nyingine, Pale walipofikia muda wao ukawa umeisha waliendeleza waliofuatia katika ngazi hio ya rais.Tz wakifanya makosa ya kubadili katiba ili magufuli aendelee kuwa madarakani,tutaenda kupoteza dira kama taifa.
 
Miradi isiyogusa watu ndiyo ipi? Halafu jaribu kutumia kichwa chako vizuri, kumbuka siyo kila anayetoa mawazo dhidi ya Magu Ni CHADEMA!! Angalia ubora wa hoja tu
Ni CHADEMA ndio vichwa maji. Wanawaza kupiga deal tu
 
Acha ubinafsi mkuu....mishahara ni kwa ajili ya watumishi, reli na Umeme ni kwa ajili vizazi vya sasa na vijavyo!
SGR na gorge yake na miradi mingine ya kukurupuka ambayo imezima ajira na nyongeza za mishahara bado inamuwazisha kichwa , ameona haitakamailika anataka ajimilikishe hii nchi
 
😏😏🙄🙄😶😶😑😉😎😟😞☹😲😒😮😯
 
Kwani Musukuma ana elimu gani. Hebu tuanzie hapo!

Tusije tukawa tunamsikiliza layman aliyepata bahati ya kuwa bungeni kwa kusaidiwa na wizi wa kura!

Anafikiri maendeleo ya China yameletwa na Xi Jinping peke yake?
Mpinge Mtu kwa Hoja na siyo kwa Kumdharau kuhusu Elimu yake tafadhali. Kama Elimu Kwako ni Tija sana mbona Tanzania yetu hii miaka nenda rudi inaongozwa na hao hao Wasomi wako lakini bado nchi yako inasuasua kama si kujikongoja katika kuyatafuta Maendeleo ya kweli?

Najua kuwa Mbunge Msukuma hakupata Elimu Kubwa kama walizonazo wengine ila kuna Hoja zingine ambazo huwa anaziibua Bungeni na Kuzijenga vyema kuliko hata hso Wasomi na hizo Elimu zao.

Huwa sipendi Mtu aliyebahatisha au kupata tu fursa ya Elimu halafu akaitumia hiyo Elimu yake ambayo hata Yeye Mwenyewe japo anayo Kuwadharau wasio kuwa nayo, na pengine haijamsaidia chochote ila anajitutumua nayo tu hapa JamiiForums ambapo bahati mbaya wengi Wetu hatujuani Kiuhalisia.
 
Hii sasa inaitwa uelewa una decrease in increasing rate
 
Akizungumza bungeni leo Mheshimiwa Msukuma kadai hakuna Rais aliyedhubutu Kama Magufuli tangu tupate uhuru.

Akiitolea mfano China yenye maendeleo makubwa huku mihula ya Urais haizingatiwi, kasema sio dhambi kumpa muda zaidi Rais John Magufuli mwenye udhubutu.

Hata hivyo akiichagiza ushauri huoo kwa bunge, Mheshimiwa Spika Job Ndugai alimwambia muda wako umeisha na muda haupo upande wako.

Nashindwa kuipakua video yake Msukuma You Tube na kuiweka humu.
Tunamtakia kila la heri
 
Back
Top Bottom