Mbunge Joseph Kasheku Msukuma ataka Magufuli apewe Mihula minne ya Miaka 20 ili kukamilisha miradi

Mbunge Joseph Kasheku Msukuma ataka Magufuli apewe Mihula minne ya Miaka 20 ili kukamilisha miradi

Magufuli ni raisi tunayemuhitaji kwa kipindi kirefu, idgaf about democracy, wewe umemtaja Nyerere mbona hao wengine hujawataja michango yao?for me baada ya Nyerere ni Magufuli, hatuwezi kuwa na democracy inayotuletea viongozi wa ovyo ovyo, mfano Tundu lisu angeshinda 2020, ingekuwa ni miaka mi 5 mipya ya upuuzi, cha msingi Magufuli ana weakness zake, kelele ipigwe ajirekebishe yeye siyo Mungu kuwa hakosei, ndio maana huwa anarudi nyuma na kusahihisha (kusamehe)

Hawa politician wengi wanawaza matumbo yao, madaraka, wanadhani wakishafika level flani basi cha mwisho ni kuwa raisi, uzalendo hamna. As long as haki za binadamu zinazingatiwa, Magufuli is my president, ila naye ajirekebishe, mkali sana mpaka wasaidizi wake wanaogopa kumshauri
Tuheshimu Katiba iliyopo japo ina mapungufu. Kama tunataka kupanua muda wa ukomo wa uongozi wa nchi, basi tuanzie kwenye mchakato wa Katiba.

Halafu tukiongeza muda iwe ni haki ya watu wote kugombea including Jakaya Kikwette na Mwinyi waliopo hai. Tusijidandanye kwamba JPM anapendwa au amefanya mambo makubwa kuliko wengine. Ngoja tuweke uwanja sawa tuone kama anaweza kupata hata 10% ya Jakaya Kikwette.

JPM kwa huu uchaguzi wa 2020 kiukweli aliiba uchaguzi wote. Yaani kura zilitengenezwa na ma DSO wa kila wilaya. Halafu vyombo vya habari haviko huru kuandika ukweli. Vikiandika vinafungiwa na Dr Abbas Katibu Mkuu Habari.

TUSIDANGANYIKE, kuna watu wana vision kuliko MAGUFULI na wanaweza kuifanya Tanzania ikapiga hatua bila kuua wakosoaji wala kunyang'anya fedha za matajiri.
 
Hawa watu wenye akili kama hizi huwa wanafikaje kwenye ngazi ya ubunge?

Sasa kwa ufahamu huu tutafika popote kweli?
 
Msukuma ni k!, japo wazo hili limeshapita, imekula kwangu.
 
Akizungumza bungeni leo Mheshimiwa Msukuma kadai hakuna Rais aliyedhubutu Kama Magufuli tangu tupate uhuru.

Akiitolea mfano China yenye maendeleo makubwa huku mihula ya Urais haizingatiwi, kasema sio dhambi kumpa muda zaidi Rais John Magufuli mwenye udhubutu.

Hata hivyo akiichagiza ushauri huoo kwa bunge, Mheshimiwa Spika Job Ndugai alimwambia muda wako umeisha na muda haupo upande wako.

Nashindwa kuipakua video yake Msukuma You Tube na kuiweka humu.
Kwa maelezo ya msukuma ni kwamba magufuli amefeli kutekeleza majukumu yaliyo kwenye ilani ya chama ndani ya miaka mitano ya kwanza na hawana uhakika kama ataweza kwenye miaka mitano ya mwisho ndo maana wanaomba aongezewe. swali, kama ameshindwa majukumu ya miaka mitano je ataweza miaka mingine ikiongezwa kwani na ilani itakuja na mambo mengine mapya?
 
Akizungumza bungeni leo Mheshimiwa Msukuma kadai hakuna Rais aliyedhubutu Kama Magufuli tangu tupate uhuru.

Akiitolea mfano China yenye maendeleo makubwa huku mihula ya Urais haizingatiwi, kasema sio dhambi kumpa muda zaidi Rais John Magufuli mwenye udhubutu.

Hata hivyo akiichagiza ushauri huoo kwa bunge, Mheshimiwa Spika Job Ndugai alimwambia muda wako umeisha na muda haupo upande wako.

Nashindwa kuipakua video yake Msukuma You Tube na kuiweka humu.
Binafsi nashangaa hoja ya Mh. Msukuma ya kuongeza muda ili Mh. Rais aendelee na majukumu aliyoyaanzisha ya kukuza uchumi.
Msingi wa kukataa ni huu;
1.Kwa kuwa Mh. Mbunge amekiri kuwa miradi inayotekelezwa sasa haina tija kwa wananchi wa hali ya chini inakuaje Mh. Rais aendelee kukaa madarakani?
2.Kwa kuwa Mh. Rais aliwahi kusema hadharani akiwa Korogwe kuwa hatoongeza muda wa Urais, inakuaje Waheshimiwa wabunge wanaendelea kumlazimisha huko si kumkosea Mh. Rais na kuivunja katiba na ku tumia muda wa kujadili vitu vingine vyenye maslahi kwa nchi vibaya.?
3.Mh.Mbunge kusema kuwa biashara zinafungwa awamu hii, je ndani ya miaka 20 si biashara zote zitakuwa hoi bin taabani?
Mh. Mbunge katika hotuba yake alipatia sana mwanzoni, lakini mwishoni aliharibu kwa kumchongea Mh. Rais /kujipendekeza ili aonekane anampenda Mh. Rais kwa hoja ya kumuongezea muda.
Hata hivyo suala la kujadili muda /ukomo wa Urais lisiwe wakati huu,lisubili hadi pale miaka yake hii mitano itakapoisha alafu tathmini ifanywe ili kama itaonekana inafaa si dhambi kumuongezea muda Mh. Rais ilimradi nayeye akubali kututumikia na sio kumlazimisha.
 
Kwani Musukuma ana elimu gani. Hebu tuanzie hapo!

Tusije tukawa tunamsikiliza layman aliyepata bahati ya kuwa bungeni kwa kusaidiwa na wizi wa kura!

Anafikiri maendeleo ya China yameletwa na Xi Jinping peke yake?
Vilaza aina ya musukuma ndio upeo wao ulipoishia. Wanafikiri Watanzania wote ni vilaza kama wao. Magufuli yeye kama yeye kitu gan cha tofauti na wengine amefanya? Tangu tupate uhuru tumekua tunajenga miundombinu, huku maisha yakiendelea km kawada- bila watu kupotea, kupigwa risasi, kuuwawa au kuokotwa ndani ya viroba
 
Binafsi nashangaa hoja ya Mh. Msukuma ya kuongeza muda ili Mh. Rais aendelee na majukumu aliyoyaanzisha ya kukuza uchumi.
Msingi wa kukataa ni huu;
1.Kwa kuwa Mh. Mbunge amekiri kuwa miradi inayotekelezwa sasa haina tija kwa wananchi wa hali ya chini inakuaje Mh. Rais aendelee kukaa madarakani?
2.Kwa kuwa Mh. Rais aliwahi kusema hadharani akiwa Korogwe kuwa hatoongeza muda wa Urais, inakuaje Waheshimiwa wabunge wanaendelea kumlazimisha huko si kumkosea Mh. Rais na kuivunja katiba na ku tumia muda wa kujadili vitu vingine vyenye maslahi kwa nchi vibaya.?
3.Mh.Mbunge kusema kuwa biashara zinafungwa awamu hii, je ndani ya miaka 20 si biashara zote zitakuwa hoi bin taabani?
Mh. Mbunge katika hotuba yake alipatia sana mwanzoni, lakini mwishoni aliharibu kwa kumchongea Mh. Rais /kujipendekeza ili aonekane anampenda Mh. Rais kwa hoja ya kumuongezea muda.
Hata hivyo suala la kujadili muda /ukomo wa Urais lisiwe wakati huu,lisubili hadi pale miaka yake hii mitano itakapoisha alafu tathmini ifanywe ili kama itaonekana inafaa si dhambi kumuongezea muda Mh. Rais ilimradi nayeye akubali kututumikia na sio kumlazimisha.
Wewe nawe mwishoni ndio umeharibu kabisa.
 
U
Anatukomoa watanzania
Mtu anaetegemea ndumba ndo aishi katu hawezi kuwa perfect. Kiongozi wa china sio mwizi, fisadi, mkabila, kujaza ndugu zake KILA mahali, hana dabo standard kwenye kudeal na ufisadi, ajengi kijijini kwake asomeshi namba Ili aabudiwe, anajenga nchi, abomoi nchi, akomoi matajiri kwake ni sahihi hata akiongeza.Hofu ni Hawa wenye mikopo mikubwa wataishije watailipaje akiondoka mungu wao kwao tumbo ni best kuliko wanyonge wanaonyongwa na Utawala huu dhalimu.
 
Hawa eti ndio wabunge,watu wanakufa kama kuku kwa changamoto za upumuaji wao wanawaza kuongezeana muda wa Ku**rana
 
Kwa nini tunashupalia na kutaka kujadili kitu ambacho hakina uhakika? Je kuna mtu anayeijua kesho yake? Hivi watu wanavyokufa ghafla hatuoni kuna tatizo mahala fulani? Nani mwenye kujua huko 2025 atakuwepo? Pengine wengi wetu 2021 hatutoimaliza kwani sisi sote ni wafu watarajiwa.
Wakina Msukuma waangalie na kuzungumzia mambo yaliyopo siyo kuzungumzia raisi aongezew muda, na ikiwa CCM inatekeleza ilani ya chama sijaona tatizo raisi akimaliza muda wake kuondoka, unless ikiwa CCM inatekeleza ilani ya Magufuli hapo wampigie debe mpaka atakapomaliza kutekeleza ilani zake au Mungu akimuhitaji.
Nadhani tuongeze maombi ya kuwa na viongozi wenye maono na wenye kujali wanaowaongoza.
 
Back
Top Bottom