Mbunge Joseph Kasheku Msukuma ataka Magufuli apewe Mihula minne ya Miaka 20 ili kukamilisha miradi

Mbunge Joseph Kasheku Msukuma ataka Magufuli apewe Mihula minne ya Miaka 20 ili kukamilisha miradi

Fungeni kamba haraka mtu amesahau kumeza dawa zake..
 
Katiba yetu imetamka wazi kwamba ni awamu mbili achia ngazi wengine waingie..akiruhusiwa kuendelea kisa kafanya miradi mingi inatia mashaka kwa sababu hakuna rais ambae hakufanya jitihada zake ili kuweza kutoka hali moja kwenda nyingine, Pale walipofikia muda wao ukawa umeisha waliendeleza waliofuatia katika ngazi hio ya rais.Tz wakifanya makosa ya kubadili katiba ili magufuli aendelee kuwa madarakani,tutaenda kupoteza dira kama taifa.
wasaliti na wahaini wa nchi hii ni WABUNGE NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA Vimekosa huruma na waTZ
 
Nchi haitafuti Mpishano wa Viongozi kwenda Ikulu. Bali tuna hitaji kiongozi kama Magufuli Mjomba.

Watu kama Hawa ni Adimu sana Mjomba. Tunapo mpata hatuna budi tumtumie Mjomba.

Magufuli 10 Tena 👐👐👐👐
Nawapashaga Chadema humu JF, ila inonekana kuna watu wapuuzi kama wewe
 
zile kanda zilizokua zinajisifu na kujiona ni bora sana kuliko kanda zingine,naona ndo zinaongoza kumwaga mapovu hapa.Sisi wa lindi na mtwala wala hatuna makuu nyie pambaneni tu
 
Akizungumza bungeni leo Mheshimiwa Msukuma kadai hakuna Rais aliyedhubutu Kama Magufuli tangu tupate uhuru...
Jamani mie nina wazo. Hawa wanaotaka kutuletea hili janga jamii iwagomee na kuwatenga na familia zao. Yoyote yule alieropoka haya mambo ya kuengezeana muda, popote aliposemea hafai kuwa katika jamii yetu kwa sababu ni wabinafsi.

Ni kama vile hawaoni yanayoendelea wao wanajali matumbo yao na ya familia zao tu. Natoa wito shime watanzania wote tuwagomee wabinafsi hawa kwa kila hali ili liwe funzo kwa wengine!
 
Naunga mkono hoja. Katiba sio msaafu inabadilika tokana na mahitaji na wakati.

Jiwe ✊ ✊✊
 
Mbona hoja yake ya miradi isiyogusa wananchi tuachane nao Ufipa Wote mlishangilia na hamkumuita Darasa la Saba.Saizi ni kilaza Bwashee
Miradi isiyogusa watu ndiyo ipi? Halafu jaribu kutumia kichwa chako vizuri, kumbuka siyo kila anayetoa mawazo dhidi ya Magu Ni CHADEMA!! Angalia ubora wa hoja tu
 
Mihula yake miwili inatosha,hatujawatuma kuongeza muda wa Magufuli bali kuongelea changamoto inayowakabili watanzania,hasa katika kipindi chake hichi,bei ya vitu imepanda lakini kipato cha mtanzani ni kilekile,kama mna mpango wa kujenga huko kwenu Geita malizieni katika awamu hii ya mwisho, Kikwete aliakuwa na mradi mkubwa wa bandari Bagamoyo,Bwana mkubwa alipoingia akaufutilia mbali,naye asubiri muda wake ukiisha uwanja wa ndege wa Chato utabakia vichakani,sidhani kama kuna shirika la ndege litafanya kazi ya hasara ya kubeba abiria wachache.
 
Hapo ndipo alipoboa. JPM kipenzi cha wengi akamilishe miaka yake 10 na 2025 akabidhi kijiti kwa mwingine. Hizi ngonjera za akina Msukuma ni za kupuuzwa
Kinacho nistaajabisha hadi sasa wabunge walio ishia la pili c ndio wanao taka JPM aongezewe mda sijui kwanini
Kaanza deo sanga sifa hajui kusoma wala kuandika
Leo msukuma sifa darasa la saba , itakuwa ajabu wabunge wasomi wakiungana na hawa vilaza na walafi wa madaraka.
 
"Haya mambo ambayo tunaona Rais ameyafanya tunaweza kuona namna tukamuongezea muda, kwani kitu gani mbona wenzetu wamefanya?, ina maana sisi watanzania tunaijua demokrasia zaidi ya wachina ambao ni matrilionea wamefka mahal wakaona tumuongeze Mtu hata miaka 20 mbele"---- MUSUKUMA
Hatutaki
 
"Haya mambo ambayo tunaona Rais ameyafanya tunaweza kuona namna tukamuongezea muda, kwani kitu gani mbona wenzetu wamefanya?, ina maana sisi watanzania tunaijua demokrasia zaidi ya wachina ambao ni matrilionea wamefka mahal wakaona tumuongeze Mtu hata miaka 20 mbele"---- MUSUKUMA
Ukiwa na akili ndogo halafu una influence ni msiba kwa jamii maana utatumia vibaya karama hizo na kwakuwa maccm huwa hayasomi vitabu basi ni shida. Mkapa alishaona ubaya wa extension ya muda wa kukaa madarakani na alionya.
 
Ukiwa na akili ndogo halafu una influence ni msiba kwa jamii maana utatumia vibaya karama hizo na kwakuwa maccm huwa hayasomi vitabu basi ni shida. Mkapa alishaona ubaya wa extension ya muda wa kukaa madarakani na alionya.
Mkuu kwa huyu yohana alivyo na tamaa pia katuumiza watu wengi sana kwenye utawala wake ni dhahiri kabisa kutoka kwake kwenye kiti haitakuwa rahisi maana anaogopa naye atakuja kuumizwa kama alivyoumiza watu hivi sasa
 
Back
Top Bottom