Akizungumza bungeni leo Mheshimiwa Msukuma kadai hakuna Rais aliyedhubutu Kama Magufuli tangu tupate uhuru...
Musukuma asitufanye sisi sote ni wa la Saba Kama yeye. Ni kitu gani cha ajabu ambacho Magufuli amefanya Mtanzania mwingine hawezi?? Angalia mambo ya Nyerere hapa;
Nyerere alijenga madaraja makubwa kama Kirumi, Selander, Wami, Mara na mengine mengi.
Nyerere alijenga viwanda vya kuchakata mazao ya Pamba, Kahawa, Pareto, Chai, Ngozi, Nyama, Maziwa, Viatu.
Nyerere alinunua Meli na vivuko (Panton) katika maeneo kadhaa nchini.
Nyerere alijenga viwanda vya kutengeneza Vifaa/Zana za kilimo, Mbolea, Madawa, Magurudumu n.k
Wakati wa Nyerere wanafunzi walisoma na kusafiri kwenye usafiri wa umma bure.
Nyerere alijenga Reli ya TAZARA
Pamoja na mambo mengine kede kede na kuwafanya Watanzania kuwa wamoja na upendo bila chuki za kikabila kisiasa au ukanda.
Lakini bado aliondoka madarakani kwa hiari yake mwenyewe (kung'atuka) na hakuogopa ama kuhofia kwamba akiondoka madarakani ni nani atafanya kama yeye!
Vimbwanga vya kutaka kuaminisha watanzania kwamba hakuna mwingine mwenye uwezo wa kufanya kama WEWE yanatokea wapi???