Mbunge kusimama Bungeni kutaka Rais aongezwe muda wa kukaa madarakani. Je, Umewasiliana na waliokutuma uwawakilishe hapo Bungeni au ni mawazo yako?

Ukitaka kuua nyoka anza kuangalia miguuni kwako, usianzie nyumba ya pili wakati chumba chako kinaweza kuwa na nyoka.

Demokrasia ya vipindi vya uongozi tunge anza kwenye vyama vyenu tungesikilizwa sana. Lakini vipindi au muda wa uongozi sisi hatutaki heshima na tunataka wenzetu wa heshima ni double speak.

Mbowe tumempa miaka 25 ya kuongoza, wana CCM wanataka wamuongezee mwenyekiti wao miaka 5, ili iwe jumla miaka 15 sisi midomo juu kama vile nchi ni mbili.

Wao wanataka kumuongezea muda Mwenyekiti wao CCM miaka mingine mitano akimaliza hii mitano, tatizo ni nini? Au kwa kuwa Mwenyekiti wa CCM ni mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania?
 
Wabunge msijisahau Wananchi wamewatuma muwawakilishe tafadhali msifanye mambo kama mmejipeleka wenyewe Bungeni msiwe walafi wa madaraka

Maana kelele hizi za kutaka Rais abaki madarakakani si kwamba ni kweli mnampenda abaki kwa sababu amefanya mazuri kuliko walio pita hapana bali kwa sababu mnajua kabisa kubaki kwake madarakani ndio kubaki kwenu madarakani

Rais tafadhali usiuvae mkenge huu wa Wabunge wanye ulafi wa madaraka mkwa sababu walio pita nao wangekuwa na mawazo kama hayo hata Rais wa sasa asinge ipata nafasi hiyo.
Hicho chama kimejaa wachumia tumbo tupu,
tapatalk_1612397829016.jpeg
 
Katiba yetu hairuhusu jambo hilo.
Nakumbuka Mwalimu Nyerere alikemea jambo hilo,lakini na yeye alishutuka baada ya kuondoka madarakani.
Magufuli mwenyewe hataki kuongeza hata dakika mmoja.
Kama Chadema wamebadilisha ukomo wa uongozi, CCM wakibadilisha katiba yao taabu iko wapi?

Wote wenye akili timamu ya Siasa ya nchi hii wanajua katiba tulio nayo ni ya CCM na sio ya wananchi, wanaweza kuibadili kwa kuwa ndio walio iweka.
 
Kwa hoja hii, inashangaza Sana na inasikitisha, sijui wamechoka amani waliyonayo au shibe imepitiliza katiba tulinayo ipo wazi. Kama gains Cha kuongea bungeni piga usingizi, ujatumwa hayo na wananchi
 
Kwani wewe mleta mada unajuaje kama mbunge hajatumwa na watu wake kutoa hayo maoni. Nyinyi si waumini wa demokrasia? Na demokrasia si maana yake uhuru wa kutoa maoni. Sasa kwa nini umfundishe mtu maoni haya mazuri yale mabaya. Ukiufuata ujinga unaufuata mpaka mwisho. Vivyo hivyo ukiifuata demokrasia unaifuata mpaka mwisho.

Kusema watu wasijadili ukomo wa urais ni udikteta. Kama wewe unadhani ukomo wa vipindi viwili ndiyo sahihi yupo mwingine yeye anataka kiwe kimoja. Kuna mwingine anataka viwe vitatu! Ndiyo, ndiyo demokrasia hiyo.

Maoni yangu: Suala la ukomo wa mihula ya urais linahitaji busara ya hali ya juu. Maamuzi yoyote sharti yafanyike kwa uwazi na iwe juu ya wananchi wenyewe kuamua. Wala bunge lisijitwike madaraka hayo.

Ikiwa bunge litaona linataka kufanya hivyo sharti likabidhi suala hilo kwa wenye nchi wenyewe waamue wanachotaka kupitia mchakato wa wazi.

Hapana shida yoyote wananchi kumwongezea rais wao muda wa kukaa madarakani. Vivyo hivyo wananchi wakiamua wampunguzie rais muda wa kukaa madarakani. Ndiyo demokrasia hiyo.

Tuache maigizo kwenye demokrasia kama wanavyoigiza wamiliki wa JamiiForums. Nje wanapigania demokrasia. Lakini huku ndani ukisajili ID huwezi hata kuibadili kirahisi. Ukitaka kuifuta ndiyo sahau kabisa! Ila unaambiwa ni wanaharakati wa uhuru wa habari na demokrasia na tuzo wanapewa! Siyo kwa chuki, ni ukweli tu; demokrasia.
 
Kuna baadhi ya binadamu wana hulka za kibinafsi ma kinafiki sana. Ngoja tuone mpaka hiyo 2025 itakuwaje.

Akiongezewa/Akijiongezea huo muda, hakika Wafanyakazi wengi wa umma wenye mioyo myepesi tutaacha/tutafukuzwa kazi.

Mwisho wa uvumilivu wa huu unyonyaji na dhuluma dhidi yetu, ni 2025!
 
Wabunge msijisahau Wananchi wamewatuma muwawakilishe tafadhali msifanye mambo kama mmejipeleka wenyewe Bungeni msiwe walafi wa madaraka

Maana kelele hizi za kutaka Rais abaki madarakakani si kwamba ni kweli mnampenda abaki kwa sababu amefanya mazuri kuliko walio pita hapana bali kwa sababu mnajua kabisa kubaki kwake madarakani ndio kubaki kwenu madarakani

Rais tafadhali usiuvae mkenge huu wa Wabunge wanye ulafi wa madaraka mkwa sababu walio pita nao wangekuwa na mawazo kama hayo hata Rais wa sasa asinge ipata nafasi hiyo.
Mbunge hufanya kazi bungeni kwa kufuata mawazo ya wananchi wake,na pia ana haki ya kutumua conscious yake binafsi,mradi kama ni kwa faida ya umma
 
Wabunge msijisahau Wananchi wamewatuma muwawakilishe tafadhali msifanye mambo kama mmejipeleka wenyewe Bungeni msiwe walafi wa madaraka

Maana kelele hizi za kutaka Rais abaki madarakakani si kwamba ni kweli mnampenda abaki kwa sababu amefanya mazuri kuliko walio pita hapana bali kwa sababu mnajua kabisa kubaki kwake madarakani ndio kubaki kwenu madarakani

Rais tafadhali usiuvae mkenge huu wa Wabunge wanye ulafi wa madaraka mkwa sababu walio pita nao wangekuwa na mawazo kama hayo hata Rais wa sasa asinge ipata nafasi hiyo.
Wabunge na rais lao moja wamefanya kiini macho kuwa wanaomba rais aongezewe muda lakini hilo liko kwenye ilani yao kisiri siri ukitaka kujua rejea uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020 hapo ndiyo utajua lengo la serikali iliyopo madarakani.
 
Wabunge msijisahau Wananchi wamewatuma muwawakilishe tafadhali msifanye mambo kama mmejipeleka wenyewe Bungeni msiwe walafi wa madaraka

Maana kelele hizi za kutaka Rais abaki madarakakani si kwamba ni kweli mnampenda abaki kwa sababu amefanya mazuri kuliko walio pita hapana bali kwa sababu mnajua kabisa kubaki kwake madarakani ndio kubaki kwenu madarakani

Rais tafadhali usiuvae mkenge huu wa Wabunge wanye ulafi wa madaraka mkwa sababu walio pita nao wangekuwa na mawazo kama hayo hata Rais wa sasa asinge ipata nafasi hiyo.
Nitarudi kukujibu kwanini Magufuli apewe 5 miningine.
 
Jiwe linatutega boss ,si kweli kama halitaki kubakia
Katiba yetu hairuhusu jambo hilo.
Nakumbuka Mwalimu Nyerere alikemea jambo hilo,lakini na yeye alishutuka baada ya kuondoka madarakani.
Magufuli mwenyewe hataki kuongeza hata dakika mmoja.
 
Mkuu mbona umeongea kana kwamba wewe haya hayakuhusu?
Mliambiwe mkaandamane mkasema waache waende wao na familia zao. Sasa wao wapo nje ya nchi wanakula bata sa hivi nyie mliobaki kwenye shithole mnazidi kunyooshwa. Hakuna mbunge kachaguliwa na wananchi, wamepachikwa pale na jiwe. Kaeni mnyooshwe mtajifunza na nyie kudai haki yenu jiwe litawakamua left and right hadi there’s nothing left
 
Ukitaka kujua huyu Mzee ana kasoro kubwa sana aachie madaraka japo mwezi mmoja halafu sikia hizo kashfa zitakazoibuliwa.
Hili halina mjadala mkitaka msitake Mheshimiwa Magufuli tunamuongezea mingine,sasa jamani mtu huyu hana kasoro kubwa sana za kiuongozi na imeonekanika kabisa sio hapa Tanzania tu,dunia nzima na ulimwengu wake hata huku kwenye ulimwengu wa tatu wananchi wa nchi nyingi wanawaonea gere wananchi wa Tanzania kwa kupata kiongozi mchapa kazi,kasoro ndogondogo ni za kiubinadamu ambazo hakuna anaeweza kuziepuka,kasoro hizo wazungu au mabeberu wanaziita minor yaani vitu viduchu viduchu,ambavyo haviathiri utendaji wake wa kazi.

Sasa wewe usietaka aendelee miaka mingine unataka utuletee mjomba wako ? na mkileta za kuleta tunaondoa hata uchaguzi kwani waTanzania hawana sababu ya kufanya uchaguzi kwa kuwa aliekuwepo anatosha,yanini kupoteza hela,ambazo zinaweza kutumika kuendeleza mfumuko wa miundo mbunu,

Sasa hivi WaTanzania tunahitaji Express train Mwanza tu Mtwara na hela ikitosha tunajenda ring road ya Tanzania nzima ikienda sambamba na reli, hii Ring road ndio mwisho ,sijui hawa wapinzani hewa kama wanelewa faida ya Ring road au wanaelewa ni kitu gani.
 
Ukitaka kujua huyu Mzee ana kasoro kubwa sana aachie madaraka japo mwezi mmoja halafu sikia hizo kashfa zitakazoibuliwa.
Hili halina mjadala mkitaka msitake Mheshimiwa Magufuli tunamuongezea mingine,sasa jamani mtu huyu hana kasoro kubwa sana za kiuongozi na imeonekanika kabisa sio hapa Tanzania tu,dunia nzima na ulimwengu wake hata huku kwenye ulimwengu wa tatu wananchi wa nchi nyingi wanawaonea gere wananchi wa Tanzania kwa kupata kiongozi mchapa kazi,kasoro ndogondogo ni za kiubinadamu ambazo hakuna anaeweza kuziepuka,kasoro hizo wazungu au mabeberu wanaziita minor yaani vitu viduchu viduchu,ambavyo haviathiri utendaji wake wa kazi.

Sasa wewe usietaka aendelee miaka mingine unataka utuletee mjomba wako ? na mkileta za kuleta tunaondoa hata uchaguzi kwani waTanzania hawana sababu ya kufanya uchaguzi kwa kuwa aliekuwepo anatosha,yanini kupoteza hela,ambazo zinaweza kutumika kuendeleza mfumuko wa miundo mbunu,

Sasa hivi WaTanzania tunahitaji Express train Mwanza tu Mtwara na hela ikitosha tunajenda ring road ya Tanzania nzima ikienda sambamba na reli, hii Ring road ndio mwisho ,sijui hawa wapinzani hewa kama wanelewa faida ya Ring road au wanaelewa ni kitu gani.
 
Wabunge msijisahau Wananchi wamewatuma muwawakilishe tafadhali msifanye mambo kama mmejipeleka wenyewe Bungeni msiwe walafi wa madaraka
Mbunge amewakilisha maoni ya wananchi wake: wewe kwanini unapinga?, wananchi wamekutuma uwasemee?
 
Ukitaka kujua huyu Mzee ana kasoro kubwa sana aachie madaraka japo mwezi mmoja halafu sikia hizo kashfa zitakazoibuliwa.
Kila jambo lina sura mbili
 
Kuuliza kwamba mbunge aliwasiliana na waliomchagua kabla ya kuwasilisha hoja bungeni si sahihi. Nahisi unahoji hivyo kwa kuwa hoja husika hukubaliani nayo. Hoja ipi ambayo unakubaliana nayo ambayo mbunge aliita wananchi wa jimbo lake wakakubaliana kwamba awasilishe hoja hiyo?

Niseme wazi kwamba hata mimi sikubaliani kabisa na hoja ya kumwongezea muda Rais JPM kwani Bunge siyo chombo cha kumtungia sheria mtu mmoja mmoja kufuatana na jinsi anavyoonekana kwa mambo ya mpito bali kibaki chombo cha kutunga sheria za kudumu kwa manufaa ya nchi kwa ujumla. La sivyo itakuwa huyu aongezewe mitano; yule mitatu na mwingine ishirini, kufuatana na mihemko wanayoipata watu katika kipindi husika. Huu ni uchuro utakaoiharibu nchi.

Pamoja na kupinga hoja ya mbunge, tusitumie hoja za kuuliza kama mbunge ameshauriana na waliomchagua kabla ya kufikisha hoja bungeni. Hakuna mbunge anayofanya hivyo kama modus operandi. Uzuri ni kwamba JPM mwenyewe ameisha sema mara kadhaa kwamba hakubaliani na wazo hilo.
Umeandika maneno mengi sana yenye mantiki lakini umesahau malengo ya ndugai,magu,mwigulu na ccm kwa ujumla subiri muda wenyewe utaongea na hapo ndipo utakapoamini kuwa mawazo yako yalikuwa hasi.
 
Back
Top Bottom