Mbunge Lijualikali ahojiwa na TAKUKURU. Adai wabunge wa CHADEMA wamejipanga kudanganya lakini hawatafanikiwa!

Mbunge Lijualikali ahojiwa na TAKUKURU. Adai wabunge wa CHADEMA wamejipanga kudanganya lakini hawatafanikiwa!

Nimemsitua moderator asije kuonekana analipwa na polepole , hata ule wangu ulihusu wanahabari kukanyagana
Sugu alikuwa anawakimbia wasimuulize maswali.

Lijualikali na Silinde ndio walikubali kuhojiwa kila mmoja kwa wakati wake!
 
Wachaga kila kwenye upigaji wapo.

Na Mbowe akipona jeraha la kuanguka kwenye ulevi ataitwa Takukuru??
Labda ndo maana alijitegua. Kuteguka mguu sio kuumwa kichwa. Mguu mmoja mzima, achukuwe magongo awe anarukaruka. Akimaliza mapumziko ya operation aende tu TAKUKURU akajieleze yaishe.
 
Mbunge wa Kilombero mh Lijualikali alikuwa ni miongoni mwa wabunge wa Chadema waliohojiwa na Takukuru kuhusiana na matumizi ya fedha za chama.

Baada ya kuhojiwa mh Lijualikali aliongea na waandishi wa habari na kuwaambia mahojiano yake na Takukuru yamefanyika vizuri.

Zaidi akasema ana taarifa kuwa wabunge wa Chadema wamejipanga ili kutoa taarifa za uwongo na kumnusuru Mbowe.

Lijualikali ameapa kuwa wabunge hao hawatafanikiwa katika njama walizopanga.

Source Eatv habari

Maendeleo hayana vyama!
Walichekelea sana kila CCM ilipowatumbua watu wake.
 
Kwanza asante kuwa mdau wa Jicho Letu Ndani ya Habari, na asante kuangalia kipindi. Kwavile uliangalia kipindi, jee ulisikia nikishauri Twitter ifungwe?. Kama uliangalia kipindi, ulisikia nilichosema, sasa umewezaje kusema haya?!,

Wale ambao hawakuona kipindi wakiambiwa Pasco amesema Twitter ifungwe, rukhsa kuamini lakini hata wewe uliotazama na kusikia?!.

P

Yeah, Mimi Ni mdau mkubwa wa hicho kipindi cha jicho letu ndani ya habari, tena sio kwa hizi promo zako ulioanza juzi humu jukwaani, bali ni kabla hata ya awamu hii ya tano kuingia madarakani. Nashukuru kwa siku za karibuni kwa ushawishi wako, umeongeza hamasa na watazamaji toka jf, kwa hili nakupongeza.

Paskali ulichozungumza kwenye kipindi kile kuhusu twitter nilikisikia, sitaki kujiweka kwenye mitazamo ya wengi walisikia nini, lakini mtiririko wako ilikuwa ni kuwa ndani ya twitter kuna michango inakukwaza, na inakukwaza sio kwakuwa ni wakosaji sana, bali kuna mtu au watu kadhaa wainaikosoa serikali bila staha au vyovyote utakavyoiweka ww.

Ni wazi ulikuwa negative kwa mwenendo wa michango ya watu kadhaa wa twitter dhidi vya serikali, na ulifikia hitimisho la twitter kuchukuliwa hatua, kwa ww kujiweka kwenye kundi la huu uzalendo academia, for the reason best known to you. Unaweza kutumia utetezi wowote uutakao maana ni haki yako, lakini hivyo ndio nilivyokuelewa na sina shaka na hilo.
 
Tunatofautiana kutazama mambo.

Jinsi nilivyomuelewa Pascal Mayalla ni kwamba kuna haja ya viongozi kujibu kile kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii. Kama wataendelea kukalia kimya yanayozungumzwa kwenye mitandao wanaondoa shauku ya jamii kutaka kujua ukweli. Na ndipo linapokuja suala la wanajamii kuhamasishana kutoitumia mitandao hiyo kwasababu ya kukosekana kwa ukweli.

Zinazotolewa mitandaoni ni tuhuma lakini kuna mtu wa kujibu anatakiwa apatikane. Naona kataja baadhi ya maofisa ambao kama waandishi wa habari wangependa kukutana nao.

Kwa mtazamo wangu sijaona ubaya wa Mayalla.

Sina tatizo na mtazamo wa Paskali kwenye eneo hili uliloliweka hapa, ila nilichomwambia Paskali kwenye mtazamo wake kuhusu twitter, sina shaka na hilo.
 
Tayari kwa akili ya haraka Lijuakali ashaharibu planing yao kuropokaropoka. Kama busara itstumika Takukuru wanapaswa wsjue kuwa hii Ni chuki iliyopandikizwa na waiofika Bei kuwanunua kina Lijuakali na kina Silinde
 
Kauli za kikabila kama hii,ni hatari sana.
Unajua kuna siku hao wachaga wanaweza kupata nafasi ya kuongoza kupitia ccm na wakaamua kutawala miliele.
Maana kwa hali ilivyo mnajitahidi kuonesha kuwa hawapendwi(sijui na nani?)Na mtu akishajua hayo ni kweli,anaweza kutumia nguvu zake kujihakikishia anatawala milele.

Pia hizi chuki za ukabila,zinaeweza kufanya hata kabila lolote wakiingia madarakani,kujitahidi kujimilikisha madaraka milele kwa kuhofia kulipiziwa kisasi.

Naamini siku wachaga wakiingia madarakani hata kupitia ccm au hata nccr ya mbatia,watalipiza kisasi.Mimi si mchaga ila sifurahishwi na hizi kampeni za vijana wa Lumumba kuhamasisha chuki za ukabila na udini.Kumbuka mbegu hii mmeshaipanda tayari na mnaendelea kuimwagilia maji.
Chuki dhidi ya wachaga inakua kwa kasi sana.Kama kweli ni wapigaji waende jela tu
 
Dr Slaa, Zito, Kitila hawa wote walikua vigogo ndani ya chadema lakini wameondoka bila kulalamikia ufujaji pesa pale cdm,......

Hawa vijana walioondoka awamu hii ya Magufuli sijui wamejifunza wapi kutukana waliowatoa jalalani.

Lijualikali simfahamu, lakn Silinde ameni-disappoint sana jamani, nilikua namwona kama very matured!
Kweli kabisa Slaa, Zito, Kitila waliondoka bila malalamiko ya ufujaji. Hawa wanaolalamika ufujaji huu umefanyika kwenye fedha za michango walizokatwa mishahara tangu 2016 Hadi Sasa zipatazo 8.9 billion ambazo hazieleweki matumizi yake.
Kumbuka kipindi hiki Dr. Slaa, Zito Kitila hawakuwepo chadema hivyo hawawezi kulalamika Jambo Hilo. wanaolalamika ni hao waliokatwa hiyo mishahara yao.
Wakuchaguliwa tsh 520000
Viti maalumu. tsh 1560000 kila mwezi toka 2016

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani hii ndo imethibitisha kuwa hao takukuru ni mpango mkakati wa kusaidia jamaa wale walio hoi.
Ingekuwa ni nchi ya watu makini hii kima lijualikali ingekamatwa iisaidie polisi kuhusu kauli yake.
Kwamba analazimisha wingine wawe na mawazo yake?
Why?
Afrika tuna safari ndefu kufikia ustaarabu.
Ustaarabu wa kula kula pesa za watu na kufisadi?Kwa kweli Arawa hata pia la taka likijaa litatulia na hapo taka zikianza mwaka nje ni lazima zitanuka na hao Paka wa vichochoroni na M'mbwa kuko watazichakura na kuzisambaza."IMEFIKA WAKATI MUAFAKA".Mnakula hadi mnavimbiwa na kujambia midomoni.
Hivyo kumtoa mtu chini na kumfikisha mahali pa juu ni CV ya kumnyanyasa na kumfisadi?(Time will tell !!!)
 
Mbunge wa Kilombero mh Lijualikali alikuwa ni miongoni mwa wabunge wa Chadema waliohojiwa na Takukuru kuhusiana na matumizi ya fedha za chama.

Baada ya kuhojiwa mh Lijualikali aliongea na waandishi wa habari na kuwaambia mahojiano yake na Takukuru yamefanyika vizuri.

Zaidi akasema ana taarifa kuwa wabunge wa Chadema wamejipanga ili kutoa taarifa za uwongo na kumnusuru Mbowe.

Lijualikali ameapa kuwa wabunge hao hawatafanikiwa katika njama walizopanga.

Source Eatv habari

Maendeleo hayana vyama!
Hapo wanamkagua CAG na wala sio chadema jambo ambalo ni hatari Kwa utendaji Kazi WA vyombo vyetu.
 
We jamaa unachekesha sana! yaani mtu aibe hela za umma halafu asisemwe eti kisa wewe utakua disappointed!! hell no!! lazima Takukuru wafanye kazi yao kwa uhuru na DJ awajibishwe.

CAG Musa Asad, trilion 1.5 zimetumika,

lakini maelezo na viambatanisho havitoshi.

Wapi TAKUKURU?
 
Yaani hii ndo imethibitisha kuwa hao takukuru ni mpango mkakati wa kusaidia jamaa wale walio hoi. Ingekuwa ni nchi ya watu makini hii kima lijualikali ingekamatwa iisaidie polisi kuhusu kauli yake. Kwamba analazimisha wingine wawe na mawazo yake?

Why? Afrika tuna safari ndefu kufikia ustaarabu.
Akamatwe kwa kauli yake! Nchi gani hiyo unayoita makini inayofanya hivyo! Na anashtakiwa kwa kosa gani ? Mbona kama na wewe umo kwenye kisima hicho hicho cha kulazimisha mawazo yako!
 
Back
Top Bottom