Nchi hii inahitaji wazalendo wa kweli wenye ujasiri wa kuacha kazi na nyadhifa zao serikalini kupinga mateso na maonevu yanayofanywa na watawala dhidi ya wananchi wanyonge wasio na mtetezi.
Tulimuona wote Lipumba akijitokeza mbele ya vyombo vya habari kutoa wito kwa Lowassa aje UKAWA. Siku chache mbele Lipumba yuleyule akajitoa! Swali la kujiuliza, Lipumba na uzoefu wake wote nani alimlazimisha kutoa wito ule?!
Wananchi hawawahitaji wanasiasa wa kwenye vyama vya siasa visivyo hata madarakani wawachanganye kwa upuuzi wa aina hiyo. Wazalendo walio ndani ya serikali wajipambanue wazi bila unafiki waonekane, siyo hizi jitihada zisizo na tija kwa taifa zinazofanywa kwa visingizio vya kupinga mambo ambayo hayana faida yoyote kwa taifa.