Kati ya vitu ambavyo havihitaji akili ni ngono au kujamihiana. Kwa sababu ni tendo lisilohitaji akili, upeo, werevu au hekima, ndiyo maana mbwa hujamihiana, fisi hujamihiana, nzi hujamihiana, mijusi hujamihiana, hata minyoo na konokono hujamihiana.
Kwa binadamu, watu wengi wajingawajinga, muda mwingi hujadili na kufikiria ngono au mambo yanayohusiana na ngono.
Hata Bungeni, ukifuatilia, wale wabunge ambao hawana uelewa mkubwa na hawana uwezo wa kujenga hoja kwenye mambo makubwa ya msingi, mara nyingi wakijitutumua kutaka kuuliza swali au kuchangia, wataongelea masuala ya ngono, voungo vinavyohusiana na ngono au mambo yanayohusiana na ngono.
Kuna mbunge mmoja wakati fulani aliwahi kukomalia kuwa bunge lijadili wanaume wenye mkono wa sweta, na ikiwezekana wabunge wanaume wachunguzwe kwa sababu ana uhakika wengine wana mikono ya sweta. Ukifuatilia upeo wa huyo mbunge, unagundua ni zero brain. Cha ajabu eti ni kiongozi pia wa mkoa wa CCM. Ukifuatilia utagundua jimboni kwake kuna matatizo lukuki, watu wake hawana hata chakula, hawana hospitali, hawana shule, wana vipato duni, lakini yeye, kwa ujinga tu, amebakia na hadithi za mikono ya sweta alizookoteza mitaani. Ukimwuliza, mikono hiyo ya sweta inachangia vipi wananchi wake kukosa maendeleo, hana hata jibu.
Mwingine aliwahi kutamka kuwa kama wanawake watagundua waume zao wanachelewa kurudi majumbani, wawape adhabu ya kuwanyima unyumba. Halafu naye huyo, ni kiongozi wa CCM wa mkoa.
Mwingine leo anasema eti kila.mbunge kabla ya kuingia bungeni apimwe kama amewahi kulawitiwa, yaani maana yake na yeye anataka kupimwa. Na kumjua anayelawitiwa, ni lazima daktari aingize mkono kwenye njia ya haja kubwa. Kwa hiyo, inamaanisha huyo mbunge anataka yeye aingizwe mkono, na ili asiwe pekee yake anataka na wabumge wengine wote wafanyiwe hivyo. Huenda kwa akili yake ndogo, anaona likikubaliwa hilo, wale wote wenye akili timamu hawatakuwa tayari kudhalilishwa kwa mtindo huo kwa sababu ya ubunge, hivyo yeye ataendelea kuwa mbunge pamoja na wenzake wengine waliokosa akili.