Mbunge Mchafu: Wanaume Tanzania wanajadili zaidi Simba na Yanga kuliko afya zao

Mambo Ni mengi muda mchache ye Hana stress za posho sisi wengine vijiweni kwetu tunapopatia posho stori mezani ndo Kama hizo Simba na yanga Sasa ukiamua kubunda unakaa kwa kutulia na ukiamua kujilipua ruksa unafeli wapi Sasa mzee baba.
Poa
 
Nadhani angeanza kujijadili mwenyewe kwanini yeye ni mchafu
 
Wabunge wengine, basi tu brain zao zimeburn. Simba na Yanga kwa jicho la kawaida anaona Kama timu za kawaida. Simba na Yanga ni hisia za wanaume walio wengi. Ni afya ya akili mahali penye msongo. Mara ngapi amesikia watu wakifa eti sababu CCM imekosa ushindi Jimbo fulani? Lakini watu hufa kwa mshituko pale, Simba au yanga inapoleta matokeo yasiyotarajiwa. Aachane na sisi aendelee na kula posho bila kuwaza sana
 
Yeye mwenyewe majuzi kashindwa kujiandikisha kumuuliza maswali waziri mkuu wakati hapa nchini changamoto kibao...
 
Hajui kitu hobby.

Hisia za furaha zinaboresha afya.
Mkuu hobby ndo ujadili siku nzima?
andalia maana ya hobby-a pursuit outside one's regular occupation engaged in especially for relaxation.
 
"Wanaume wa Tanzania wanatumia muda mwingi kujadili Usimba na Uyanga, hawapimi virusi vya Ukimwi na hawataki kupima, hivi ingetumika muda huo kuzungumza masuala ya kupima afya zao si tungeshinda," amehoji Mchafu.
Moja ya njia ya kupambana na UKIMWI ni ninyi wenyewe wabunge kuacha uchafu na mnyimane kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…