johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Mbunge wa Singida Mashariki mh Miraji Mtaturu amesema Tundu Lisu amerejea alikokuwa kimya kimya Baada ya kuona Wana wa Ikungi wameshaachana na mambo ya Upinzani
Mtaturu amesema hata Mbowe alishangaa kukuta Wapinzani kiduchu Ikungi hali iliyofanya amuhiji Tundu Lisu " Ulisema Ikungi kuna Wapinzani Ndio hawa kiduchu?!!
Source Jambo tv
===
"Mwaka wa 2012, CHADEMA walipokea visima 100 kutoka kwa Mzee Sabodo ili kusaidia wananchi katika majimbo yao. Miongoni mwao, Mbunge wa Ikungi alipewa visima 10. Lakini je, kisima chochote kiliweza kuchimbwa? Kama haukuonesha uaminifu katika visima 10 ulivyopewa, tutakuaminije kuhusu kupewa nchi yetu?" - Miraji Mtaturu (Mb)
"Jamaa huyo aliyetoka nje ya nchi alipokelewa kwa shangwe, lakini alipofika Ikungi alikutana na kikundi kidogo cha watu hadi mwenyekiti wake alimuuliza, 'Je, huu ndio upinzani unaosemwa Ikungi?' Lakini mwishowe, aliondoka kimya kimya na kurudi alipotoka." - Miraji Mtaturu, Mbunge wa Singida Mashariki
"Kuna ndugu yetu mmoja ambaye alikuwa nje ya nchi. Aliporudi Singida na kukutana na viongozi wote, alitegemea kuona watu wanaendelea kusema uongo. Lakini watu wa Ikungi wamebadilika, wanatambua maendeleo yanayoletwa na Mama @SuluhuSamia." - Miraji Mtaturu, Mbunge wa Singida Mashariki
"Dk. Slaa anasema katika Katiba mpya kuwa wakuu wa wilaya wasiwe na nafasi tena. Anadhani kwamba kuwepo kwao ni tatizo, lakini tatizo hili halionekani na ni sawa na kuzungumzia jambo ambalo halipo. Mkuu wa Wilaya anasimamia shughuli za maendeleo, hivyo kuwepo kwake hakuna tatizo." - Miraji Mtaturu, Mbunge wa Singida Mashariki
"Kuna mzee ambaye aliwahi kuwa balozi wa Sweden. Alipofanya kazi yake ya ubalozi, aliipokea kwa mikono miwili na kusema wazi kuwa CCM ndio chama pekee kinachoweza kuendeleza nchi hii. Lakini baada ya kuondoka kwa ubalozi na njaa kumkaba, alianza kuishambulia CCM." - Miraji Mtaturu, Mbunge wa Singida Mashariki.