Mbunge mmoja anatosha kuwakilisha mkoa mzima

Mbunge mmoja anatosha kuwakilisha mkoa mzima

Leverage

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2021
Posts
2,125
Reaction score
3,169
Nami natia neno kwenye kauli ya spika Ndugai. Kama mwalimu mmoja anaweza kufundisha masomo matano basi mbunge mmoja pia anatosha kuwakilisha mkoa mzima.

Hakuna haja ya kuwa na wabunge 400 kasoro. Wakati huku chini kuna madiwani na wakurugenzi wa halmashauriri hawa ndio wanaojua changamoto za maeneo yao vizuri kuliko wabunge.

Kila mkoa utoe mbunge mmoja atakaepata taarifa zote kutoka kwa madiwani na wakurugenzi. Hivyo basi nchi nzima tuwe na wabunge 36 tu ili tubane matumizi.

Cc: spika
Cc: waziri mkuu
Cc: rais
 
Nami natia neno kwenye kauli ya spika Ndugai. Kama mwalimu mmoja anaweza kufundisha masomo matano basi mbunge mmoja pia anatosha kuwakilisha mkoa mzima...
Sio mkoa tu hata kanda nzima!!awe mmoja tu!!kanda ya ziwa, magharibi, kati, nyanda za juu kusini, pwani kwani wana kazi gani??sasa hakuna cha kutunga sheria, kupanga bajeti, kazi zote hizo sasa ni mtu mmoja tu?

Miradi iliyotengewa pesa na bunge, haipewi pesa, ila miradi inayompendeza MEKO, tena hata kwenye bajeti haipo ndio anaagiza ipelekewe pesa!!kuna wabunge hapo??
 
Sio mkoa tu hata kanda nzima!!awe mmoja tu!!kanda ya ziwa, magharibi, kati, nyanda za juu kusini, pwani kwani wana kazi gani??sasa hakuna cha kutunga sheria, kupanga bajeti, kazi zote hizo sasa ni mtu mmoja tu,?miradi iliyotengewa pesa na bunge, haipewi pesa, ila miradi inayompendeza MEKO, tena hata kwenye bajeti haipo ndio anaagiza ipelekewe pesa!!kuna wabunge hapo??
Eti nchi ina wabunge 400+ !
Kazi yao ni nini hasa?
Kupeana ulaji tu
 
Tupo gari moja, wawili kila mkoa kwa jenda.

Mawaziri wasiwe wanasiasa wateuliwe kwa vigeze ikiwemo ujuzi na weledi tasinia husika.Sijui huu mfumo wa ajabu tulirithi kwq nani!?
RC cheo futilia mbali na kufumua na kuunganisha vitengo na maamlaka.

Wachumi mpeni hesabu mkuu ataokoa kiasi gani.
 
Nami natia neno kwenye kauli ya spika Ndugai. Kama mwalimu mmoja anaweza kufundisha masomo matano basi mbunge mmoja pia anatosha kuwakilisha mkoa mzima...

Unamaanisha jimbo na magavana
 
DSM pekee ina wabunge 10. Wote hao wanaenda wanaenda kusemea kero za zahanati na madarasa.
Milioni 11*10*60 kwa miaka 5.
Hiyo hela ingetosha kumaliza tatizo la zahanati na madarasa mkoa mzima
 
Back
Top Bottom