Mbunge mmoja anatosha kuwakilisha mkoa mzima

Mbunge mmoja anatosha kuwakilisha mkoa mzima

Sijasema habari ya kanda hapa ila wananchi hatuoni faida ya wabunge 400+ .
Kipi hasa wanachokifanya hasa watu 400+ huko bungeni?

Kabisa, hata mimi sioni sababu ya kuwa na wabunge wengi hivyo hasa wa viti maalum, na hata hilo bunge ni rubber stamp tu. Kwangu bunge ni sehemu ya kulia hela za wananchi bure kisheria.
 
Kwa awamu hii hata wangeufuta tu huo utaratibu wa kuwa na Wabunge sawa tu. Kwangu mimi naona hawana tija yoyote ile, zaidi ya kula mishahara na posho za bure.

Mtu anapewa dk 10 za kuchangia, anatumia nusu ya hizo dk kusifia na kumpongeza Rais wake, chama chake na familia yake! Hakuna tena ule utaratibu wa kuisimamia na kuiwajibisha serikali.

Spika nae akiongea, unakutana ni ugoro tu
 
Nami natia neno kwenye kauli ya spika Ndugai. Kama mwalimu mmoja anaweza kufundisha masomo matano basi mbunge mmoja pia anatosha kuwakilisha mkoa mzima. Hakuna haja ya kuwa na wabunge 400 kasoro. Wakati huku chini kuna madiwani na wakurugenzi wa halmashauriri hawa ndio wanaojua changamoto za maeneo yao vizuri kuliko wabunge. Kila mkoa utoe mbunge mmoja atakaepata taarifa zote kutoka kwa madiwani na wakurugenzi. Hivyo basi nchi nzima tuwe na wabunge 36 tu ili tubane matumizi.
Cc: spika
Cc: waziri mkuu
Cc: rais
Wazo zuri Sana, hebu tutafakari hili, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na makatibu wao, madiwani, maafisa watendaji wote Hawa wanafanya kazi kwaajili ya wananchi lakini mbunge pia tunahitaji. Labda ni kwaajili ya kazi ya mhimili wao Ila ni swala la muda tu.
 
Kwa awamu hii hata wangeufuta tu huo utaratibu wa kuwa na Wabunge sawa tu. Kwangu mimi naona hawana tija yoyote ile, zaidi ya kula mishahara na posho za bure.

Mtu anapewa dk 10 za kuchangia, anatumia nusu ya hizo dk kusifia na kumpongeza Rais wake, chama chake na familia yake! Hakuna tena ule utaratibu wa kuisimamia na kuiwajibisha serikali.

Spika nae akiongea, unakutana ni ugoro tu
Ukiwa huna cha kuongea lazima ushukuru kwa dakika 8, dakika mbili zilizobaki unaunga mkono hoja unasubiri mwisho wa mwezi milioni 11.
 
Wazo zuri Sana, hebu tutafakari hili, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na makatibu wao, madiwani, maafisa watendaji wote Hawa wanafanya kazi kwaajili ya wananchi lakini mbunge pia tunahitaji. Labda ni kwaajili ya kazi ya mhimili wao Ila ni swala la muda tu.
Kweli tunahitaji wabunge ila sio wengi kiasi hicho
 
Ukiwa huna cha kuongea lazima ushukuru kwa dakika 8, dakika mbili zilizobaki unaunga mkono hoja unasubiri mwisho wa mwezi milioni 11.
Halafu Spika wao anawataka Walimu waongeze masomo ya kufundisha walau yafikie matatu au matano!! Hawa watu naona kuna kitu wanakitafuta.

Wamesahau mwanadamu ni mnyama tu aliye staarabika. Kipimo chake cha uvumilivu na upole kikifikia ukomo, hugeuka na kuwa mnyama mkali sana.
 
Kuwe na magavana tuachane na ubunge....Aajiriwe kabisa ,nafasi itangazwe apigwe interview na bodi ya kibabe.....Sio wabunge kama kina Kibajji au msukuma au babu tale.
Tuwe na Bunge lenye vyumba viwili, cha Wawakilishi na cha Senate lililochaguliwa na wananchi na wingi wao utategemea wingi wa majimbo na mikoa, Magavana watakuwa wasomi badala ya Wakuu wa Mikoa na wingi wao utategemea wingi wa Mikoa iliyokubalika, siyo Wilaya inakuwa Mikoa miwili na Tarafa Wilaya. Bunge dhaifu la Ndugai dhaifu limetuonyesha umuhimu wa kuwa na Senate kuthibiti Bunge lisiwe Idara ya Ikulu ya usanii wa kupiga meza miaka 5 yote. Tuweke mfano wa uzuri wa mfumo huu: Mama Pelosi Spika wa Bunge la chini la Marekani alivyofanikiwa kuimpeach mara mbili Rais ambaye Chama chake kilikuwa kinaongoza Senate, sasa yanaandaliwa mashitaka ya kumfukuza asigombee tena uongozi ingawa hayupo madarakani. Huu ndo Utawala Bora Wapinzani na wananchi wenye akili wamekuwa wanalilia maana kwenye mfumo huu Mswada ukipita Bunge la chini lazima pia upite Senate ndo uende kwa Rais kupitishwa kuwa Sheria. Kwetu kiongizi akiboronga anaongezewa muda wa kuboronga zaidi!
 
...."Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru asali wa moyo wangu, laazizi mwanasheria nguli, baba watoto wangu, nyonga mkalia ini, najua wengi mlikuwa hamumjui Honorable Dk. Gwajima"
😁😁😁😁😁😁😁😁😁 kmmmk mbunge wa aina hii anakabidhiwa jimbo na 12M yake iko pale pale mwisho wa mwezi...Only in Tanzania tu!!!
 
Nami natia neno kwenye kauli ya spika Ndugai. Kama mwalimu mmoja anaweza kufundisha masomo matano basi mbunge mmoja pia anatosha kuwakilisha mkoa mzima.

Hakuna haja ya kuwa na wabunge 400 kasoro. Wakati huku chini kuna madiwani na wakurugenzi wa halmashauriri hawa ndio wanaojua changamoto za maeneo yao vizuri kuliko wabunge.

Kila mkoa utoe mbunge mmoja atakaepata taarifa zote kutoka kwa madiwani na wakurugenzi. Hivyo basi nchi nzima tuwe na wabunge 36 tu ili tubane matumizi.

Cc: spika
Cc: waziri mkuu
Cc: rais

Mimi naona wanahitajika ili kujua changamoto za kila eneo.

Muhimu Mishahara ikatwe zaidi ya nusu. Ili wote wanaoenda pale mjengoni wawe na nia ya dhati, ukweli wa kuwakilisha wananchi wao.

Sio maslahi binafsi. Hawatabiga kula za ndio kwa huu muswaada.
 
...."Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru asali wa moyo wangu, laazizi mwanasheria nguli, baba watoto wangu, nyonga mkalia ini, najua wengi mlikuwa hamumjui Honorable Dk. Gwajima"
😁😁😁😁😁😁😁😁😁 kmmmk mbunge wa aina hii anakabidhiwa jimbo na 12M yake iko pale pale mwisho wa mwezi...Only in Tanzania tu!!!
Huyu mama kila nikimuona vimbwanga vya Ebitoke vinanijia.
 
Babu Tale....... Morogoro

Jah people...... Njombe

Musukuma...... Geita

Kibajaji.......... Dodoma

Kinanasi...... Mbeya

Tabasamu..... Mwanza

Unaweza kuongezea waheshimiwa Finance and Building wa mikoa mingine!
Chakubanga vp?
 
DSM pekee ina wabunge 10. Wote hao wanaenda wanaenda kusemea kero za zahanati na madarasa.
Milioni 11*10*60 kwa miaka 5.
Hiyo hela ingetosha kumaliza tatizo la zahanati na madarasa mkoa mzima
bilion. 6.6 kwa miaka 5, hiyo pesa ingetosha kabisa
 
Babu Tale....... Morogoro

Jah people...... Njombe

Musukuma...... Geita

Kibajaji.......... Dodoma

Kinanasi...... Mbeya

Tabasamu..... Mwanza

Unaweza kuongezea waheshimiwa Finance and Building wa mikoa mingine!
Dar nireteeni Gwajimaaaah!
Imeishaaaa hiyooooo!😅😂

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Au ikishindikana kupunguza idadi ya wabunge basi mshahara upunguzwe wapewe basic 2M bila posho mi hata sioni kazi yao huko.
 
Back
Top Bottom