Mbunge mmoja anatosha kuwakilisha mkoa mzima

bilion. 6.6 kwa miaka 5, hiyo pesa ingetosha kabisa
Wanafunzi King'ong'o walikuwa wanakaa chini. Hii sawa na kufanya biashara ya karanga kwa kukaanga kwa jiko LA umeme. Unatumia umeme wa 7000 kwa mauzo ya 3500
 
Ni hoja nzuri sana hii wadau ni vizuri tukaidadavua vizuri. Hawa watu 400 kasoro ni wengi mno kwa taifa changa kama letu. Walau tungekuwa na mbunge mmoja kila wilaya ingekuwa economical na tena tuweke vigezo vya kikatiba kuwa mbunge ili akawe msimamizi kweli wa serikali awe na elimu ya kutosha na uzoefu katika utendaji wa serikali. Rais Magufuli ameweza kuwakaba hadi wasomi wanaojulikana kwa sababu aliijua serikali vilivyo na mianya hawa watu wa serikalini walikuwa wanaiibia serikali. Hatuwezi kugharamia Wabunge kama Jah People ambaye sijawahi kusikia akichangia lolote ila tu kumpamba Mheshimiwa Rais na kuomba aongezewe vipindi vya Urais. Ili kuenenda na dunia ya sasa tunahitaji Wabunge wajuvi na weledi kwenye mambo anuai ya kiuongozi, usimamizi, udhibiti, sheria, sayansi na uchumi. Si lazima ajue yote kwa undani lakini awe ni mtu anayeweza kuyajua basics zaje na kuweza kujisomea kuingia deep zaidi inapohitajika.
 
Wanafunzi King'ong'o walikuwa wanakaa chini. Hii sawa na kufanya biashara ya karanga kwa kukaanga kwa jiko LA umeme. Unatumia umeme wa 7000 kwa mauzo ya 3500
kwa hiyo bl. 6.6 unaweza ukanunua madawati yenye thamani ya 100k ukanunua madawati 66,000.

hiyo 66,000 uigawe kwenye shule yenye wanafunzi 400 ina maana shule 165 watapata hayo madawati.

kwa mantiki hiyo mkoa wa dar es salaam mzima kero ya madawati itakuwa imeisha
 
Kuwe na magavana tuachane na ubunge....Aajiriwe kabisa ,nafasi itangazwe apigwe interview na bodi ya kibabe.....Sio wabunge kama kina Kibajji au msukuma au babu tale.
Msukuma Usimuweke kundi moja na watu wa ajabu ajabu.
 
Ukiwa huna cha kuongea lazima ushukuru kwa dakika 8, dakika mbili zilizobaki unaunga mkono hoja unasubiri mwisho wa mwezi milioni 11.
Hivi mil.11 ni sawa na madawati mangapi? Tunaweza kuwa tunajadili tatizo la madawati kumbe suluhu ni Wabunge.
 
Sasa hivi ubunge imekuwa sehemu ya ulaji bila ya kuangalia weledi wa mtu.
Inasikitisha sana
 
Hivi mil.11 ni sawa na madawati mangapi? Tunaweza kuwa tunajadili tatizo la madawati kumbe suluhu ni Wabunge.
Dawati na kiti chake ni 70,000/= kwa bei ya supplier Ila ukiingia front mwenyewe hadi 60,000/=
 
Huu uzi wangu bora wa mwaka. Ingekuwa twitter ninge retweet. Bonge moja la point.
 
Nakwambiaje mkuu ni aibu kulipa mishahara wabunge 10 wa DSM wakati wanafunzi wanakaa chini. Kama taifa hatuna vipaombele
 
DSM pekee ina wabunge 10. Wote hao wanaenda wanaenda kusemea kero za zahanati na madarasa.
Milioni 11*10*60 kwa miaka 5.
Hiyo hela ingetosha kumaliza tatizo la zahanati na madarasa mkoa mzima
Hapo bado seating allowance na marupurupu kibao, mafao after 5yrs
 
Mi naenda mbali zaidi; hivi nani anaweza kunambia umuhimu wa bunge kwasasa? Mfano likifutwa kabisa, nini kitakacho athiri Utanzania wetu au hata maendeleo yetu? Binafsi naona kama linaongeza gharama za tu za uendeshaji wa nchi, lingefutwa kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…