Mbunge Mohamed Issa: Wanaotoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar wawe na Passport
hili jambo tangu nazaliwa nalitamani, tumechoshwa na watanganyika wanaokwenda kuzurura tu kule bila ya kazi maalumu, kule Zaznibar badala ya kunukia marashi ya karafuu sasa kunanuka vundo

Waleteee waleteeee !!!!
 
Kama anadai wakutoka bara kwenda znz wawe na passport hiyo ni sawa na wa znz wanaoishi bara kwanza warudi znz Kisha wakitaka kurudi bara waombe kama wageni wengine. Kwa ujumla muungano huu ni wa mashaka bora ufutwe
 
Ila sisi ndio tunazingua
Unatoka kisiwani na TV moja unaona jamaa anakusimamisha anasema lipia ushuru bila aibu
TV moja?
Kama sio uhasama ni nini?
Kuingia na pasi hapana ila tuishi kama wamoja
Kuna kitu ila serikali iingilie kati suala la bandarini watu wanalipishwa mpaka mihogo
 
Zanzibar inatumika kama uchochoro wa kukwepa kodi. Hizo TV unazosema zikiingia kwa mamia zinaua soko la TV za Tanganyika, kukosesha mapato na tunalipa kodi zaid. Fikiri vijana 50 kila mmoja analeta TV kila siku, kwa siku 5 ni sawa na 250. Huyu mfanyabishara wa Tanganyika aliyeagiza anauza wapi na kwa bei gani!

Kuingiza ndizi Zanzibar ni tatizo wana sheria zao, kwanini iwe nongwa kulipisha bidhaa kodi.

Hili la Passport naunga mkono, waweke hata kesho lakini nao waje na passport! period.
Halimuathiri Mtanganyika yoyote maana unaowano katika meli ni wao wanarudi kwao!
Yote sawa ila la TV sidhani kama mtu ana zawadi yake na mzigo wake tu kama sanduku moja unaweza kumuuliza kodi
Hao vijana 50 unaosema haiwezekani kila siku TV zinaingia individuals never
Wafanyabiashara wanajulikana wanaingia na bidhaa zao
Bado kuna tatizo na changamoto kubwa bandarini, tukubali tukatae

Ukifikika border hiyo ndio utajua ni nchi 2 tofauti kabisa bali wanalazimisha tu
Wangeweka wazi kila kitu
Ila kama ni mapato huko wanalipa na huku wanalipa pia
Je wanalipa mara ngapi hapo? Naona kuna ya muungano na yasio ya muungano hapo
Lazima sheria ziwe wazi
 
Nasemaje...! Zanzibar asiachwe, hiyo ndoa akae akijua ni ya hadi dahari!

Na ikiwezekana, Zanzibar iachwe kuwa huru kwa siku tatu halafu itekwe na kulazimishwa kuwa nchi moja ambayo itakuwa na Rais mmoja tu

Hakuna tena sjui cha serikali ya wapi na wapi
Haitakiwi kuachwa,ishu hapa ni kuvunja muungano na kuifanya nchi moja bil ya kuwa na serikali mbili,kwani tunashindwa wapi? Tukiwa serious kabisa hata kesho tu tunatangaza kuondoa hichi kiraka cha Muungano na kutangaza kuwa ni nchi moja na wakileta fyoko fyoko ni kichapo
 
Hii hoja ikipita, kila Mtanzania kutokea bara atapaswa kuonwa kama mgeni kutokea mataifa mengine kila anapoingia Zanzibar.
Mara ya mwisho mimi kutembelea hicho kisiwa niliona wageni wa mataifa mengine wanaotokea bara kuingia Zanzibar ilikua inabidi wapitie kwanza uhamiaji kama ambao wanaingia nchi nyingine yaani, unahojiwa maswali yale yale uliyohojiwa pale ukiingia Tanzania, unapigiwa muhuri wa kuingia Zanzibar kama nchi nyingine na ukitoka pia unaagwa na muhuri.
Zamani haikua hivyo, ilikua kama wewe mgeni ila unatokea bara, ulikua unaingia kama ambaye umetokea Dar kwenda Morogoro.
===============

. Just two days before Tanzania celebrates 60 years of unification between Tanganyika and Zanzibar to form a United Republic, a parliamentarian hailing from the isles has ignited a debate that threatens the Union.
Konde Constituency Member of Parliament, Mohammed Said Issa, has sparked a debate on both sides of the Union by suggesting that the government reinstate the use of passports for mainland Tanzanians crossing to Zanzibar.
 
Back
Top Bottom