Mbunge wa Konde (ACT Wazalendo), Mohamed Said Issa ameitaka Serikali kurejesha upya utaratibu wa watu wote wanaoingia Zanzibar kuwa na hati ya kusafiria...
Imagine, mzanzibari anaongea haya bila kujua yafuatayo:
1. Yeye amevuka maji kuja kula perdiem bungeni, bila passport.
2. Wazanzibar wanamiliki ardhi na nyumba, mashamba n.k bara popote.
3. Wazanzibar wameajiriwa kwenye serikali kuu na hata kwenye private sector Bara.
4. Pato kubwa la wazanzibar wengi sana ni biashara wanazozifanya DSM au la, pesa wanazotumiwa na watoto wao wanaoishi DSM, Tanga na maeneo mengine ya bara. kuna wapemba hadi Arusha, hadi Mwanza popote nchini huwezi kukosa alau mpemba mmoja. ukienda Kigamboni, gongolamboto, tuseme maeneo mengi ya uswahilini DSM yamejaa maduka ya wapemba, wapika chips na mikahawa wazanzibar n.k.
halafu yeye leo hii anaona wabara wanaenda kule kuchukua ardhi, kuchukua kazi. hivi kuna wabara wanaendaga kutafuta ajira zanzibar kweli? nilikuwa sijui hili. pia, kwani samia anapokuja huku anakuwa na passport?