Kusema serikali moja ni kuwachokoza wanaokana Utanzania kutokea ule upande wa visiwani umeliwazia au umebandika tu " Serikali moja"? Hawa watu hawataki kuchokozwa wao ni Zanzibar tu, haya ya Muungano hawataki kuyasikia.
Wazo la Serikali moja nashindwa kuelewa wanaolitoa wanapata wapi uthubutu.
Nani atawapa au kuwabeba W'bar kama ilivyo sasa na bado hawaridhiki. Kila kitu kuna sehemu ya Zanzibar
Na Wazanzibar wasiotaka kusikia Tanzania wataishi vipi bila Uzanzibar. Hili wazo ni DOA (Dead on arri
-Mara wanajaribu kila kitu, mara njooni na Passport- wakibanwa sana wanasema hawakumaanisha hivyo.
Hili la Passport ni Tusi kubwa sana halafu likaongezewa na kuukana Utanzania ndani ya Bunge la Tanzania
-Mara wanakuja na kauli ya wao sio watanzania- na tuone Bunge/serikali itawafanya nini?
Tena wanajadili 90% ya mambo ya Tanganyika yasiyowahusu, ya Muungano kwa mujibu wa mkataba ni 11 na kwa mujibu wa Tume ya Warioba yangekuwa 7 tu. Wakiwa wanajadili au kula na kulala wanatukana Watannganyika.
Ni Watanganyika hao hao wanaolipa mishahara , posho na bili za umeme za wake zao huko Zanzibar.
Ni Watanganyika wanaolipa mfuko wa Jimbo la watu 3,338 sawa na jimbo la Serengeti, Ilala, Tanga, Tunduru, Ifakara, Katavi au Kibondo. Na huyo anayeukana Utanzania kasomea Tanganyika tena bure.
-wanajaribu kila mbinu - ili mradi tu Zanzibar ijichomoe humo kwenye Muungano.
Sio kwamba hawawezi la hasha! kuna mambo yanawazuia. Ukisikia wanataka mkataba ni kwa kuelewa kwamba gharama za ulinzi na usalama, mambo ya ndani , nje n.k. yatakuwa mzigo kwao. Wanatambua kwamba soko lao ni Tanganyika, si biashara bali ajira pia. Tanganyika inaajiri Wazanzibar wengi kuliko SMZ kwa upendeleo hata kuumiza watu wake.
-Mwisho wakishindwa, watafanya mengine ya hatari zaidi na bado hawatafanywa kitu.
Kama wanaweza kudai Rais wa nchi moja watumie passport kuingia kwao na wakiwa ndani ya Bunge la JMT wanaukana Utanzania kuna hatari gani imebaki? Hawa wanaweza kuona hatari wasijali kwasababu si Watanzania.
Kuna Mbunge anaitwa Ali Salehe, yeye alisema '' Ninafurahi nasikia bandari ya Bagamoyo imekwama''
Ifike mahali mamlaka itoe kauli, kwamba kama mtu ni kiongozi, yumo kwenye chombo cha kutunga sheria, halafu anakana kwamba hastari kuwemo humo ( Principel ya legal estoppel) maana yake ni kwamba hata hizo sheria zote alizoshiriki kutunga ni batili ab nitio. Haya ndio madhara makubwa zaidi ya kumyamazia huyi Mbunge.
Kauli ya kuukana Utanzania na kuomba passport imetolewa Bungeni
1. Spika wa Bunge yupo kakaa kimya
2. Waziri Mkuu yupo kakaa kimya
3. Makamu wa Rais yupo kakaa kimya
4. Raia wa SMZ yupo kakaa kimya
5. Rais wa JMT yupo kakaa kimya
6. Mstaafu Kikwete kimyaa! anasubiri aseme Mbowe. Tunaombwe la 'statesman'
Kimya kinawawezesha Wazanzibar kusema hoyo. Walianza kwenye mikutano sasa ndani ya Bunge
Ni kama vile viongozi hao wanakubaliana . Haikuanza na Passport, ilianza na katazo la ndizi, passport sasa wanaukana Utanzania. Hatudhani kwama wanahitaji Muungano!
Hatuwezi kutungiwa sheria na wanyarwanda wa visiwani maana ili uwe Mbunge, kigezo mojawapo ni Uraia, na yeye kakana na hata kwenye Hansard ipo, au landa waifute.
Haiwezi kufutwa bila kujadiliwa tena Bungeni, wakifanya hivyo watakuwa wamekiuka sheria zao wenyewe
Yaani Wazanzibar wanaukana Utanzania, tumebaki na nini?
Tena hawa Wazanzibar wanaiukana Utanzania ndio wanajadili mambo ya ''Tanzania'' hatuwahitaji ni wakati sasa wakijadili ya Muungano(kama wana japo wazo) waondoke watuache!
Ipo siko wanasheria watenda mahakamani na kuitumia hiyo kauli yake kubadilisha vifungu vyote vya sheria vilivyo pitishwa na huyu Mbunge na mahakama itakubali bila ajizi, na hili hawa viongozi wa Bunge hawalioni labda mpaka wavae miwani...
Natamani kama wanasheria wataliona hili