Mbunge Mstaafu na Mtu Maarufu anahitaji Mchango wa matibabu, wewe unadhani uta survive vipi?

Mbunge Mstaafu na Mtu Maarufu anahitaji Mchango wa matibabu, wewe unadhani uta survive vipi?

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Nimejiuliza hili swali sana si kwa nia mbaya. Kwa nia njema kabisa. Prof Jay. Joseph Haule amekuwa Mbunge kwa miaka 5 akilipwa mamimilioni ya pesa. Baada ya kumaliza kipindi chake amelipwa mamilioni mengine ya kiinuna mgongo.

Leo ameumwa na kulazwa kwa mwezi mmoja anadai achangiwe. Je yule mswahili ambaye anapata mshahara wa tsh 400,000 kwa mwezi ana mke na watoto. Hana malupulupu, hana mbele wala nyuma. akiumwa inakuaje?

Twende mbele na kurudi nyuma. Joseph Haule si mtu wa kuchangiwa pesa ya matibabu. ni kutaka kutumia umaarufu wake vibaya. sisi watanzania tufikie hatua tuwe makini na watu wenye kufikiri kwa kina. Huyu bwana alipokuwa Mbunge miaka 5 aliwahi fikiria nini kuhusiana na gharama za matibabu?

Kama wenzie sasa hivi hawajali maumivu wanayopata watanzania wa kipato cha chini pengine kwa kudhani hayawahusu. But ipo siku pia nao yanaweza kuwakuta ni vyema kujipanga kwa mambo ambayo ukiwa mbunge na usipokuwa mbunge yanaweza saidia taifa hili.

Tuchangini wenye mahitaji ya kweli kweli ndugu zanguni. Prof J ana weza hata uza moja ya nyumba zake au lake. Ila wewe mwenzangu ukiumwa hutoweza jitibia wala kuchangiwa na watu sababu hufahamiki na huna cha kuuza.
 
Umeongea ukweli mchungu ambao wengi hawapendi kuusikia, mtu aliyekuwa akilipwa 12M per month eti leo achangiwe matibabu, vipi walimu wanaolipwa laki 5 wakiumwa hawachangiwi?

Familia iache kujidhalilisha wakomae na matibabu ikishindikana basi Mungu kapanga ila sio kumchangia tajiri matibabu.
 
Hiki ni kiwanda cha uongo. Prof hahitaji michango bali michango ndo inakuhitaji Prof. Sio wakati wote tunamchangia mtu kwa sababu hana uwezo bali ni kuonyesha mshikamano wakati wa shida
Acha uongo, familia imeenda clouds na kuhitaji mochango na wamesema kea wiki inatumika mil 4 ni nyingi wanaomba washikwe mkono
 
Nimejiuliza hili swali sana si kwa nia mbaya. Kwa nia njema kabisa. Prof Jay. Joseph Haule amekuwa Mbunge kwa miaka 5 akilipwa mamimilioni ya pesa. Baada ya kumaliza kipindi chake amelipwa mamilioni mengine ya kiinuna mgongo. Leo ameumwa na kulazwa kwa mwezi mmoja anadai achangiwe. Je yule mswahili ambaye anapata mshahara wa tsh 400,000 kwa mwezi ana mke na watoto. Hana malupulupu, hana mbele wala nyuma. akiumwa inakuaje?

Twende mbele na kurudi nyuma. Joseph Haule si mtu wa kuchangiwa pesa ya matibabu. ni kutaka kutumia umaarufu wake vibaya. sisi watanzania tufikie hatua tuwe makini na watu wenye kufikiri kwa kina. Huyu bwana alipokuwa Mbunge miaka 5 aliwahi fikiria nini kuhusiana na gharama za matibabu? Kama wenzie sasa hivi hawajali maumivu wanayopata watanzania wa kipato cha chini pengine kwa kudhani hayawahusu. But ipo siku pia nao yanaweza kuwakuta ni vyema kujipanga kwa mambo ambayo ukiwa mbunge na usipokuwa mbunge yanaweza saidia taifa hili.

Tuchangini wenye mahitaji ya kweli kweli ndugu zanguni. Prof J ana weza hata uza moja ya nyumba zake au lake. Ila wewe mwenzangu ukiumwa hutoweza jitibia wala kuchangiwa na watu sababu hufahamiki na huna cha kuuza.
Kuna Kocha mmoja juzi uingereza Wamemchangia £60,000 kwa ajili ya cancer ya ubongo ya mke wake. Mashabiki wa Crystal palace wamechanga. Sio kwamba huyu Kocha hana mshahara mkubwa ila kuna magonjwa mkuu hata kama una Hela ni gharama kuyatibu.

Hizi Issue za Figo kupigwa tu Laser Hospitali Nzuri hapa Tanzania unaambiwa milioni 12, Hapo bado Hela nyengine za kitanda na mambo mengine madogo madogo, na Hapo uombe Mungu isirudie kama Unarudi Rudi hospitali na Ugonjwa unakupelekesha muda Mrefu ndo Hapo unaona mtu anatembeza Bakuli.
 
Hiki ni kiwanda cha uongo. Prof hahitaji michango bali michango ndo inakuhitaji Prof. Sio wakati wote tunamchangia mtu kwa sababu hana uwezo bali ni kuonyesha mshikamano wakati wa shida
Kwnini mshikamano uwe kwa watu kama hao ivi umesha wahi fika pale muhimbili kuna wangojwa wangapi ambao wametelekezwa pale hana ndugu wana teseka , au kule vujijini ndani mtu Ana umwa mwaka wa 5 huu hajui hatma yake Ana subiri kufa tu , naamini hata vitabu vya dini vina sisitiza tuwape wenye uhitaji wasio jiweza ili tupate thawabu .... any way kupanga ni kuchagua
 
Haumwi malaria au UTI au mafua ambapo matibabu yake angeliweza kuyahimili...

Anaumwa ugonjwa ambao hata ukiwa na "pesa kama alizonazo", itafika mahali utarudisha tu mpira kwa kipa...

All in all umaarufu unasaidia nyakati kama hizi...
 
Kwnini mshikamano uwe kwa watu kama hao ivi umesha wahi fika pale muhimbili kuna wangojwa wangapi ambao wametelekezwa pale hana ndugu wana teseka , au kule vujijini ndani mtu Ana umwa mwaka wa 5 huu hajui hatma yake Ana subiri kufa tu , naamini hata vitabu vya dini vina sisitiza tuwape wenye uhitaji wasio jiweza ili tupate thawabu .... any way kupanga ni kuchagua
kabisa, wengi wanapoteza maisha kwakua tu hana 20k ya matibabu, hao ndiyo wakusaidiwa kwa hali na mali na wapo wengi kweli, nenda MOI Muhimbili pale au vitengo vingine
 
Jambo la ugonjwa halitabiriki kama ilivyo kwa kifo. Yawezekana mzee wa mitulinga ana bima nzuri tu lakini kumbuka vigezo na masharti ya bima. Bima zingine zinataja kwamba kwa ugonjwa X kiwango cha juu tutalipa Tsh kadhaa na ziada ya hapo mteja utalipia mwenyewe. Kuna baadhi ya magonjwa bima zinaweka wazi kwamba hili hatulipii. Unaweza ukute malaria, typhoid na UTI wametenga 20M kwa mwaka lakini magonjwa mengine wameweka 3,00,000 zaidi ya hapo utalipia mwenyewe. Na kama figo zimedhoofika unadhani bima inanunua figo? Au kama moyo una tundu?

Tukienda kwenye kipato ndo hivyo labda kawekeza kwenye hotel ambayo inaingiza faida ya 100,000 kwa siku. Kwa magonjwa yasiyoambukizwa nakwambia hela hiyo haitoshi.

Hivyo tubakize maneno maana mifumo yetu ya kiuchumi inachechemea watu wanaishi kwenye nyumba na kuendesha magari huku wakibeba mikopo ya mamilioni kwenye taasisi za fedha mbalimbali.
 
Kuna kijana toka Tanga alivunjika mkono akaletwa Muhimbili ili kufanyiwa operation alitakiwa laki nne na nusu tu. Familia haikua na hiyo hela. Alisota pale Muhimbili kulala chini wodi inanuka vidonda vya majeruhi wa bodaboda hata maji huwezi kunywea mle ndani.
Baada ya kukaa zaidi ya mwezi Alaina liwalo na liwe naenda kutibiwa nyumbani na waganga wa kienyeji. Kweli alittoroka Muhimbili na sasa mkono umepona japo sio kivile. Aliumia kipindi Cha serikali ya wanyonge.
 
Nchi yetu bado ni masikini sana hatuwezi kuacha kuishi kwa kuchangiana. Hata hao mnaodhani wana pesa nyingi kimsingi ni za kawaida tu. Watu walioyapatia maisha ni wachache sana, ni familia fulani fulani tu. Wengi tunawaona wametoboa lakini nyuma yao kuna utitiri wa majukumu yanayotokana na familia ndugu jamaa na marafiki ambao bado ni masikini.

Ukiona nchi ambayo unahitaji kuwa na mipesa mingi ili upate huduma nzuri za kijamii jua hiyo nchi bado masikini wa kutupwa. Acha tuchangiane ndugu. Yeyote akiletwa mbele ya jamii na ikathibitika anahitaji msaada wanaoguswa acheni wachange.
 
Nimejiuliza hili swali sana si kwa nia mbaya. Kwa nia njema kabisa. Prof Jay. Joseph Haule amekuwa Mbunge kwa miaka 5 akilipwa mamimilioni ya pesa. Baada ya kumaliza kipindi chake amelipwa mamilioni mengine ya kiinuna mgongo.

Leo ameumwa na kulazwa kwa mwezi mmoja anadai achangiwe. Je yule mswahili ambaye anapata mshahara wa tsh 400,000 kwa mwezi ana mke na watoto. Hana malupulupu, hana mbele wala nyuma. akiumwa inakuaje?

Twende mbele na kurudi nyuma. Joseph Haule si mtu wa kuchangiwa pesa ya matibabu. ni kutaka kutumia umaarufu wake vibaya. sisi watanzania tufikie hatua tuwe makini na watu wenye kufikiri kwa kina. Huyu bwana alipokuwa Mbunge miaka 5 aliwahi fikiria nini kuhusiana na gharama za matibabu?

Kama wenzie sasa hivi hawajali maumivu wanayopata watanzania wa kipato cha chini pengine kwa kudhani hayawahusu. But ipo siku pia nao yanaweza kuwakuta ni vyema kujipanga kwa mambo ambayo ukiwa mbunge na usipokuwa mbunge yanaweza saidia taifa hili.

Tuchangini wenye mahitaji ya kweli kweli ndugu zanguni. Prof J ana weza hata uza moja ya nyumba zake au lake. Ila wewe mwenzangu ukiumwa hutoweza jitibia wala kuchangiwa na watu sababu hufahamiki na huna cha kuuza.
Ugonjwa ni mwanzo wa umasikini unajikuta umetumia zoteee mpaka unatamani mgonjwa atoke duniani
 
Back
Top Bottom