Mbunge Mstaafu na Mtu Maarufu anahitaji Mchango wa matibabu, wewe unadhani uta survive vipi?

Mbunge Mstaafu na Mtu Maarufu anahitaji Mchango wa matibabu, wewe unadhani uta survive vipi?

Nimejiuliza hili swali sana si kwa nia mbaya. Kwa nia njema kabisa. Prof Jay. Joseph Haule amekuwa Mbunge kwa miaka 5 akilipwa mamimilioni ya pesa. Baada ya kumaliza kipindi chake amelipwa mamilioni mengine ya kiinuna mgongo.

Leo ameumwa na kulazwa kwa mwezi mmoja anadai achangiwe. Je yule mswahili ambaye anapata mshahara wa tsh 400,000 kwa mwezi ana mke na watoto. Hana malupulupu, hana mbele wala nyuma. akiumwa inakuaje?

Twende mbele na kurudi nyuma. Joseph Haule si mtu wa kuchangiwa pesa ya matibabu. ni kutaka kutumia umaarufu wake vibaya. sisi watanzania tufikie hatua tuwe makini na watu wenye kufikiri kwa kina. Huyu bwana alipokuwa Mbunge miaka 5 aliwahi fikiria nini kuhusiana na gharama za matibabu?

Kama wenzie sasa hivi hawajali maumivu wanayopata watanzania wa kipato cha chini pengine kwa kudhani hayawahusu. But ipo siku pia nao yanaweza kuwakuta ni vyema kujipanga kwa mambo ambayo ukiwa mbunge na usipokuwa mbunge yanaweza saidia taifa hili.

Tuchangini wenye mahitaji ya kweli kweli ndugu zanguni. Prof J ana weza hata uza moja ya nyumba zake au lake. Ila wewe mwenzangu ukiumwa hutoweza jitibia wala kuchangiwa na watu sababu hufahamiki na huna cha kuuza.
Ndugu kutoa ni Moyo maana waswahili tunamsemowetu Bata ukemchunguza sana uwezi kumla
 
Kuna kijana toka Tanga alivunjika mkono akaletwa Muhimbili ili kufanyiwa operation alitakiwa laki nne na nusu tu. Familia haikua na hiyo hela. Alisota pale Muhimbili kulala chini wodi inanuka vidonda vya majeruhi wa bodaboda hata maji huwezi kunywea mle ndani.
Baada ya kukaa zaidi ya mwezi Alaina liwalo na liwe naenda kutibiwa nyumbani na waganga wa kienyeji. Kweli alittoroka Muhimbili na sasa mkono umepona japo sio kivile. Aliumia kipindi Cha serikali ya wanyonge.
Duh!!, Umasikini kitu Kibaya Sana.Wengi wanakufa kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu.
 
wako daily kwenye media: tv,nk, ila hupuuzwa, ila mwenye 500m+ kwa account ndiyo wa kwanza kujaziwa bakuli
upuuzi wa hali ya juu
Mwenye chake muungwana. Mtoaji ndiye huamua ampe nani na amnyime nani! Ninachokushauri: anzisha harakati, elimisha watu, kusanya michango kwa ajili ya hao unaoona wanastahili.
 
Familia imesema hawajashindwa kugharamia matibabu ila watanzania wenyewe mmelazimisha mnataka kumchangia kipenzi chenu Jay wa mitulinga, Jay tunakuzimia, mgodi unao tembea

Lakin jinsi inavyo tangazwa inanitisha sana inaonekana gharama zimewazidi sisi wananchi wa kawaida inawezekana tunakufa sana kwa kushindwa gharama za matibabu na siyo kwamba madkari wanashindwa
 
Prof Jay msanii ambaye ametuburudisha miaka mingi kwa nyimbo zilizojaa hekima tele uburudishaji pole sana kwa ugonjwa unaokusumbua. Hakika tusikae kuhukumu kuhusu kumchangia. Kwa sasa anaumwa na yanahitaji msaada. Tumchangie kwa kukumbuka kuwa Prof Jay ni binadamu kama sisi na kwa miaka mingi ameitendea vyema jamii yake kisanii.
 
Watu wa karibu wanasema sio kwamba hela hawana ila ni gesture tu kwasababu ni mtu wa watu.

Aahaah wapi mkuu, dogo wake wakishirikiana na mke wake walikiri mzigo wa matibabu umekuwa mkubwa hivyo wanahitaji huruma za watanzania wanyonge waweze kufanikisha hilo zoezi la jamaa kupewa matibabu..

Figo isikie mkuu, ikiwa comprimized sana inasababisha MOF, so guess what will be next?? Hapo ni coma then caput..
 
Back
Top Bottom