Mbunge Mstaafu na Mtu Maarufu anahitaji Mchango wa matibabu, wewe unadhani uta survive vipi?

Mbunge Mstaafu na Mtu Maarufu anahitaji Mchango wa matibabu, wewe unadhani uta survive vipi?

Ruge alikuwa anapigwa 6M daily jamaa wakawa wamepiga kimya ilipofika mzigo umegonga 650M ilibidi wafunguke tu kuwa mziki mnene jamani tunaomba mlioguswa tusaidiane😂!

Hao ni Clouds Media Group pamoja na viburi vyao vyote.
We nae tumekuchoka sasa...

Kila comment umeshupalia "6M"

Utadhani ulikua personal accountant wake!
 
Kuna Kocha mmoja juzi uingereza Wamemchangia £60,000 kwa ajili ya cancer ya ubongo ya mke wake. Mashabiki wa Crystal palace wamechanga. Sio kwamba huyu Kocha hana mshahara mkubwa ila kuna magonjwa mkuu hata kama una Hela ni gharama kuyatibu.

Hizi Issue za Figo kupigwa tu Laser Hospitali Nzuri hapa Tanzania unaambiwa milioni 12, Hapo bado Hela nyengine za kitanda na mambo mengine madogo madogo, na Hapo uombe Mungu isirudie kama Unarudi Rudi hospitali na Ugonjwa unakupelekesha muda Mrefu ndo Hapo unaona mtu anatembeza Bakuli.
Hapo Mhimbili kuna wagonjwa wanapigwa kalenda mpaka wanakufa bila kupata matibabu, kisa hawana hela. Hospitali mikoani watu wana kufa kwa kukosa hela za matibabu na hakuna anaejali. Kumchangia Jay si kuonesha mshikamano, ni kuonesha uozo wa mfumo wa bima ya matibabu Tanzania.
 
Dah jamaa hakujiwekeza freshy kwa 5 yrs, bila shaka jamaa alikuwa ni mtumishi wa wananchi hasaaa
 
Ruge alikuwa anapigwa 6M daily jamaa wakawa wamepiga kimya ilipofika mzigo umegonga 650M ilibidi wafunguke tu kuwa mziki mnene jamani tunaomba mlioguswa tusaidiane😂!

Hao ni Clouds Media Group pamoja na viburi vyao vyote.
Mbaya zaidi, hata baada ya efforts zote hizo na gharama zote hizo, inatokea kumpoteza mgonjwa kama ilivyokuwa kwa mwenzetu. Hakuna guarantee ya maisha.
 
Mbaya zaidi, hata baada ya efforts zote hizo na gharama zote hizo, inatokea kumpoteza mgonjwa kama ilivyokuwa kwa mwenzetu. Hakuna guarantee ya maisha.
Yeah inaonesha hio treatment sio suluhisho! Ni ku prolong siku tu
 
KILA SIKU NASEMA HAPA.
TUNADANGANYWA SANA NA HAWA WASANII. SIKU MOJA DIAMOND AKIUMWA NDIO MTAJUA UTAJIRI WAKE.
UGONJWA/KIFO NDIO MWISHO WA UDANGANYIFU.
 
Nimejiuliza hili swali sana si kwa nia mbaya. Kwa nia njema kabisa. Prof Jay. Joseph Haule amekuwa Mbunge kwa miaka 5 akilipwa mamimilioni ya pesa. Baada ya kumaliza kipindi chake amelipwa mamilioni mengine ya kiinuna mgongo.

Leo ameumwa na kulazwa kwa mwezi mmoja anadai achangiwe. Je yule mswahili ambaye anapata mshahara wa tsh 400,000 kwa mwezi ana mke na watoto. Hana malupulupu, hana mbele wala nyuma. akiumwa inakuaje?

Twende mbele na kurudi nyuma. Joseph Haule si mtu wa kuchangiwa pesa ya matibabu. ni kutaka kutumia umaarufu wake vibaya. sisi watanzania tufikie hatua tuwe makini na watu wenye kufikiri kwa kina. Huyu bwana alipokuwa Mbunge miaka 5 aliwahi fikiria nini kuhusiana na gharama za matibabu?

Kama wenzie sasa hivi hawajali maumivu wanayopata watanzania wa kipato cha chini pengine kwa kudhani hayawahusu. But ipo siku pia nao yanaweza kuwakuta ni vyema kujipanga kwa mambo ambayo ukiwa mbunge na usipokuwa mbunge yanaweza saidia taifa hili.

Tuchangini wenye mahitaji ya kweli kweli ndugu zanguni. Prof J ana weza hata uza moja ya nyumba zake au lake. Ila wewe mwenzangu ukiumwa hutoweza jitibia wala kuchangiwa na watu sababu hufahamiki na huna cha kuuza.
 
Familia ya Prof wala haikuomba Msaada na aliyeanzisha ni AYTz,
Lakin pia cha ajabu kipi Mbunge mstaafu kuchangiwa, Job alikuwa speaker na Bado serkali ndio ilitake over
 
Bima ya afya imekaa kitapeli sana hasa hii ya NHIF!

Magonjwa yote critical na yanayohitaji care kama za Dialysis wameyaondoa sababu yana gharama kubwa ila wameacha malaria ambayo kila mtu ana mudu!

Kawaida ya bima inatakiwa kundi la watoto na vijana libebe watu wazima wenye matatizo Mengi ila hali ni tofauti! Watoto wana options nyingi kuliko watu wazima ambao ndio wako Prone to sickness!
Bima dialsisi mbna wanacover.
 
Acha kabisa hio moment ya kusomewa mkeka wanaitwa wazee kwenda kuchukua taarifa za deni! Lazma warudi mwengine mkono kiunoni mwengine anaongea na simu 😂huku akipuputa jasho!
Wewe unapajua Mloganzila . Badala ya furaha mgonjwa amepona, vinaanza vikao, na muafaka usipoatikana fasta Deni linaongezeka maana jamaa amezuia kitanda.
Usiku mmoja pale Mloganzila ni zaidi ya hoteli nyingi Dar
 
Haumwi malaria au UTI au mafua ambapo matibabu yake angeliweza kuyahimili...

Anaumwa ugonjwa ambao hata ukiwa na "pesa kama alizonazo", itafika mahali utarudisha tu mpira kwa kipa...

All in all umaarufu unasaidia nyakati kama hizi...
Ugonjwa gani huo?
 
Wewe unapajua Mloganzila . Badala ya furaha mgonjwa amepona, vinaanza vikao, na muafaka usipoatikana fasta Deni linaongezeka maana jamaa amezuia kitanda.
Usiku mmoja pale Mloganzila ni zaidi ya hoteli nyingi Dar
Hio moment naielewa vyema sana, aunt yangu alifariki last year mwezi March. Alikuwa kwenye comma from Sunday to Friday akakata kauli! All that time alikuwa VIP pale.

Kimbembe kilikuja ku organise taratibu za kupewa mwili. Washua jasho liliwatoka 😅
 
Back
Top Bottom