Mbunge Musukuma asitake Kuhalalisha kuwa wenye Elimu ndogo wapendelewe, wasikilizwe sana na waonewe mno huruma na Watu kwa gharama ya kuwananga wasomi

Mbunge Musukuma asitake Kuhalalisha kuwa wenye Elimu ndogo wapendelewe, wasikilizwe sana na waonewe mno huruma na Watu kwa gharama ya kuwananga wasomi

Hapana. Relevancy ya wasomi unaowafikiria siyo tu anavyokusemesha ukikutana naye au akichangia Bungeni. Kwao hiyo ni ziada na kwetu ni bonus. Ukitaka kujua faida zao, soma maandishi yao. Yamejaa maktaba na serikalini na yanatumika sana kwa taarifa yako. Sana tu. Kisha, kwa ambao ni walimu, hebu angalia mchango wao wa kuelimisha taifa! Kwa upande wa michango kwa taifa, wa Musukuma ni kichuguu na wa Muhongo au wenzake kama Kimei ni Mlima Kilimanjaro!
 
Msomi kumjibu mtu kama msukuma itaamsha hasira za wajinga wengi sana. Yaani ni sawa na zile kelele za wanaopigania haki za wanawake. Haki za mtu kariba ya msukuma ina watetezi wengi sana.
Aisee kwani ni wengi mkuu
 
Hapana. Relevancy ya wasomi unaowafikiria siyo tu anavyokusemesha ukikutana naye au akichangia Bungeni. Kwao hiyo ni ziada na kwetu ni bonus. Ukitaka kujua faida zao, soma maandishi yao. Yamejaa maktaba na serikalini na yanatumika sana kwa taarifa yako. Sana tu. Kisha, kwa ambao ni walimu, hebu angalia mchango wao wa kuelimisha taifa! Kwa upande wa michango kwa taifa, wa Musukuma ni kichuguu na wa Muhongo au wenzake kama Kimei ni Mlima Kilimanjaro!
Mwerevu akienda nchi ya wajinga yeye ndiye huwa mjinga. Tz tujitathmini kama nchi. Ni nchi ya werevu au wajinga? Kwa nini werevu wakija Tz wanakuwa wajinga? Au kwa usahihi niseme tunawafanya wajinga! Muhongo mwamba katika miamba wa miamba kawa mjinga. Huyu bahati mbaya sana ana superiority complex balaa. Nikikumbuka Tido Mhando wa BBC alivyoanza kuleta mapinduzi tbc akaonekana mjinga! Tuna haja kabisa kama taifa kujitathmini.
 
Mimi ninachoamini mtu aliyesoma anajua vitu vingi vingi sana ambavyo hao wakina msukuma hawajui degree ni Elimu kubwa sana. Sijui wabunge wasomi Wanamuogopa kumjibu ndio maana anavimba kichwa na kuwa nanga, hakusoma tu akubali au arudi shule umri na umbo vinamruhusu.
Inferiority complex mzee hamna kingine. Nashangaa kale ka chama ka taasisi za juu kamekaa kimya tu. Yaani maprofesa wanatukanwa Afu kesho wanaingia darasani kutengeneza maprofesa zaidi?
 
Darasa lw saba ni wengi na ndo wenye mchango mkubwa katika uchumi na siasa hapa bongo kwahiyo ni haki kusikilizwa
 
Aisee kwani ni wengi mkuu
Yaani hawana idadi ndugu yangu... kwa hesabu za haraka chukua idadi ya wafuasi wa msukuma, jah people, kibajaji, mchungaji masanja mkandamizaji, mfalme zumaridi, kondeboy na wajinga wengine wenye ufuasi mkubwa halafu jumlisha ili upate picha ya uwingi wa watetezi.
 
Utamaduni wa kuonea aibu watu wajinga
Na kuwaacha waeneze ujinga wao hadharani
Hadi sasa wanaingia bungeni kwenda ongea
Upuuzi wao..ni utamaduni wa kipumbavu Sana....

Taifa linazidi kuwa Taifa la upumbavu wa halaiki.."mass embacilization"
chanzo cha tatizo ukikifahamu hutapanick badala yake utayatathmini mawazo yako ili kutengeneza solution ya kudumu yenye tija
 
Maneno mengi tena yenye kingereza kizuri hayatoshi kuonyesha ubora wako, bado kuna ziada kutoka kwako otherwise utabaki kama hao wasomi wasio na faida wanaowapa nafasi hao unao wachukulia poa waonekane mashujaa
 
Lakini pia haimaanishi kuwa basi kwakuwa hukubahatika kuwa na Elimu za Wastani ( Degree ) aliyonayo Generalist, ya Kati ( Masters ) aliyonayo @Sky Eclat na @Mmawia
Mmawia ana masters? Are you kidding me?!
Matusi na fyongo anazorusha humu jukwaani kila siku vinamtofautishaje na Msukuma? Kama wasomi wetu ndo aina ya akina Mmawia, basi mwacheni msukuma ajinafasi.
 
Hili jambo ni kweli umeshindwa tu kuliwasilisha vizuri. Lakini nadhani wasomi wamenyamaza sana kiasi Musukuma anataka kuhalalisha illiteracy yake ionekane ni jambo la kujivunia na kutweza utu na elimu ya wenye Elimu.

Mimi nina Degrees 3 but huwa sijitanabaishi katika Umma kwa kutangaza Degree zangu. Hili watu huliona kwenye utendaji napokuwa kazini au mambo ya kitaaluma popote napokuwepo.

Otherwise nabaki tu kama Chizi mwingine yeyote wa hapa JF na Tanzania au Duniani kwa Ujumla.
Ila pamoja na degrees zako tatu huwa unazingua sana kwa story zako za uongo halafu zisizoisha.
 
Bongo Vita sio umasikini ni kutambiana huyu kasoma huyu ajasoma huku umeme na maji yakiendelea kuwa changamoto...mkishasoma inatakiwa msahau ingieni field kutatua changamoto zinazotuzunguka kila kukicha msomi sio msomi mna tatizo gani wazee na mabibi..
 
Msukuma for Presdency 2025, twendeni na msukuma kwa nafasi ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa maendeleo ya kweli, Chagua ccm chagua Msukuma, tujenge Tanzania mpya.
 
Spika mwenyewe anaona ufahari kumuita kbs eti kundi la darasa la saba. Bunge hili wanadominate watu eti Sanga, KIbajaji na Mpush.
 
Unapomlaumu mtu kama Msukuma unamuonea hasa ikizingatia kuwa kwake ujinga ndiyo elimu na elimu ni ujinga. Kimsingi,wasomi wetu bungeni ndiyo wamewapandisha chati hawa mabunga. Onyesheni usomi muone kama watasikika. Simpo.
 
Back
Top Bottom