Mbunge Musukuma asitake Kuhalalisha kuwa wenye Elimu ndogo wapendelewe, wasikilizwe sana na waonewe mno huruma na Watu kwa gharama ya kuwananga wasomi

Mbunge Musukuma asitake Kuhalalisha kuwa wenye Elimu ndogo wapendelewe, wasikilizwe sana na waonewe mno huruma na Watu kwa gharama ya kuwananga wasomi

Shida siasa na wanasiasa ndio vinapewa heshima zaidi Tanzania. Wasomi wetu wanatafuta zote kuendeleza hii nchi lakini waekatishwa tamaa na siasa.
Msukuma na wenzie wametajirika si kwa uwezo wao bali wizi wa rasilimali na kukwepa kodi. Ulizeni mtapata hadithi zao leo wanajamba tu sababu ya loopholes za mifumo yetu. Nenda Arusha utaona wengi wa aina yake. Hovyo kabisa.
Wasomi turudishe heshima zetu. Tumekua na huruma sana na nchi hii. Tuna maslahi mengi ya kutendea Taifa hili.
VICHAA WAMEKIMBIA NA NGUO ZETU TUJIPANGE TUSIKIMBIE NAO.
 
Mwerevu akienda nchi ya wajinga yeye ndiye huwa mjinga. Tz tujitathmini kama nchi. Ni nchi ya werevu au wajinga? Kwa nini werevu wakija Tz wanakuwa wajinga? Au kwa usahihi niseme tunawafanya wajinga! Muhongo mwamba katika miamba wa miamba kawa mjinga. Huyu bahati mbaya sana ana superiority complex balaa. Nikikumbuka Tido Mhando wa BBC alivyoanza kuleta mapinduzi tbc akaonekana mjinga! Tuna haja kabisa kama taifa kujitathmini.
Tido case yake ni tofauti sana na Mhongo. Tido was a revolutionist pale TBC, tatizo alishindana na akina mzee Makamba walipotaka afanye ndivyo sivyo kwenye project ya uchaguzi ambayo TBC ilikuwa ishatengeneze na ilikuwa funded ili kuonesha midahalo ya wagombea ubunge.

Case ya Muhingo ni dharau kwa Watanzania. Fuatilia wizara ya madini na nishati pindi akiwa waziri; alikuwa hashauriki/haambiliki. Maana as long as yeye ni profesa aliwaona wengine wote "hamnazo". Hakuna anaetilia shaka vyeti vyake na ujuvi ailio nao kichwani. Ila pale inapofikia kuwachukulia poa Watanzania, hiyo haikubaliki.
Nyerere alikuwa msomi wa Master's kabla ya uhuru, yet aliweza kukaa na akina Kawawa, akina Mzee Mwinyi akina bibi Titi kwa staha na kuwaunganisha. Uwezo wake kimaarifa, fikra na exposure ulikwua juu sana, yet akajichanganya na Watanganyika na baadae Watanzania.

Muhongo is a different case, no wonder akina Musukuma wanamdharau. Mbona akina Prof. Mwandosya hawajawahi kutolewa maneno ya kejeli, simply walijua kuishi na watu vema. Kuna Prof. David Mwakyusa, alikuwa daktari bingwa na tabibu wa Mwl. Nyerere, he was down to earth. Ila Muhongo ni mtu wa aina yake.

Juzi kaja na takwimu za kukejeli mradi wa maji, kuna takwimu za kutosha duniani kwanini kuzalisha umeme kwa maji ni gharama nafuu na ndio maana uwekezaji unafanyika; sasa yeye kaja na data ambazo zinakinzana na wenzake woote.
Bila shaka ana akili, ila kama akili zake haziwezi kuwatumikia Watanzania basi haina maana.

Yesu akasema, yeye anaetaka kuwa bwana mkubwa, basi ashuke chini na kuwatumikia wengine.
 
Mimi ninachoamini mtu aliyesoma anajua vitu vingi vingi sana ambavyo hao wakina msukuma hawajui degree ni Elimu kubwa sana. Sijui wabunge wasomi Wanamuogopa kumjibu ndio maana anavimba kichwa na kuwa nanga, hakusoma tu akubali au arudi shule umri na umbo vinamruhusu.

Ukiona vichaa wanaongezeka kwenye ka mji fulani basi jua soon happy patakuwa jiji...tuliombee bunge letu.
 
Wenye elimu ndogo wapewe nafasi kuendesha nchi. Labda wako practical zaidi. Hawa wasomi wa kukariri wametuongoza toka uhuru lakini hakuna tulipofika. Haya maendeleo ni natural course tu ya mambo.
tangu uhuru msomi alikuwa nyerere tu na kambona. Kambona alikimbia akamuachia nyerere aongoze pekee msomi.. Tumefika hapa ajili ya mamburula walioitikia azimio la arusha kikasuku.
Jakaya alikuwa na wasomi wengi tukafika uchumi wa kati.

Jiwe alikariri madarasa tu. akachukia wasomi wenye uchumi wa kati .badala yake akawachomekea kwenye ubunge km huyu msukuma ili wasihoji uhalali wa kuijenga chato.

tumerudi nyuma sasa.

Ma mburula hawana soko tena ndo kina idd amini hao wanaendesha nchi kwa nguvu za kichawi kula nyama za watu ili wafikie malengo.hatutaki!!!!

Ukiona rais anateua drs la saba anataka kutawala milele.
 
Uko sahihi sana braza
Hayuko sahihi wasiosoma wanachuki.na vinyongo sana hata kwa level ya familia tu sana.popote chunguza. Wasipo kuchukia wewe sababu ya misaada unayotoa wanao watachukiwa mno.kuwa na baba msomi. Watoto Waki fail kidogo tu utaona ndg wenye chuki haoooo!!
"Nilijua tu wewe ni division zero tu!! Unaona??? Si nilikwambia??

Haya pasua paper ya marudio mpaka chuo kikuu! Weee!! Hutawaona wakija. utadhani wamekufa.
Tumbuliwa na jiwe tu!! hawa hapa...
 
Dawa ya kuwapunguza hawa kenge kwenye chombo mhimu cha kuwakilisha wananchi ni ku-set academic qualifications kwa mtu kugombea nafasi nyeti kama ya ubunge. Dunia imebadilika sana tunahitaji smart and focused mind kuwawakilisha wananchi. Ifike mahali hawa darasa la tatu A walisaidie taifa kalika nafasi nyingine. SIYO UBUNGE. Kwa mtizamo wangu hata mwenyekiti wa mtaa anapaswa angalau awe amehitimu kidato cha nne.
Ova.
Smartness and focused mind ipo kwenye academic qualification?
 
Huelewi hata kusoma wewe vepe??
Unakuzakuza mambo km mjinga flani hivi japo ulianza vizuri!!
Hakuna sehemu walisema wanadharau! bali

Wamemtia changa moto mbunge! na ndiyo adabu na sheria za mabunge yote Duniani.

Kwa akil zako finyu umeona ni dharau ile??

Yeye muongo akisema kitu ndo anavoamini!!Ndo maana ya kuwa pale km mbunge!!

Utamshauri nini mtu anae jua yuko sahihi?
Km wana kushauri una haki ya kukataa au kukubali sasa wewe unataka akubali tuu!!! Akikataa unaangalia kwa tamaa shule yake??

oooh! Ana dharau!!!
Wewe ndo unajidharau!!

kwanza muacheni siyo mpaka awe km jk nyerere na kawawa.
Nyie si ndo mlimuita nyerere majina ya kila aina eti
mchonga!! Mara
haambiliki!!!
Mara.....
Leo mnasema jk aliambilika. Vigeugeu ndi tabia zenu

Msituyumbishe!!!Ajili ya chuki binafsi!
size yenu jiwe ndo aliwaweza.kenge nyie msinijibu sitaki kuwasikiliza muache muongo achape kazi anavojua na kutaka. Punguzeni chuki si mkasome na nyie km ni rahisi???
 
tangu uhuru msomi alikuwa nyerere tu na kambona. Kambona alikimbia akamuachia nyerere aongoze pekee msomi.. Tumefika hapa ajili ya mamburula walioitikia azimio la arusha kikasuku.
Jakaya alikuwa na wasomi wengi tukafika uchumi wa kati.

Jiwe alikariri madarasa tu. akachukia wasomi wenye uchumi wa kati .badala yake akawachomekea kwenye ubunge km huyu msukuma ili wasihoji uhalali wa kuijenga chato.

tumerudi nyuma sasa.

Ma mburula hawana soko tena ndo kina idd amini hao wanaendesha nchi kwa nguvu za kichawi kula nyama za watu ili wafikie malengo.hatutaki!!!!

Ukiona rais anateua drs la saba anataka kutawala milele.
Wew upo kwenye kundi gani mkuu? La wasomi au darasa la saba?
 
Mkuu unajua kwanini wengi waliosima King Msukuma anawazalau?

Wengi wao ni masikini hawana hela, lakini msukuma hajasoma lakini anamiliki ukwasi wa maana tena inawezekana ameajiri hao wasomi.

Pili elimu siyo more practical hebu chukulia mfano mtu ameasoma Bussness administration lakini ameshindwa kuanzisha biashara ya aina yoyote, mtu amesoma Agriculture General lakini hana hata nusu heka ya shamba. Lakini hao ambao hawajasomq wanafanya hivi vyote bila kwanini wasiwazarau?
 
You are right;
Kimsingi watu wanaojitambua hueshimu watu wenye akili, akili Ni kile kinachobakia kichwani baada ya kuondoa elimu,Hawa watu wenye akili ndio waliovumbua elimu na ukitaka kujua akili Ni juu zaidi ya elimu jiulize mtu wa Kwanza duniani kupata degree alifundishwa na mtu mwenye elimu gani?
Kwa hiyo ukiwa na akili (whether una elimu au huna elimu) wanaojitambua watajua na watakuheshimu tu Wala hulazimiki kutumia msuli kulumbana
 
Wew upo kwenye kundi gani mkuu? La wasomi au darasa la saba?
Mkuu sina kundi mie! Ni Neutral gentlegirl msema kweli.
nawarekebisha wote wanao kosea ili waende sawa.
 
Back
Top Bottom