Mwerevu akienda nchi ya wajinga yeye ndiye huwa mjinga. Tz tujitathmini kama nchi. Ni nchi ya werevu au wajinga? Kwa nini werevu wakija Tz wanakuwa wajinga? Au kwa usahihi niseme tunawafanya wajinga! Muhongo mwamba katika miamba wa miamba kawa mjinga. Huyu bahati mbaya sana ana superiority complex balaa. Nikikumbuka Tido Mhando wa BBC alivyoanza kuleta mapinduzi tbc akaonekana mjinga! Tuna haja kabisa kama taifa kujitathmini.
Tido case yake ni tofauti sana na Mhongo. Tido was a revolutionist pale TBC, tatizo alishindana na akina mzee Makamba walipotaka afanye ndivyo sivyo kwenye project ya uchaguzi ambayo TBC ilikuwa ishatengeneze na ilikuwa funded ili kuonesha midahalo ya wagombea ubunge.
Case ya Muhingo ni dharau kwa Watanzania. Fuatilia wizara ya madini na nishati pindi akiwa waziri; alikuwa hashauriki/haambiliki. Maana as long as yeye ni profesa aliwaona wengine wote "hamnazo". Hakuna anaetilia shaka vyeti vyake na ujuvi ailio nao kichwani. Ila pale inapofikia kuwachukulia poa Watanzania, hiyo haikubaliki.
Nyerere alikuwa msomi wa Master's kabla ya uhuru, yet aliweza kukaa na akina Kawawa, akina Mzee Mwinyi akina bibi Titi kwa staha na kuwaunganisha. Uwezo wake kimaarifa, fikra na exposure ulikwua juu sana, yet akajichanganya na Watanganyika na baadae Watanzania.
Muhongo is a different case, no wonder akina Musukuma wanamdharau. Mbona akina Prof. Mwandosya hawajawahi kutolewa maneno ya kejeli, simply walijua kuishi na watu vema. Kuna Prof. David Mwakyusa, alikuwa daktari bingwa na tabibu wa Mwl. Nyerere, he was down to earth. Ila Muhongo ni mtu wa aina yake.
Juzi kaja na takwimu za kukejeli mradi wa maji, kuna takwimu za kutosha duniani kwanini kuzalisha umeme kwa maji ni gharama nafuu na ndio maana uwekezaji unafanyika; sasa yeye kaja na data ambazo zinakinzana na wenzake woote.
Bila shaka ana akili, ila kama akili zake haziwezi kuwatumikia Watanzania basi haina maana.
Yesu akasema, yeye anaetaka kuwa bwana mkubwa, basi ashuke chini na kuwatumikia wengine.