Mbunge Ntate: Wazazi Kuweni Makini na Malezi Hasa ya Watoto wa Kike

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum (Anayewakilisha Wafanyakazi Nchini) Anayetokea Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Janejelly James Ntate amewaasa wazazi na walezi kuwa makini na malezi ya watoto hasa watoto wa kike kwa kuwa watoto hao wapo hatarini sana kutokana na kukumbana na vishawishi vya kila aina tofauti.

Mhe. Janejelly James Ntate ameyasema hayo katika mahafali ya kidato cha nne yaliyofanyika Shule ya Sekondari ya Buyuni Zavala ambapo alialikwa kama mgeni rasmi.

Akizungumza na Wazazi na Walimu wa Buyuni, Mhe. Janejelly James Ntate ametaka pia wazazi wasipuuze malezi ya watoto wa kiume kwani hata nao wamekuwa wakiharibiwa sana na masuala ya unajisi na mtindo wa kisasa na kuwataka washirikiane na walimu kuhakikisha watoto wa jinsia zote wanafikia malengo yao.

Aidha, Mhe. Janejelly James Ntate aliahidi kuchangia idadi ya Viti 20, Meza 5 za Plastiki na Vyeti kwa ajili ya wanafunzi waliofanya vizuri kwenye usafi na taaluma.

 
Viform 4 vikimaliza tu vikaingia mtaani miez 6 mingi vinanepa na kunawiri manyangau lazima turuke navyo si sio wanafunzi tena
 
Kwani watoto wa kiume hawakutani na vishawishi? Huyu ni mjinsia tu hana lolote. Heri wasichana wapambane na vishawishi vya kuliwa kuliko warume kukumbana na hivyo hivyo
 
na watoto wenyewe waache viherehere,

Mtoto kutoka karume hadi msimbazi center hawezi kutembea, si Bodaboda anapita nae vizuri tu

malezi ni pamoja na ukakamavu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…