Mbunge Pauline Gekul atakiwa kufika Mahakamani Disemba 27, 2023 kujibu tuhuma dhidi yake

wanasheria wanisaidie hapa, hv kesi ya jinai mtuhumiwa huwa anatumiwa wito wa kufika mahakamani na mahakama?
Hii ni kesi ya jinai ambayo malalamikaji ni victim mwenyewe tofauti na jinai tulizo zoea ambazo malalamikaji ni Jamuhuri.
 
Mahakama ya Wilaya ya Babati imemtumia wito Mbunge Pauline Gekul kufika Mahakamani hapo Disemba 27, 2023 kujibu kesi inayomkabili.

Mahakama hiyo imemtaka kufika pasipo kukosa.
View attachment 2839748

Mbunge wa Babati Mjini (CCM), Pauline Gekul ameitwa mahakamani, kujibu tuhuma za kumshambulia na kumdhuru Hashim Ally, Novemba 11, mwaka huu, kinyume na kifungu cha 241 cha Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya mwaka 2022.

Wito huo uliotolewa leo Jumatatu, Desemba 11, 2023 na Mahakama ya Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara baada ya wakili Peter Madeleka kumfungulia kesi ya jinai Novemba 11, mwaka huu.

Kulingana na barua ya wito huo (Mwananchi tumeiona), iliyogongwa muhuri wa mahakama hiyo, Gekul anapaswa kuripoti mahakamani hapo Desemba 27, mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo ikitajwa.

Katika wito huo, mlalamikaji ni Hashim Ally dhidi ya Pauline Gekul.

Akizungumzia wito huo, wakili wa mlalamikaji, Madeleka amesema umekuja baada ya kufungua kesi ya jinai ya shambulio la kudhuru mwili. "Kwa wito huo kesi itaanza kusikilizwa Desemba 27."

Alipotafutwa kuthibitisha iwapo amepokea wito huo, Gekul amesema hakuona wala kuupokea.

"Sijaona, sijapokea wala sifahamu chochote kuhusu hilo," amesema Gekul ambaye Novemba 25 mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan alitengua uteuzi wake wa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria

Gekul anapokea wito huo, kipindi ambacho Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limewasilisha jadala la tuhuma zake katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa hatua zaidi.

Mzizi wa yote hayo ni tuhuma zilizoibuliwa na Hashim Ally, zilizosambaa mitandaoni akiomba msaada kwa watetezi wa haki za binadamu ili apate haki yake baada ya kufanyiwa ukatili na mbunge huyo.

Katika kipande hicho cha video, Ally alieleza ukatili aliofanyiwa unatokana na kile kilichodaiwa kuwa ameshiriki kuweka dawa za kishirikina katika eneo la kazi na sumu kwenye chakula.

Kijana huyo alieleza baada ya kukana hayo, mbunge huyo alimtaka avue nguo na kuingizwa chupa kwenye makalio.

Mbali na hilo, kijana huyo alieleza pia alitishiwa bastola na kupelekwa polisi.

Tayari Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetaka uchunguzi wa kina ufanyike juu ya tuhuma za mbunge wake na akithibitika kuhusika achukuliwe hatua za kisheria.

Pia soma: Peter Madeleka kusikiliza kesi ya Gekul mahakama ya Wilaya kwa tuhuma alizonazo dhidi ya Hamis
Janja janja ya serikali kulifunika suala.hili limejionesha hapo.

Jinai yeyote ni dhidi ya Jamhuri.

Sasa Iweje Hashim Ally nsiye aae mshtaki badala ya Jamhuri?

Serikali imeshawageuza wananchi wake misukule inawachezea itakavyo
 
Bora wee umenifungua macho, maana nilikua nashangaa au utaratibu umebadilika.
 
Mchezo wake pendwa alishauacha? Namkumbuka enzi zile. Kwenye sekta ile mtaalamu sana. Ndugu yangu Mkurugenzi Idara ya Wakimbizi miaka ile kafaidi sana walikutana wadau mchezo pendwa .
 
Mkuu hadi hakiza binadamu wamesimama nayo kazianayooo
Ukizingatia huko CCM alikuwa mgeni, na alikuwa ameziba nafasi za wafia chama, lazima atakomeshwa.

Angekuwa mfia CCM aliyekulia ndani ya CCM, maovu yote yangefunikwa. Si mnaona, mwenzake Makonda, licha ya jina lake kutajwa mara kwa mara kuhusika kwenye mauaji, utekaji watu, utesaji wa watu, uvamizi wa Clouds, mnaona anasumbuliwa na yeyote?

Gekul aliona wenzake wanafanya uovu mkubwa kama huo wa kuteka watu, hata kuua lakini hawaguswi wala kusumbuliwa, akaona kuwa kwa yeye kumkalishia kijana chupa, hawezi hata kuulizwa. Akasahau kuwa yeye ni mgeni aliyepewa tu hisani ya kula mema ya nchi lakini hajawa sawa na wenyeji wa uovu.
 
Mahakama ya Wilaya ya Babati imemtumia wito Mbunge Pauline Gekul kufika Mahakamani hapo Disemba 27, 2023 kujibu kesi inayomkabili.

Mahakama hiyo imemtaka kufika pasipo kukosa.
View attachment 2839748

Mbunge wa Babati Mjini (CCM), Pauline Gekul ameitwa mahakamani, kujibu tuhuma za kumshambulia na kumdhuru Hashim Ally, Novemba 11, mwaka huu, kinyume na kifungu cha 241 cha Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya mwaka 2022.

Wito huo uliotolewa leo Jumatatu, Desemba 11, 2023 na Mahakama ya Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara baada ya wakili Peter Madeleka kumfungulia kesi ya jinai Novemba 11, mwaka huu.

Kulingana na barua ya wito huo (Mwananchi tumeiona), iliyogongwa muhuri wa mahakama hiyo, Gekul anapaswa kuripoti mahakamani hapo Desemba 27, mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo ikitajwa.

Katika wito huo, mlalamikaji ni Hashim Ally dhidi ya Pauline Gekul.

Akizungumzia wito huo, wakili wa mlalamikaji, Madeleka amesema umekuja baada ya kufungua kesi ya jinai ya shambulio la kudhuru mwili. "Kwa wito huo kesi itaanza kusikilizwa Desemba 27."

Alipotafutwa kuthibitisha iwapo amepokea wito huo, Gekul amesema hakuona wala kuupokea.

"Sijaona, sijapokea wala sifahamu chochote kuhusu hilo," amesema Gekul ambaye Novemba 25 mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan alitengua uteuzi wake wa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria

Gekul anapokea wito huo, kipindi ambacho Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limewasilisha jadala la tuhuma zake katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa hatua zaidi.

Mzizi wa yote hayo ni tuhuma zilizoibuliwa na Hashim Ally, zilizosambaa mitandaoni akiomba msaada kwa watetezi wa haki za binadamu ili apate haki yake baada ya kufanyiwa ukatili na mbunge huyo.

Katika kipande hicho cha video, Ally alieleza ukatili aliofanyiwa unatokana na kile kilichodaiwa kuwa ameshiriki kuweka dawa za kishirikina katika eneo la kazi na sumu kwenye chakula.

Kijana huyo alieleza baada ya kukana hayo, mbunge huyo alimtaka avue nguo na kuingizwa chupa kwenye makalio.

Mbali na hilo, kijana huyo alieleza pia alitishiwa bastola na kupelekwa polisi.

Tayari Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetaka uchunguzi wa kina ufanyike juu ya tuhuma za mbunge wake na akithibitika kuhusika achukuliwe hatua za kisheria.

Pia soma: Peter Madeleka kusikiliza kesi ya Gekul mahakama ya Wilaya kwa tuhuma alizonazo dhidi ya Hamis
kesi ikisimamiwa na pita tu, ujue mambo yaishaisha hanna kesi apo...
 
Mahakama zipo kwaajili ya maskini basi. Huyo kwanza serikali haitaki kumshtaki ni Wakilia binafsi kaomba kuisimamia kesi.
 
wanasheria wanisaidie hapa, hv kesi ya jinai mtuhumiwa huwa anatumiwa wito wa kufika mahakamani na mahakama?

Hata ni maombi ya kuomba wakilia binafsi afungue mashtaka dhidi ya Gekul. Maana serikali imegoma kufungua jalada. Ni Kama inamkingia kifua Gekul. Imebidi raia wenyewe waingie mzigoni
 
Back
Top Bottom