Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Mkuu achatu yaaniHaki za bindamu ndio nini walioshindwa kwa sabaya bashite huyo ana kubwa gani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu achatu yaaniHaki za bindamu ndio nini walioshindwa kwa sabaya bashite huyo ana kubwa gani
👍Ngoja tusubiri haki itendeke
Inaweza kusuluhishwa nje ya mahakama ?! 😅Hakuna kesi hapo.
Kwa matajiri ndiyo pakoje?Kwa masikini kule
Hii ni kesi ya jinai ambayo malalamikaji ni victim mwenyewe tofauti na jinai tulizo zoea ambazo malalamikaji ni Jamuhuri.wanasheria wanisaidie hapa, hv kesi ya jinai mtuhumiwa huwa anatumiwa wito wa kufika mahakamani na mahakama?
Hii kisheria ipo? Jinai zote si zinaanzia polisi?Hii ni kesi ya jinai ambayo malalamikaji ni victim mwenyewe tofauti na jinai tulizo zoea ambazo malalamikaji ni Jamuhuri.
Janja janja ya serikali kulifunika suala.hili limejionesha hapo.Mahakama ya Wilaya ya Babati imemtumia wito Mbunge Pauline Gekul kufika Mahakamani hapo Disemba 27, 2023 kujibu kesi inayomkabili.
Mahakama hiyo imemtaka kufika pasipo kukosa.
View attachment 2839748
Mbunge wa Babati Mjini (CCM), Pauline Gekul ameitwa mahakamani, kujibu tuhuma za kumshambulia na kumdhuru Hashim Ally, Novemba 11, mwaka huu, kinyume na kifungu cha 241 cha Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya mwaka 2022.
Wito huo uliotolewa leo Jumatatu, Desemba 11, 2023 na Mahakama ya Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara baada ya wakili Peter Madeleka kumfungulia kesi ya jinai Novemba 11, mwaka huu.
Kulingana na barua ya wito huo (Mwananchi tumeiona), iliyogongwa muhuri wa mahakama hiyo, Gekul anapaswa kuripoti mahakamani hapo Desemba 27, mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo ikitajwa.
Katika wito huo, mlalamikaji ni Hashim Ally dhidi ya Pauline Gekul.
Akizungumzia wito huo, wakili wa mlalamikaji, Madeleka amesema umekuja baada ya kufungua kesi ya jinai ya shambulio la kudhuru mwili. "Kwa wito huo kesi itaanza kusikilizwa Desemba 27."
Alipotafutwa kuthibitisha iwapo amepokea wito huo, Gekul amesema hakuona wala kuupokea.
"Sijaona, sijapokea wala sifahamu chochote kuhusu hilo," amesema Gekul ambaye Novemba 25 mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan alitengua uteuzi wake wa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Gekul anapokea wito huo, kipindi ambacho Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limewasilisha jadala la tuhuma zake katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa hatua zaidi.
Mzizi wa yote hayo ni tuhuma zilizoibuliwa na Hashim Ally, zilizosambaa mitandaoni akiomba msaada kwa watetezi wa haki za binadamu ili apate haki yake baada ya kufanyiwa ukatili na mbunge huyo.
Katika kipande hicho cha video, Ally alieleza ukatili aliofanyiwa unatokana na kile kilichodaiwa kuwa ameshiriki kuweka dawa za kishirikina katika eneo la kazi na sumu kwenye chakula.
Kijana huyo alieleza baada ya kukana hayo, mbunge huyo alimtaka avue nguo na kuingizwa chupa kwenye makalio.
Mbali na hilo, kijana huyo alieleza pia alitishiwa bastola na kupelekwa polisi.
Tayari Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetaka uchunguzi wa kina ufanyike juu ya tuhuma za mbunge wake na akithibitika kuhusika achukuliwe hatua za kisheria.
Pia soma: Peter Madeleka kusikiliza kesi ya Gekul mahakama ya Wilaya kwa tuhuma alizonazo dhidi ya Hamis
Washamaliza Kazi acha asubir tu malipo yake ubunge kwishneyYaan matendoyao yanaleta npaka volkano
Ndo kitakacho kuwepo hapa.Hahaha ni mwendo wa kalenda njoo Jan njoo March njoo may familia zinakalishwa mhamala unasoma kesi closed...
Sio mtabiri lk n
Bora wee umenifungua macho, maana nilikua nashangaa au utaratibu umebadilika.Janja janja ya serikali kulifunika suala.hili limejionesha hapo.
Jinai yeyote ni dhidi ya Jamhuri.
Sasa Iweje Hashim Ally nsiye aae mshtaki badala ya Jamhuri?
Serikali imeshawageuza wananchi wake misukule inawachezea itakavyo
Ukizingatia huko CCM alikuwa mgeni, na alikuwa ameziba nafasi za wafia chama, lazima atakomeshwa.Mkuu hadi hakiza binadamu wamesimama nayo kazianayooo
kesi ikisimamiwa na pita tu, ujue mambo yaishaisha hanna kesi apo...Mahakama ya Wilaya ya Babati imemtumia wito Mbunge Pauline Gekul kufika Mahakamani hapo Disemba 27, 2023 kujibu kesi inayomkabili.
Mahakama hiyo imemtaka kufika pasipo kukosa.
View attachment 2839748
Mbunge wa Babati Mjini (CCM), Pauline Gekul ameitwa mahakamani, kujibu tuhuma za kumshambulia na kumdhuru Hashim Ally, Novemba 11, mwaka huu, kinyume na kifungu cha 241 cha Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya mwaka 2022.
Wito huo uliotolewa leo Jumatatu, Desemba 11, 2023 na Mahakama ya Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara baada ya wakili Peter Madeleka kumfungulia kesi ya jinai Novemba 11, mwaka huu.
Kulingana na barua ya wito huo (Mwananchi tumeiona), iliyogongwa muhuri wa mahakama hiyo, Gekul anapaswa kuripoti mahakamani hapo Desemba 27, mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo ikitajwa.
Katika wito huo, mlalamikaji ni Hashim Ally dhidi ya Pauline Gekul.
Akizungumzia wito huo, wakili wa mlalamikaji, Madeleka amesema umekuja baada ya kufungua kesi ya jinai ya shambulio la kudhuru mwili. "Kwa wito huo kesi itaanza kusikilizwa Desemba 27."
Alipotafutwa kuthibitisha iwapo amepokea wito huo, Gekul amesema hakuona wala kuupokea.
"Sijaona, sijapokea wala sifahamu chochote kuhusu hilo," amesema Gekul ambaye Novemba 25 mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan alitengua uteuzi wake wa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Gekul anapokea wito huo, kipindi ambacho Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limewasilisha jadala la tuhuma zake katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa hatua zaidi.
Mzizi wa yote hayo ni tuhuma zilizoibuliwa na Hashim Ally, zilizosambaa mitandaoni akiomba msaada kwa watetezi wa haki za binadamu ili apate haki yake baada ya kufanyiwa ukatili na mbunge huyo.
Katika kipande hicho cha video, Ally alieleza ukatili aliofanyiwa unatokana na kile kilichodaiwa kuwa ameshiriki kuweka dawa za kishirikina katika eneo la kazi na sumu kwenye chakula.
Kijana huyo alieleza baada ya kukana hayo, mbunge huyo alimtaka avue nguo na kuingizwa chupa kwenye makalio.
Mbali na hilo, kijana huyo alieleza pia alitishiwa bastola na kupelekwa polisi.
Tayari Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetaka uchunguzi wa kina ufanyike juu ya tuhuma za mbunge wake na akithibitika kuhusika achukuliwe hatua za kisheria.
Pia soma: Peter Madeleka kusikiliza kesi ya Gekul mahakama ya Wilaya kwa tuhuma alizonazo dhidi ya Hamis
wanasheria wanisaidie hapa, hv kesi ya jinai mtuhumiwa huwa anatumiwa wito wa kufika mahakamani na mahakama?