Pre GE2025 Mbunge Santiel Kirumba: Kila laini ikatwe Tsh. 50 tujenge barabara

Pre GE2025 Mbunge Santiel Kirumba: Kila laini ikatwe Tsh. 50 tujenge barabara

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mbunge wa Viti Maalum Santiel Eric Kirumba ameishauri Serikali kuweka makato ya Tsh. 50 kwa kila laini ya simu kwa ajili ya Mfuko wa Barabara (Road Fund) ili kuuwezesha kuwa na makusanyo yatakayowezesha ujenzi na ukarabati wa barabara Nchini.

Kirumba ameshauri hilo leo May 30,2024 wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2024/25 ambapo ameanza kwa kushauri mfuko huo kubuni njia mpya ya upatikanaji wa fedha.

“Tumekuwa tukisaini barabara mpya kila kukicha barabara kongwe hazipitiki na naendelea kusisitiza Road Fund iangalie chanzo kipya tumeona katika bajeti ya taknolojia na habari walisema laini ambazo ziko active ni milioni 72 sasa ni wakati wa kuona kama ni katika kupitia chanzo cha simu tunaweza kupata kwa kila laini Tsh. 50 ili iweze kuisaidia Road Fund na hili inabidi tuongee ukweli tatizo la kiuzalendo na tunapoendelea mbele tuangalie tunaisaidiaje Road Fund”

PIA SOMA
- Mbunge wa Gairo, Shabiby ataka fedha za bima kwa wote zikatwe kwenye laini za simu
Naunga mkono hoja,hakuna mjomba wa kujenga Nchi hii ,watu wanataka Barabara ila hawataki kuchangia pesa za ujenzi, unadhani pesa itashuka na mvua?
 
Naunga mkono hoja,hakuna mjomba wa kujenga Nchi hii ,watu wanataka Barabara ila hawataki kuchangia pesa za ujenzi, unadhani pesa itashuka na mvua?
Barabara ya Lindi haijaisha Ila full viraka Mbunge analalamika barabara Ina mashimo na HAPO bado haijaisha yaan ni sawa na kujaza maji kwenye Tenga nani achange, wachukue zile Pesa wanazotaka kuwapa wake wa viongozi million 20 kwa Mwezi kila mmoja
 
Hawataki kuchangia kivipi?
Tanzania kuna utitiri wa tozo kila mahali hadi petroli ni cheap Zambia kuliko Dar yenye bandari.

Tatizo ni wizi na ufisadi wa watawala
Nchi hii ni kubwa na Ina mahitaji mengi na usisahau ni Nchi ya 5 Kwa idadi ya watu Africa.

Hakuna shortcut lazima kuchangia tuu la sivyo Barabara zikiharibika tukae hivyo hivyo
 
Nchi hii ni kubwa na Ina mahitaji mengi na usisahau ni Nchi ya 5 Kwa idadi ya watu Africa.

Hakuna shortcut lazima kuchangia tuu la sivyo Barabara zikiharibika tukae hivyo hivyo
Kuchangia tayari kunafanywa, tena kwa kupitiliza kupitia utitiri wa tozo nyingi na kodi. Kuongeza tozo zingine juu ya zilizopo ni unyang'anyi na uporaji dhidi ya wananchi.

Wanaosema ccm imechoka wana hoja, wasikilizwe
 
Hawanaga ubunifu wa vyanzo vingine n makato ya laini ndo chanzo Cha maoato nchi hii mbona tuna watu wasio wabunifu😂🤣
 
Kuna watu wakishiba akili huwa haifanyi kazi kabisa
Unaweza ukakuta mtu mzima ila akifungua mdomo hata yeye hajui kaongea nini
Eti road fund
Kwani maskini anatumia barabara hizo

Bora wangeanza kulipa kodi ya barabara (Road Tax) na wenye mashangingi kama wao walipe 1m kwa mwaka, hakuna kumkomoa mchunga mbuzi kisa ana simu
Hebu muwe mnatumia hizo akili kwa maslahi ya nchi sio matumbo
 
Back
Top Bottom