Pre GE2025 Mbunge Santiel Kirumba: Kila laini ikatwe Tsh. 50 tujenge barabara

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mbunge wa Viti Maalum Santiel Eric Kirumba ameishauri Serikali kuweka makato ya Tsh. 50 kwa kila laini ya simu kwa ajili ya Mfuko wa Barabara (Road Fund) ili kuuwezesha kuwa na makusanyo yatakayowezesha ujenzi na ukarabati wa barabara Nchini.

Kirumba ameshauri hilo leo May 30,2024 wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2024/25 ambapo ameanza kwa kushauri mfuko huo kubuni njia mpya ya upatikanaji wa fedha.

“Tumekuwa tukisaini barabara mpya kila kukicha barabara kongwe hazipitiki na naendelea kusisitiza Road Fund iangalie chanzo kipya tumeona katika bajeti ya taknolojia na habari walisema laini ambazo ziko active ni milioni 72 sasa ni wakati wa kuona kama ni katika kupitia chanzo cha simu tunaweza kupata kwa kila laini Tsh. 50 ili iweze kuisaidia Road Fund na hili inabidi tuongee ukweli tatizo la kiuzalendo na tunapoendelea mbele tuangalie tunaisaidiaje Road Fund”

PIA SOMA
- Mbunge wa Gairo, Shabiby ataka fedha za bima kwa wote zikatwe kwenye laini za simu
jitu stupid kabisa. Yamejiongezea mamilioni mishahara, hilo halioni, takataka stupid bladifaken
 
Hata tozo ilianza hivihivi.

Hivi hii nchi ingekuwa vitani au tungekuwa na vikwazo vya kiuchumi ingekuwaje?
Umewaza kwa kina sana hata majanga ya kimbunga tu juzi tumeyatatua kwa ku dandia dandia tu, na wale wanauchumi wa bobezi hawana ushauri kwa serekali juu ya kuongeza pato kuliko hili la kuizikamata simu za wananchi? na jee kampuni za simu zikiamua kubadili biashara watatoa wapi hiyo hela walio iwazia kuichukuwa?
 
Mbunge wa Viti Maalum Santiel Eric Kirumba ameishauri Serikali kuweka makato ya Tsh. 50 kwa kila laini ya simu kwa ajili ya Mfuko wa Barabara (Road Fund) ili kuuwezesha kuwa na makusanyo yatakayowezesha ujenzi na ukarabati wa barabara Nchini.

Kirumba ameshauri hilo leo May 30,2024 wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2024/25 ambapo ameanza kwa kushauri mfuko huo kubuni njia mpya ya upatikanaji wa fedha.

“Tumekuwa tukisaini barabara mpya kila kukicha barabara kongwe hazipitiki na naendelea kusisitiza Road Fund iangalie chanzo kipya tumeona katika bajeti ya taknolojia na habari walisema laini ambazo ziko active ni milioni 72 sasa ni wakati wa kuona kama ni katika kupitia chanzo cha simu tunaweza kupata kwa kila laini Tsh. 50 ili iweze kuisaidia Road Fund na hili inabidi tuongee ukweli tatizo la kiuzalendo na tunapoendelea mbele tuangalie tunaisaidiaje Road Fund”
 
Naunga mkono hoja,hakuna mjomba wa kujenga Nchi hii ,watu wanataka Barabara ila hawataki kuchangia pesa za ujenzi, unadhani pesa itashuka na mvua?
Hakuna mtu anayekataa kuchangia maendeleo,lakini ukiangalia kuwa wabunge hawa ndiyo kila mwaka wanaletewa report ya CAG iliyojaa ubadhirifu lakini wanashindwa kutumia haki yao ya kikatiba kuibana serikali ili wabadhirifu wa kodi zetu wawajibishwe kazi yao ni kupiga makofi,vigelele na kukata mauno bungeni huku wakifurahia posho na mafao yao leo hii wanapoleta hoja tuzidi kukamuliwa inatia ukakasi kabisa. Tuna uhakika gani na matumizi sahihi ya hela hizo ikiwa hizo ambazo zimeshapangiwa matumizi zinafisadiwa kila mwaka?
 
Una uhakika? Mbona Serikali Huwa inatoa taarifa ya hatua ilizochukua? Au wewe unatakaje labda?
 
Hata tozo ilianza hivihivi.

Hivi hii nchi ingekuwa vitani au tungekuwa na vikwazo vya kiuchumi ingekuwaje?
Tungenyooka aisee. Bandari wamewapa waarabu halafu wametupandishia ushuru wa bandari na kufanya maisha yawe magumu halafu wanataka tena kutukamua hela kwenye simu? Qumer ya mama zao!
 
Ukinunua line unalipa mtandao unakatwa ushuru. Ukinunua vocha unakatwa, ukituma hela unakatwa, ukitoa hela unakatwa, ukinunua umeme unakatwa ya umeme na nyingine, tozo unakatwa…..

unakatwa unakatwa unakatwa “UNAKATWA”.

Screenshot_20240531-064238_X.jpg
 
wazo lako satiel Kirumba ni zuri sana lakini 50 x 20ml za laini zilizopo ni bilioni moja haijengi hata km 1 ya lami, lengo siyo wapiga kula kukusikia hata ktk mambo ya kipumbavu, hii inaweza kukupunguzia uhalali wa kurudi tena bungeni. kabla hujasema jambo lisikilize kwanza ndali yako kwa kifupi jifanye msikilizaji wa hoja yako uipime ina mashiko? na wakati mwingine unaweza tu kujifunza kuwa kimya miaka mitano yako ikiisha fanya shughuli nyingine, kama umekosa mchumba bungeni tafuta uraiani kuna vijana wengi wanahitaji kulelewa.
 
Back
Top Bottom