KUTATABHETAKULE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 5,159
- 5,070
Enzi zetu zile kwenye kila bajeti lazima Kodi iongezwe kwenye bia, sigara na vitu kama hivyo wenyewe wakiviita vya anasa. Baadae wananchi wakapata ufahamu kuhusu madhara ya pombe na pia tumbaku, wapunguza sana matumizi ya vitu hivyo. Matokeo yake mapato ya Kodi yaliyotokana na vitu hivi yakapungua sana. Kwa sasa baada ya kuona wananchi wengi wanatumia simu hizi za mikononi, Bunge limehamishia Kodi zake sehemu hiyo. Ujenzi wa shule, reli nk yote hayo yanategemea Kodi zitokazo huko. Wakumbuke hata hii itafika mahali watakwama. Wajitahidi kubuni vyanzo vingine bila kuumiza wengi wa wananchi.