Pre GE2025 Mbunge Santiel Kirumba: Kila laini ikatwe Tsh. 50 tujenge barabara

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuchangia tayari kunafanywa, tena kwa kupitiliza kupitia utitiri wa tozo nyingi na kodi. Kuongeza tozo zingine juu ya zilizopo ni unyang'anyi na uporaji dhidi ya wananchi.

Wanaosema ccm imechoka wana hoja, wasikilizwe
Nimekwambia Nchi hii ni kubwa na mahitaji ni mengi,hicho unachoita utitiri wa tozo ndio hakijatosha kujenga Barabara.

Sasa tuache au tujuchange tena? Leta jibu
 
Mbunge wa Viti Maalum Santiel Eric Kirumba ameishauri Serikali kuweka makato ya Tsh. 50 kwa kila laini ya simu kwa ajili ya Mfuko wa Barabara (Road Fund) ili kuuwezesha kuwa na makusanyo yatakayowezesha ujenzi na ukarabati wa barabara Nchini.

Kirumba ameshauri hilo leo May 30,2024 wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2024/25 ambapo ameanza kwa kushauri mfuko huo kubuni njia mpya ya upatikanaji wa fedha.

“Tumekuwa tukisaini barabara mpya kila kukicha barabara kongwe hazipitiki na naendelea kusisitiza Road Fund iangalie chanzo kipya tumeona katika bajeti ya taknolojia na habari walisema laini ambazo ziko active ni milioni 72 sasa ni wakati wa kuona kama ni katika kupitia chanzo cha simu tunaweza kupata kwa kila laini Tsh. 50 ili iweze kuisaidia Road Fund na hili inabidi tuongee ukweli tatizo la kiuzalendo na tunapoendelea mbele tuangalie tunaisaidiaje Road Fund”

PIA SOMA
- Mbunge wa Gairo, Shabiby ataka fedha za bima kwa wote zikatwe kwenye laini za simu
Ubwaa kabisa mbunge kilaza wa chama cha wezi....huwezi sikia wakiongelea posho zao kupungwa wao wako tu kupiga makofi
 
Wafanye utekelezaji wa wazo mapema kabisa mwezi wa Saba mwanzoni mwaka huu 2024.nipo tayari kuchangia mia 5 kwa kila laini yangu🥳🤔
 
Nimekwambia Nchi hii ni kubwa na mahitaji ni mengi,hicho unachoita utitiri wa tozo ndio hakijatosha kujenga Barabara.

Sasa tuache au tujuchange tena? Leta jibu
Ulishawahi kupitia ripoti za CAG?
Suluhisho ni watawala kuacha utapeli, wizi na ufisadi wa mali za umma.

Kujaribu kurundika tozo mpya juu ya tozo zilizopo bila kudhibiti wizi ni sawa na kujaza maji kwenye tenga.

Tozo zilizopo zinatosheleza mahitaji na kuzidi wizi ukidhibitiwa..
 
Nchi gani imedhibiti wizi hapa Duniani? Pili kwani wizi haudhibitiwi? Ripoti ya CAG imefanya nini?
 
Mbunge wa Viti Maalum Santiel Eric Kirumba ameishauri Serikali kuweka makato ya Tsh. 50 kwa kila laini ya simu kwa ajili ya Mfuko wa Barabara (Road Fund) ili kuuwezesha kuwa na makusanyo yatakayowezesha ujenzi na ukarabati wa barabara Nchini.

Kirumba ameshauri hilo leo May 30,2024 wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2024/25 ambapo ameanza kwa kushauri mfuko huo kubuni njia mpya ya upatikanaji wa fedha.

“Tumekuwa tukisaini barabara mpya kila kukicha barabara kongwe hazipitiki na naendelea kusisitiza Road Fund iangalie chanzo kipya tumeona katika bajeti ya taknolojia na habari walisema laini ambazo ziko active ni milioni 72 sasa ni wakati wa kuona kama ni katika kupitia chanzo cha simu tunaweza kupata kwa kila laini Tsh. 50 ili iweze kuisaidia Road Fund na hili inabidi tuongee ukweli tatizo la kiuzalendo na tunapoendelea mbele tuangalie tunaisaidiaje Road Fund”

PIA SOMA
- Mbunge wa Gairo, Shabiby ataka fedha za bima kwa wote zikatwe kwenye laini za simu
Wabunge wengi ni wajinga na wenye maarifa ya kuungaunga.
Ndiyo maana hawana ubunifu wa kupata pesa mbali na tozo za miamala ya simu.
Mfano kuntu wa hawa wajinga ni Mwigulu Nchemba.
 
Back
Top Bottom