residentura
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 8,146
- 11,434
Hilo ni kweli,mtu wangu wa karibu anahusika huko.Mbunge wa Gairo, Shabiby amesema kuna kampuni inalipwa kati ya sh bilioni 5 hadi 7 kila mwezi kwa kazi ya kuweka rangi kwenye mafuta yanayotumika nchini.
Shabiby amesema 'fee' hizo ni nyingi mno kulinganisha na kazi ndogo sana inayofanywa na kwamba kazi hiyo ingeweza kufanywa bure na TBS
Shabiby kasema kazi hiyo wamepewa kampuni binafsi ambayo inatupiga haswa.
Waziri wa nishati mh Kalemani alitoa taarifa kwamba mkataba wa kampuni hiyo ya kifisadi ulishasitishwa lakini Shabiby aliikataa taarifa hiyo na kusema hata jana aliiwaona watendaji wa kampuni hiyo wakiendelea na kazi hiyo ya kitapeli
Chanzo: ITV Habari
Ramadhan Kareem