Mbunge Sigrada: Kufeli Shule ya Sheria ni mkakati wa kisiasa wa kutokuzalisha mawakili wengi

Mkuu, kujadili hilo inahitaji reasoning sana. Ikiwa unaamini ripoti ya Dk. Mwakyembe kwa Law School bila shaka unaamini pia ripoti ya Jaji Chande kwa mauaji ya Oktoba 25.

Hao wawili wote ni wanasheria nguli nchini, mmoja akiwa amewahi kuhudumu kama Waziri wa Sheria na Katiba, mwingine kama Jaji Mkuu wa Tanzania.
Bado scenario za matukio mawili yote ambayo yamepelekea hizo ripoti hayalingani, kusema kuamini ripoti moja ni sawa na kuamini zote hutakuaa sahibi. Bado upo na mtazamo wa upande wa kisiasa, unachotaka kuonesha ripoti zote walikurupuka.

Ishu ya Law school nimewahi kuuliza waliyopita pale, ikiwemo baba yangu mzazi mwenyewe ambaye ni Wakili. Jibu nililopata kwa wote wa miaka ya nyuma hadi sasa, halina tofauti na ripoti ilivyosema.

Je ripoti ya Jaji Chande ina scenario ya namna hii?
 
Ungemuuliza mzee wako kama wanafunzi wanaofeli hapo LST baada ya matokeo kutoka huwa wanajua wamepata marks zipi na pia kama huwa wanapewa booklet zao walizojibia mitihani ili kukagua kama zilizahishwa kwa usahihi au kama maksi zilijumulishwa kwa usahihi, halafu majibu utayopata uyahusianishe na ripoti, na utajua kama ripoti ni halisi au ni za kisiasa
 
Booklet? Yaani mtihani unakuwa mbele ya majaji watano, unaulizwa maswali kwa mdomo na unatakiwa ujibu kwa mdomo hapohapo maswali ya majaji hao. Hiyo booklet unayozungumzia ni ya nini hapo? Nishaeleeza pale ni tofauti na vyuoni huko
 
Ungemuuliza mzee wako kama wanafunzi wanaofeli hapo LST baada ya matokeo kutoka huwa wanajua wamepata marks zipi na pia kama huwa wanapewa booklet zao walizojibia mitihani ili kukagua kama zilizahishwa kwa usahihi au kama maksi zilijumulishwa kwa usahihi, halafu majibu utayopata uyahusianishe na ripoti, na utajua kama ripoti ni halisi au ni za kisiasa
Mkuu sikia huo mtihani wao unavyokuwa, hakuna kuandika ni kujieleza. Sasa watahini wenyewe ni Jaji kiongozi, Mwanasheria mkuu wa serikali, Dean wa Faculty of Law na mawakili wawili.

Hao kila mmoja anatandika maswali matano na unatakiwa ujibu kwa kujieleza tu.
 
Mkuu, mimi ni wakili, nimesoma hapo LST. Achana na hizo story ulizoambiwa, hata kama aliyekuambia ni mzee wako, ni za kupotosha😀😀. Soma kwanza https://www.lst.ac.tz/uploads/documents/sw-1741078671-GN NO. 617 OF 2024 - THE LAW SCHOOL OF TANZANIA (EXAMINATION AND APPEALS) BY LAWS 2024.pdf ujue mitihani ipoje.
 
Back
Top Bottom