Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE SUMA FYANDOMO Alia na Barabara ya Mbeya, Ataka Mkandarasi Apewe Fedha kwa Wakati
"Nampongeza Waziri Bashungwa, anafanya kazi nzuri sana, anaitendea haki Wizara ya Ujenzi, endelea na moyo wako huo unaokutuma kufanya kazi za Watanzania, sina mashaka na wewe unafanya kazi kubwa sana. Mwenyezi MUNGU aendelee kukusimamia" - Mhe. Suma Ikenda Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya
"Barabara ya kwetu Mkoani Mbeya, tunaishukuru sana Serikali imemleta Mkandarasi na kuanza kazi. Wananchi wa Mkoa wa Mbeya tuna imani na matumaini makubwa sana Barabara itakwenda kukamilika"
"Mkandarasi alisaini tarehe 14 Februari 2023 na kutakiwa kukamilika 14 Aprili 2025 na mpaka sasa mmesema imekamilika kwa asilimia 14 lakini Wananchi wa Mbeya tuna mashaka kama kweli Barabara itakamilika"
"Awamu ya kwanza Mkandarasi aliomba Shilingi Bilioni 13.6 alikabidhiwa kwa wakati. Awamu ya pili aliomba Shilingi Bilioni 6.8 hajapewa, awamu ya tatu akaomba Shilingi Bilioni 4.3 alipewa Shilingi 4 pekee, awamu ya nne aliomba Shilingi Bilioni 2.8 hajapewa kabisa. Mkandarasi anahitaji fedha, hapewi kwa wakati, Barabara inakwenda kwa kusuasua ambayo inategemewa na Wilaya zote za Rungwe, Kyela, Mbarali, Mbeya Vijijini" - Mhe. Suma Ikenda Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya.